Kadi za Kieletroniki kwa usafiri wa Mabasi mwendo kasi kuanza kutolewa leo

Mi nimeelewa bt naongelea wale wasio na hata uhakika wa mlo wa kesho,,sembuse nauli!sasa hiyo 4500 ikishaisha kwa hizo safar nane watapata vp pesa za jumla kwa usafiri? hata kuongeza elf kumi wanashindwa.Si watarud kweny daladala tu
Tiketi za 650/- zipo pale pale. Hii kadi inawasaidia wale wenye kupanda bus kila siku wanaenda maofisini kwa mfano. Anajua anapanda siku tano kwa wiki hana sababu ya kupanga foleni kukata tiketi kila siku.
 
Wadau salio likiisha kwenye hii kadi unatumia utaratibu gani kurecharge.
Mkuu huku kwetu Ushirombo kuna machines maalum kwenye vituo vya mabasi, ambazo tunatumia Ku recharge salio kwenye card na pia tunaweza Ku recharge kwa kutumia ATM.
Hivyo, naamini huko mjini lazima wataweka machine kwaajili ya kuongezea salio
 
vilevile namna ya kuitunza isiharibike maana siku tatu tu utakuta haiwezi kutambuliwa na mashine mara imekunjwa kunjwa, imechubuka, n.k. Lakini kibaya zaidi ni kuibiwa na mateja wa jiji
Mkuu....
Ebu jaribu kua na mawazo chanya.
Hizi kadi ni sawa na kadi za Bank au kitambulisho, au leseni ya kuendeshea.
Hivyo........ kujikunja / kuharibika au kuibiwa ni kitendo ambacho sio cha kukusudia.
Muhimu ni kuitunza kadi yako kama unavyo tunza kadi zingine.
 
Nimenunua hio kadi yao aisee ni nzur na hata kwenye zile get zao inasoma fasta kuliko tiket... Ni nzur kiujumla ila zinahitaj maboresho kw mfano: kuangalia salio ni mpaka kituoni ila ingekua poa kama mtu ungekua unaweza ukaangalia salio hata kwa simu yako au kwa mtandao .. Yan kiufupi iwe na njia mbadala za kuangalia salio kama ilivyo kwenye kuongeza salio... Ni hayo tu
Well done mkuu
 
Hiyo kadi inauzwa bei ghali sana, mathalani kwa Mtanzania mwenye kipato cha chini asubuhi anaianza na jero mfukoni. Hizo kadi zingeuzwa buku tu, na credit zinunulike kirahisi kwa tigopesa, mpesa, halomoney na zingine bila matozo ya ziada.
Mkuu kadi mbona zinauzwa bei cheee tu sh 500
 
Vipi ikiwa itaibiwa mkuu?
Duuuh hapo ndo majanga kwa maana mpaka sasa hakuna kitu /doc yoyote ya kua ww ndo mmiliki wa hiyo kadi.. So ikiibiwa ndo imekula kwako.. Labda kama watarekebisha kwa kuzisajili kwa majina na namba za simu.. Ili watu wawe wanaweza kuacces kadi zao via phone numbers... Ila cjui kama kutakua na hayo marekebisho.. Tuombe Mungu na kuwapa support tu hawa jamaa naamin katika mifumo ya mawasiliano/computer hakuna lisilowezekana
 
Mi nimeelewa bt naongelea wale wasio na hata uhakika wa mlo wa kesho,,sembuse nauli!sasa hiyo 4500 ikishaisha kwa hizo safar nane watapata vp pesa za jumla kwa usafiri? hata kuongeza elf kumi wanashindwa.Si watarud kweny daladala tu
Kama huna hela sio lazima ununue kadi mkuu. Huduma ya tiketi itaendelea kama kawaida. Huduma ya kadi ni kuongeza ufanisi tu. Ukiona 5000 kubwa basi kila siku panga foleni ya kununua tiketi. Nadhani umeelewa
 
Nimenunua hio kadi yao aisee ni nzur na hata kwenye zile get zao inasoma fasta kuliko tiket... Ni nzur kiujumla ila zinahitaj maboresho kw mfano: kuangalia salio ni mpaka kituoni ila ingekua poa kama mtu ungekua unaweza ukaangalia salio hata kwa simu yako au kwa mtandao .. Yan kiufupi iwe na njia mbadala za kuangalia salio kama ilivyo kwenye kuongeza salio... Ni hayo tu
Naamini uliyoyasema ni ya msingi na wahusika bila shaka wanafanyia kazi suala hili.
 
Wale kina kajamba nani tunaotoka kimara had kivukon..Tukiamka tunasachi kibubu tunatoa mia tano,tukipapasa mfukoni nguo nlovaa jana nakutana na mia mbili..Mia saba hiyo naparamia kitu cha mwendo kas...Sasa hii budget ya kujaza credit nauli ya elfu thelathin kwenye hiyo kad niitoe wapi mie??
Wapande tu wafanya kazi mi narud kwenye daldala.
akili zako zinafanana na wewe
 
View attachment 358316
Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa leo katika juhudi za kupunguza msongamano wa kununua tiketi za karatasi.

