Kabla uchaguzi kufanyika Marekani.Yatajwa kuna njama za kumuua Trump.Aongezewa ulinzi.Naye asema ataifuta Iran kwenye uso wa dunia.

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
8,271
13,178
Dunia itaendelelea kuwa sehemu ambayo si salamu kwa watu kuishi kwa utulivu muda wote ambao Marekani na Israel zitaendelea kuwa washirika wa karibu.
Hivi karibuni kulifanyika jaribio la kumuua mgombea uraisi wa Marekani na ambaye amewahi kuwa rais,bwana Donal Trump.Jaribio hilo lilifanywa na raia wa kimarekani asiye na asili ya nje ya taifa hilo.
Cha ajabu ni kuwa baada ya Trump kuponea chupu chupu kufa na bila kutolewa ufafanuzi wa kutosha kuhusu shambulio hilo.wiki moja tu mbele vyombo vya usalama vya nchi hiyo vimesema kuna njama za kutaka kumuua Trump zinazofanywa na Iran na hivyo kumuongezea ulinzi mgombea huyo.
Katika mkutano wake na Benjamin Netanyahu hapo juzi kwenye makao yake ya MarLago, kwanza Trump alimshutumu anayetarajiwa kuwa mgombea mwenzake kutoka chama cha Democratic,bibi Kamala Harris kuwa anawachukia wayahudi.
Baada ya kutoa tamko hilo,Trump akafoka kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa kijamii kuwa iwapo Iran itamuua yeye basi na Marekani haitakaa kimya kwani wataifuta Iran kwenye uso wa dunia.
Vitu vya kutunga na kufikirika tu ndivyo vianaifanya Marekani kufanya uhasama na mataifa mengi duniani na kupoteza rasilimali zake nyingi kwa ajili hiyo.
Hata hivyo ubabe na vituko hivyo mara nyingi huwa inavifanya kwa mataifa madogo na manyonge na si kwa wababe wenzake kama vile Korea Kaskazini,Taliban,Vietnam,Uchina na Urusi.

Trump discusses US wiping Iran 'off the face of the Earth'

Umasikini ni mbaya na haufai, Maendeleo nayo ni vita tupu na walioendelea!

Sjiui bora nini??
 
Hakuna rais marekani mwenye kheri na waislamu, tangu lini kafiri akawa rafiki wa kweli kwa Muislamu! Ukiona hivyo basi kwa maslahi tu.

Bush
G.W.Bush
Obama
Trump

Hawa wote hawafai, utaongeza na wewe
 
Dunia itaendelelea kuwa sehemu ambayo si salamu kwa watu kuishi kwa utulivu muda wote ambao Marekani na Israel zitaendelea kuwa washirika wa karibu.
Hivi karibuni kulifanyika jaribio la kumuua mgombea uraisi wa Marekani na ambaye amewahi kuwa rais,bwana Donal Trump.Jaribio hilo lilifanywa na raia wa kimarekani asiye na asili ya nje ya taifa hilo.
Cha ajabu ni kuwa baada ya Trump kuponea chupu chupu kufa na bila kutolewa ufafanuzi wa kutosha kuhusu shambulio hilo.wiki moja tu mbele vyombo vya usalama vya nchi hiyo vimesema kuna njama za kutaka kumuua Trump zinazofanywa na Iran na hivyo kumuongezea ulinzi mgombea huyo.
Katika mkutano wake na Benjamin Netanyahu hapo juzi kwenye makao yake ya MarLago, kwanza Trump alimshutumu anayetarajiwa kuwa mgombea mwenzake kutoka chama cha Democratic,bibi Kamala Harris kuwa anawachukia wayahudi.
Baada ya kutoa tamko hilo,Trump akafoka kwenye akaunti yake ya mtandao wake wa kijamii kuwa iwapo Iran itamuua yeye basi na Marekani haitakaa kimya kwani wataifuta Iran kwenye uso wa dunia.
Vitu vya kutunga na kufikirika tu ndivyo vianaifanya Marekani kufanya uhasama na mataifa mengi duniani na kupoteza rasilimali zake nyingi kwa ajili hiyo.
Hata hivyo ubabe na vituko hivyo mara nyingi huwa inavifanya kwa mataifa madogo na manyonge na si kwa wababe wenzake kama vile Korea Kaskazini,Taliban,Vietnam,Uchina na Urusi.

Trump discusses US wiping Iran 'off the face of the Earth'

Propaganda tu za watu wansotafuta kura za huruma.
 
Back
Top Bottom