Kabla ya kuumba ulimwengu Mungu alikua anafanya nini?

Mpaka sasa kuna mabillion ya sayari lakini kile kifaa kinaitwa 'Kepler space craft' kishavumbua sayari kama 100 hivi ambazo zina size ya dunia na zenye uwezekano wa kuwa na maisha, wanaenda mbali zaidi na kusema kuna 'civilization' huko na ndio maana wanasisitiza kuwa 'we have been visited'.
Sielewi vizuri Quran inasema nini juu ya sayari zingine lakini kwenye Biblia Takatifu kuna sehemu Yesu alisema kuwa "Katika Nyumba ya Baba yangu kuna malimwengu (dunia) mengi" uthibitisho kwamba maisha hayako duniani tu.
Kama watu walioishi miaka 700 iliyopita waliamini kuwa dunia ndio kila kitu ni wazi watakaoishi miaka 600 ijayo wataweza kufanya maisha kwenye Mars au hata shemu nyinginezo!
nmeipenda comment yako mkuu
 
kama kweli mungu yupo Na yeye ndio aliuumba ulimwengu wote huu kwanini alishindwa kuandika kitu kidogo tu kitabu hadi binadamu waliamua kumuandikia
Na Wakati huo alisha kuwa amemaliza kazi ya kuumba ulimwengu. Na Alikua hana kazi.
mwisho utasema alishindwa jenga makanisa na misikiti ikajengwa na watu,au alishindwa umba watoto badala yake wanawake wanazaa
 
"Hapo mwanzo mungu aliumba mbingu na nchi" na tumefundishwa Mungu hana mwanzo.

Sasa kabla ya kuumba ulimwengu mungu alikua anafanya kazi gani?
Kabla ya mwanzo Mungu aliumba vitu vingine tofauti na mbingu na nchi, na vilivyomo.
 
hebu fikria unatokewa na mtu alokuumba na kuumba sayar zote na ulimwengu naskia zamn ilikuwa ni rahsi sana kuonana MUNGU sio sasa
 
uongo!!!! umesikia kwa nani?
mkuu hata MUSA alikuwa akipiga story mara kwa mara na MUNGU hvyo hvyo hata kwa wana waisrael kulikuwa na siku maalum nmesahau ni sehemu gan katika bible but ipo huyo mistar
 
KWA KUANZIA, Kwa sababu umeanza kwa ku quote maandiko ya bibilia tutakujibu kibiblia pia, ila kama ungeuliza kikawaida tungejaribu kukujibu kikawaida ( kimwili au sayansi ya kufikirika).
longi mapexa ametoa mchango mzuri kabisa ila kuongeza. Mungu ni roho, yeye ahijali physical world in kuweza ku exist,
biblia inaposema hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi ( Mwanzo 1:1) biblia inazungumzia mwanzo wa physical universal na earth ( mbingu sio mbinguni its universal na nchi ni earth). ukiangalia katika mstari wa 14 Mungu akatengeneza nyota, mstari wa 16 akafanya jua na mwezi.

Ok !! ukiangalia katika uumbaji hapa hakuna mahali Mungu anaongelea kuhusu malaika, lakini walikuwepo. Kama nilivyo sema kuwa Mungu ni Roho, na malaika pia ni Roho , wao hawahitaji physical universal ili kuwepo, kwahiyo dunia na universal viliubwa au vilipewa mwanzo kwaajili ya physical being ( viumbe hai). Kwa hiyo kabla ya kuumbwa au kabla ya kuwepo dunia yetu na anga na vilivyomo, Mungu alikuwepo na malaika walikuwepo.

OK! Alikuwa anafanya nini? Kazi kubwa ya malaika ni kumwabudu Mungu kama alivyochangia Usedcountrynewpipo , swali kwanini Mungu alimuumba Mwanadamu? Mungu alimuumba mwanamu ili mwanadamu amwabudu Mungu.

mkuu TECHMAN,hapo kwenye mstari wa 14 ktk kitabu cha MWANZO 1.

JE unaijua tofauti ya jua na nyota mkuu??Haiwezekani aumbe nyota then baadae aje aumbe jua na mwezi wakati kimsingi jua nayo ndio nyota

OK!! kuhusu swali lako, Je unakataa bibilia ilichoandika? ndo maana nikaweka na maandiko kabisa, Ukiangalia nilivyo anza, nimesema kwakuwa ameuliza kibiblia namimi najibu kibiblia,

OK!! Embu soma tena mstari wa 14 na 16, Mungu aliposema pakuwe na mianga, pakakuwa na mianga mingi na katika mianga hiyo palikuwa na mianga miwili mikubwa, Mwanga mkubwa mmoja ukapewa kutawala usiku na mwingine kutawala mchana. sikumaanisha kuwa Mungu aliumba mianga mingine kisha baadae akaja kuumba Jua na mwezi, katika mstari wa 14, anasema " Na iwe mianga katika anga la mbinguni" hapa anamaanisha minga yote, lakini katika hiyo kulikuwa na mianga mikuu miwili.

