JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,696
- 6,491
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) limebainisha hatua hiyo inatokana na ongezeko la raia wanaotumia mavazo hayo wakikinzana na Sheria ya Ulinzi wa Taifa, Sheria ya Taifa na Sheria ya Kanuni ya Adhabu zinazokataza raia kuvaa au kutumia mavazi ya Kijeshi au yanyoendana na Jeshi.
Angalizo hilo pia limewagusa baadhi ya Taasisi ambazo zimekuwa zikiwashonea Wafanyakazi wake mavazi ya Kijeshi na wengine Wafanyabiashara wanauza mavazi hayo.
Amesema “Kwa unyenyekevu tunawaomba Wananchi wanaokiuka Sheria hizo kuacha kuvaa, kuyatumia au kuyauza mavazi hayo kuanzia leo (Agosti 24, 2023), baada ya siku 7 atakayepatikana atapatiwa adhabu kali, tumetoa muda huo kwa kuwa kuna raia ambao hawana uelewa hivyo tunawaelewesha kwa kuzingatia Utawala wa Sheria.”