Kadi ya King'amuzi inaweza kufanya miamala?

nyumbamungu

JF-Expert Member
Mar 3, 2017
1,009
840
Naomba kujuzwa na wajuzi, upo uwezekano wa kutumia kadi ya King'amuzi kufanya miamala kama kuweka salio, kutuma na kununua kifurushi cha king'amuzi?

Nina uliza kwasababu mteja anaenunua king'amuzi kipya cha Azam anatakiwa aandike majina yake kamili, tarehe ya kuzaliwa na awe na namba ya kitambulisho cha Taifa "NIDA" sambamba na huo usajili kwa wateja wapya, kuna matangazo yanayoonesha Said Salim Bahresa Company Limited wapo mbioni kuanzisha kampuni ya huduma za kifedha "Azam Pesa"

Na kama kusajili majina, tarehe ya kuzaliwa na kitambulisho cha Nida ni sheria ya TCRA mbona kumpuni nyingine hawana huo utaratibu?
 
Back
Top Bottom