Wauzaji wa tiketi hizo MaxMalipo na Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kitengo chake cha mradi wa mabasi yaendayo haraka wamesema tiketi hizo za kieletroniki zitauzwa katika vituo vikubwa kwa shilingi elfu tanio na mnunuzi atahitaji kusajil ili hata kama kadi yake itapotea akiba ya fedha iliyokuwa imebaki iingizwe kwenye kadi mpya atakayopewa.

Mkurugenzi mtendaji wa UdaRT, David Mgwassa amesema kadi hizo zitaanza kuuzwa kesho katika vituo vikuu vya mabasi vya Kimara, Ubungo, Morocco, Gerezani na Kivukoni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Afrika ambao ndiyo watengenezaji wa kadi hizo, Juma Rajab amesema bei ya kadi hiyo ni Sh 5,000 na itakuwa na Sh 4,500 ndani yake ambazo abiria anaweza kuzitumia kama nauli kwa safari nane.

Ameaema kadi hizo hazitakuwa na namba ya siri na kuwa kiwango cha juu kitakachowekwa katika kadi hiyo ni Sh30,000.
Moja kati ya miradi mizuri ikiwa na tija pamoja na manufaa kwa wananchi,
Pongezi kwa wote waliofanikisha hili kwa namna moja au nyingine ,
Awamu hii nayo iangalie kuwarahisishia maisha watanzania,iachane na kupoteza muda na maandamano ya chadema
 
Hahahaha kumbe hata shemegi unaweza kumpa akapandia gari
I 50th
View attachment 358316
Kadi za kieletroniki kwa ajili ya wasafiri wa mabasi yaendayo haraka katika jiji la Dar es Salaam zitaanza kutolewa leo katika juhudi za kupunguza msongamano wa kununua tiketi za karatasi.

Wauzaji wa tiketi hizo MaxMalipo na Shirika la Usafiri Dar es Salaam UDA kitengo chake cha mradi wa mabasi yaendayo haraka wamesema tiketi hizo za kieletroniki zitauzwa katika vituo vikubwa kwa shilingi elfu tanio na mnunuzi atahitaji kusajil ili hata kama kadi yake itapotea akiba ya fedha iliyokuwa imebaki iingizwe kwenye kadi mpya atakayopewa.

Mkurugenzi mtendaji wa UdaRT, David Mgwassa amesema kadi hizo zitaanza kuuzwa kesho katika vituo vikuu vya mabasi vya Kimara, Ubungo, Morocco, Gerezani na Kivukoni.

Kwa upande wake mkurugenzi wa kampuni ya Maxcom Afrika ambao ndiyo watengenezaji wa kadi hizo, Juma Rajab amesema bei ya kadi hiyo ni Sh 5,000 na itakuwa na Sh 4,500 ndani yake ambazo abiria anaweza kuzitumia kama nauli kwa safari nane.

Ameaema kadi hizo hazitakuwa na namba ya siri na kuwa kiwango cha juu kitakachowekwa katika kadi hiyo ni Sh30,000.
Safi sana I like it wacha Tanzania tuonekane kama ulaya
 
Vipi ikiwa itaibiwa mkuu?
ukiibiwa au kuipoteza utakuwa na access ya kui-block wewe mwenyewe kupitia simu ya mkononi ili aliyeokota asinufaike nayo.
Baada ya hapo utaenda ku-renew na salio lako litarudishwa.
Nilimsikia yule msemaji wa UDART akisema hiyo kadi unatakiwa kuisajili mwenyewe kupitia simu ya mkononi kwa kubonyeza namba fulani ili kurahisisha yote hayo.
 
Hiyo kadi inauzwa bei ghali sana, mathalani kwa Mtanzania mwenye kipato cha chini asubuhi anaianza na jero mfukoni. Hizo kadi zingeuzwa buku tu, na credit zinunulike kirahisi kwa tigopesa, mpesa, halomoney na zingine bila matozo ya ziada.
ukiangalia kwa undani kadi inauzwa 500 maana 4500 utazitumia kwa trip 6
 
ukiangalia kwa undani kadi inauzwa 500 maana 4500 utazitumia kwa trip 6
Uko sahihi, ni sawa na simu za tigo zinazotolewa BURE, lakini lazima ununue kifurushi cha elf20! Elf5 ni nyingi, wangegawa hizo kazi kwa jerojero tu then mtu ajaze kiasi anachotaka. Uswahilini maisha magumu ndugu yangu.
 
Habari wana jamii forum,

Naomba kwa wale wakazi wa Dar na ambao wanatumia mabasi ya mwendo kasi wanielimishe juu ya matumizi ya kadi maalum za mabasi hayo kwani mimi najiuliza abiria akishanunua hiyo kadi kwa elfu tano kama nimesikia sawasawa iyo bei, je akitaka kuingia katika hilo basi halipii tena, au vipi???

Na je hiyo kadi ni electronic katika matumizi au ni ya utambulisho tu? Pia watu wote wanauziwa hizo kadi au ni kundi maalum?? Pia napenda kufahamu waliouziwa wanakuwa wanazimiliki wao na huondoka nazo au wanaziacha hapohapo bada ya kupanda basi au wakati wa kushuka???

Ahsanteni sana!!
 
Back
Top Bottom