Jua na mwezi. katika mstari wa 16 anaipatia mianga mikubwa miwili majukumu.
 
Hakuna kitu kinachoitwa mungu kilichoiumba dunia. Shitukeni mnaibiwa
Mkuu inawezekana kabisa ukawa sahihi, lakini hapa sio mahala pake, Hapa tunajadili biblia inasemaje kuhusu jambo hili.
Na wewe jaribu kuanzisha uzi kama huu kwa mtazamo wako kisha tukupe mchango maridhawa kuhusu unacho amini.
 
Usiogope challenge kwa kile unachokiamini. Ubovu wenu mnakuja na hoja za kunukuu badala ya uwezo wenu binafsi wa kufikiri
 
Usiogope challenge kwa kile unachokiamini. Ubovu wenu mnakuja na hoja za kunukuu badala ya uwezo wenu binafsi wa kufikiri
Sikia dogo nusuhela , nimesema nachangia kutokana na mlata mada, sasa kama wewe una mtazamo mwingine aanzisha uzi kuhusu unacho amini tutiririke utakavyo.
 
Mkuu maliedo sasa hivyo viumbe vya sayari nyingine vikitudiscover vitatufanya nini?
 
KWA KUANZIA, Kwa sababu umeanza kwa ku quote maandiko ya bibilia tutakujibu kibiblia pia, ila kama ungeuliza kikawaida tungejaribu kukujibu kikawaida ( kimwili au sayansi ya kufikirika).
longi mapexa ametoa mchango mzuri kabisa ila kuongeza. Mungu ni roho, yeye ahijali physical world in kuweza ku exist,
biblia inaposema hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi ( Mwanzo 1:1) biblia inazungumzia mwanzo wa physical universal na earth ( mbingu sio mbinguni its universal na nchi ni earth). ukiangalia katika mstari wa 14 Mungu akatengeneza nyota, mstari wa 16 akafanya jua na mwezi.

Ok !! ukiangalia katika uumbaji hapa hakuna mahali Mungu anaongelea kuhusu malaika, lakini walikuwepo. Kama nilivyo sema kuwa Mungu ni Roho, na malaika pia ni Roho , wao hawahitaji physical universal ili kuwepo, kwahiyo dunia na universal viliubwa au vilipewa mwanzo kwaajili ya physical being ( viumbe hai). Kwa hiyo kabla ya kuumbwa au kabla ya kuwepo dunia yetu na anga na vilivyomo, Mungu alikuwepo na malaika walikuwepo.

OK! Alikuwa anafanya nini? Kazi kubwa ya malaika ni kumwabudu Mungu kama alivyochangia Usedcountrynewpipo , swali kwanini Mungu alimuumba Mwanadamu? Mungu alimuumba mwanamu ili mwanadamu amwabudu Mungu.

Hv kweli roho inaweza kufanya hayo uliyoyataja???? Be serious bro
 
Mungu Hana Mwanzo wala Mwisho hivyo huo Mwanzo ni yeye aliyeuanzisha na Mwisho wa Dunia pia anaujua yeye lakini aliapa kuwa hapatakuwa tena na Wakati(Mwanzo na Mwisho) baada ya huu kwani walio wake watakuwa pamoja naye kwenye umilele

Mkuu unajichanganya mara useme hana mwanzo wala mwisho alafu unasema tena yy ndo ameuanzisha mwanzo. Alafu unasahau Kila chenye mwanzo kina mwisho
 
Mkuu unajichanganya mara useme hana mwanzo wala mwisho alafu unasema tena yy ndo ameuanzisha mwanzo. Alafu unasahau Kila chenye mwanzo kina mwisho
Aliuanzisha Mwanzo wa Ulimwengu na huu Ulimwengu una mwisho wake usipokuwa yeye mwenyewe Hana mwisho.
 
Swali jingne Kabla ya kuumba mbingu alikuwa anaishi wap?

Yapo mambo mengi sana unayoweza kuuliza na usipate jibu la moja kwa moja,mf hakuna anayejua siku yake ya kufa,labda aliyehukumiwa kifo,hakuna ajua kesho kitu gani kinatokea. Mungu alitupa uwezo mdogo sana wa ufahamu inaweza kuwa 1/1000000 ya anachojua Mungu,biblia takatifu inasema katika Kumbukumbu la torati 29:29 Amini Mungu yupo na kwa yeye vitu vyote vilifanyika
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom