Kama wanaongelea kufuata sheria, na wanasisitiza hivyo, basi Jeshi linapaswa kuwa mfano wa kufuata hizo sheria. Kwa kuanzia waanze kwa kupeleka malalamiko yao Polisi.
Polisi ndiyo wenye mamlaka ya kufuatilia hilo, waachane na jungle minds, zama zimebadilika hizi wanapaswa kujua majukumu yao yanapoishia. Tunalipenda na kuliheshimu Jeshi letu, so linapaswa kutambua misingi, sheria kanuni na mipaka ya majukumu yao.
Kwa Jeshi kupeleka malalamiko yao Polisi, siyo unyonge, bali itadhihirisha kuwa ni Jeshi linalojitambua, na linalotambua majukumu yake na ya wengine, na mipaka yake, zaidi itaibua hali ya Wananchi kufuata sheria na kwamba kumbe kufuata sheria siyo unyonge au utumwa bali ni ustaarabu na kujitambua.
Nguvu za hizi taasisi zinaundwa kutokana na sheria. Uhamiaji ilikua ni idara tu, sasa hivi baada ya muswada kupitishwa na kuwa sheria, Uhamiaji hivi sasa ni Jeshi kwa mujibu wa sheria iliyoliunda, na kuna sheria zinazoelekeza aina ya silaha wanazopaswa kutumia wawapo kazini, pia wanazoruhusiwa kuwa nazo popote hata majumbani.
Sheria ndiyo inaelekeza aina ya mafunzo gani yatolewe kwa Jeshi lipi, siyo kwa sababu labda Jeshi fulani ni noma kuliko lingine.
Sheria ikibadilishwa inaweza kupelekea JW inakua Polisi na Polisi wakawa JW. Tuachane na jungle minds, those days are long gone.