I think this is a very important point. Na pengine vyombo vyetu vya habari vingejifunza kuripoti habari za taasisi badala ya mtu, kwa mfano badala ya kusema Zitto alisema hivi, wangesema CHADEMA wasema hivi, hii itasaidia kukuza taasisi zaidi ya watu.
Hili nalo linaweza kuua chama, kumbukeni namna Makamba alivyosababisha mgogoro ndani ya CCM pamoja na wapambe wake akina Shaibu, Tambwe na Msabaha. CHADEMA waki-introduce hiyo system inaweza kuwa mtaji wa CCM kuwamaliza. Nina uhakika kila siku tutakuwa tunapata matamko ya watu mbalimbali yenye mtazamo tofauti na matokeo yake CCM wata-take advantage kwa kutwanga makombora kwamba chama kimoja lakini kinaongelea issue moja kwa mtazamo tofauti!
Kila taasisi lazima iwe na msemaji wake na ndiyo maana mtu kama si msemaji wa taasisi hutanguliza kauli kwamba hayo ni maoni yake binafsi, then anaendelea kutoa msimamo wake ambao kuna uwezekano ukawa tofauti na msimamo wa taasisi yake.
Hapa kitu muhimu ni kupata msemaji mmoja tu wa issues ambazo ziko sensitive ili iwe rahisi kumuwajibisha just in case akigundulika kwamba alichemsha. Lakini kama mtu si msemaji, politicians are very smart, watakuambia hayo yalikuwa ni maoni yangu binafsi na hivyo magazeti yalininukuu vibaya na kesi inakuwa imekwisha.
Kwa hiyo Wangwe na Zitto, pamoja na kusaka umaarufu, inabidi wapunguze kasi ya kusema na vyombo vya habari, vinginevyo jamii itawachoka haraka kama tulivyomchoka Makamba within a year or so! Magazeti yapo kwa ajili ya biashara japo primary goal ni kupasha habari, so hawa waheshimiwa wakae mbali nayo ili wasije wakatumika vibaya.