Robert Heriel Mtibeli
JF-Expert Member
- Mar 24, 2018
- 26,126
- 62,869
Habari za Jumapili,
Maisha sio Pouwa! Nakubaliana na wale wanaosema Maisha ni majaliwa. Na jitihada hazizidi kudura.
Wapo waliosoma kwa bidii mila hiyo na waliona taa ya matumaini kulingana na matokeo ya darasani waliyokuwa wakiyapata. Waliamini kuwa maisha yao na hatma yao ipo mikononi mwao kumbe sivyo.
Ilifika hatua wakawa wanadharau wale ambao walikuwa wanaonekana hawana mipango na mikakati kutokana na kutoipenda shule.
Wengi walifikiri kuwa kabla ya miaka 30 tayari wangekuwa wamekomesha jeuri na kiburi cha Umaskini katika maisha yao. Tayari kichwani walikuwa na picha za jumba kubwa la kifahari ambalo walijua ndio watakayoishi. Bongo zao zilishakuwa na miundombinu ya flyover ambapo gari yao ilikuwa ikipita juu yake huku ndani akiwa yeye na Pisikali moja matata ambayo ndio mkewe.
Kwa wasichana, wao nao walikuwa na maisha yao mazuri katika vichwa vyao. Wanaume Handsome, warefu na wenye vipato na Watanashati walikuwa katika fikra zao.
Sasa miaka imekimbia, hawaelewi nini kimetokea. Matumaini yameyoyoma, ngumi ya matumpa upper cut moja matata imepiga kidevu vijana chali. Hata zile ramani za majengo na magari walizokuwa nazo miaka hiyo zimefutika.
Yule Mwanamke mrembo akilini waliyemfikiria wangekuja kumuoa wanawaona kwenye magazeti, filamu na kwenye riwaya. Hakuna faraja tena, tumaini limeota mbawa. Wamejiunga kwenye chama cha faraja ya mpito cha Kataa Ndoa. Hawakumbiki tena ndoto ya kuwa na familia bora baada ya kuyapata maisha mazuri yanayotamanika. Ni Tekniko Knockout.
Hawakujua kuwa maisha yanakupa yale ambayo hujayaomba na yale ambayo huyataki. Tena maisha hukupa yale ambayo hukudhania kwamba ungekuwa nayo. Kwa sababu maisha ni Nasibu, maisha ni bahati tuu.
Sasa mipango imevurugwa na kuvurugika. Kila kitu pangala pangala! Hata kupanga hawataki kupanga tena. Hata wakisema wapange wanaona wanapoteza muda wao. Sasa ni bora liende túu! Wapo tayari kwa lolote na huo ndio mfumo wa maisha unavyotaka.
Mtu ambaye alipanga kabla ya miaka 30 awe na jumba na gari leo hii hata kodi ya chumba cha laki moja hawezi kuhimili. Unaweza kuona pigo alilopigwa ni zito kwa kiwango kipi.
Kijana, unapopanga mipango yako. Muombe Mungu
Suleiman aliwahi kusema;
Acha Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam

Mhubiri 9:11 NEN
Nimeona kitu kingine tena chini ya jua: Si wenye mbio washindao mashindano au wenye nguvu washindao vita, wala si wenye hekima wapatao chakula au wenye akili nyingi wapatao mali, wala wenye elimu wapatao upendeleo, lakini fursa huwapata wote.Acha Nipumzike sasa
Robert Heriel
Taikon wa Fasihi
Kwa sasa Dar es salaam