Kababaye Mwanaume ndiii

Masia motee....iyeye juju ye.....masia mote.......
Hapa tunaweza kutana ma age mate wengi sana.....
 
Kababayee yee na maasia mote! Dah wadau mnenikumbusha kijenge primary 1989,nakumbuka masia mote aliwahi kutoa yai kwenye kwapa la mshkaji.
 
Mi namkumba Hamishi Nyaloo yule kichaa hatari sana, alitusumbua sana Arusha enzi hizo,ukisikia Hamisi nyalooo hugeuki ni mbio balaa.
Hamisi nyaloo alikuwa noma, maeneo yake yalikuwa kuanzia clock tower, bank ya nbc uhuru na Chinese restaurant, kulikuwa na jimmy ila yeye hakuwa violent
 
kababa nibebe eyaa eyaa... nomaa sana miaka iyo mwereni primary alitisha alikuwa anabeba magunia ya mahindi kwa mdomo dah
 
Wakazi wa arusha hivi mnamkumbuka mwanamazingaumbwe aliekua anaitwa kababaye miaka ya nyuma?

Nakumbuka miaka ya nyuma alivuma sana mashuleni kiingilio ilikuaga mia mbili.

Akitaka kufanya mauza uza anasema kababaye mnaitikia yee, anasema mwanaume ndi mnaitikia ndii, mwanaume ndaa, ndaaa.

Kwa anae mkumbuka atueleze yupo wapi sikuhizi.
Hahaha umenikumbusha mbali sana na jamaa mwingine alikuwa akiitwa masiamoteee sema tena masiamoteee ila kipindi hicho kiingilio ilikuwa sh 5 hadi sh 10 nakumbuka ile sh. 10 ya noti ya kijani ilikuwa bado inatumika sijui hao watu wameishia wapi? kwa kumbukumbu wengine ni mwanamuziki chimbende, mcheza ngoma marehemu minyigu na wengine wengi ,power mabula huyu nafikiri alikuwa akitokea mwanza,timu ya waya mkali
 
Kababayee yee na maasia mote! Dah wadau mnenikumbusha kijenge primary 1989,nakumbuka masia mote aliwahi kutoa yai kwenye kwapa la mshkaji.
Masiamote alishawahi kupika pilau bila jiko wala mchele,nyama na viungo vya pilau ,daah mazingaumbe noma nakumbuka ilikuwa mida ya saa nane mchana watu tuna ubao alafu ukifikiria kipindi hicho pilau tulikuwa tunakula sikukuu hadi sikukuu lakini wanafunzi tuligoma kula pilau la masiamotee tena lilikuwa na kachumbari aisee yule jamaa alikuwa noma,sasa si akaamua kulila lile pilau alafu hakulimalizia akafanya tena mazingaumbwe likatoweka
 
Nakumbuka kipindi hicho mazingaumbwe yalikuwa yakifanyika ijumaa baada ya vipindi basi ikifika jumatatu siku nzima ni kusimuliana habari za mazingaumbwe daaah tumetoka mbali sana
 
Halafu kulikuwa na mtu akiitwa maasia mote anaambatana na mtu akiitwa juju ye.akianza mambo yake anasema ni yeye juju ye,watu ye.ghafla mshikaji akaharisha lundo la sarafu zimejaa sufuria ndogo ndogo.dah wakati huo bwana.
Aisee jamaa angu umenikumbusha arushaaa enzi hizo jombaaa masiamoteeee
 
Mwingine maarufu alikuwa anaitwa MASIAMOTE huyu nae alitamba mnoo wakati wake
 
Mimi namkumbuka power mabula enzi hizo shule ya msingi Ngudulugulu Kwimba,Mwanza
 
Mimi namkumbuka power mabula enzi hizo shule ya msingi Ngudulugulu Kwimba,Mwanza
Power Mabula ni mchungaji siku hizi amefungua kanisa la walokole olmatejo Arusha .Ila amekauka yupo kawaida tuu .body sio kama zama zake .
 
Hahaaah kababayee... Meru primary,. Hamis nyaloo na jimmy kichaa Kuna mmoja sjui alikua anaitwa Hamisi majikooo alikua anapenda kukaa pale pembeni na kaloleni hospitali
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom