KERO Jumbe fupi (sms) vamizi ni kero na usumbufu

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
Jun 16, 2024
37
44
Sms zinazotumwa kutoka kwa watu wasiojulikana zimekuwa ni kero kubwa sana na wakati mwingine zinawapa wananchi wasiwasi kuwa huenda taarifa zao binafsi zinazohifadhiwa kwenye simu ya mkononi zikawa zimevuja...tunaomba serikali au mamlaka husika itilie mkazo kwenye kudhibi tabia hizi za sms za kitapeli na nyinginezo zisizo rasmi.

Screenshot_20240723-121134_Messages.jpg
 
Sms zinazotumwa kutoka kwa watu wasiojulikana zimekuwa ni kero kubwa sana na wakati mwingine zinawapa wananchi wasiwasi kuwa huenda taarifa zao binafi zinazohifadhiwa kwenye simu ya mkonini zikawa zimevuja...tunaomba serikali au mamlaka husika itilie mkazo kwenye kudhibi tabia hizi za sms za kitapeli na nyinginezo zisizo rasmi. View attachment 3049840
Wale jamaa wa "Iyo hela itume kwenye namba hii airtel .... jina litakuja........."
Naona bado wapo. Sijui mamlaka imeshindikana kuwadhibiti au ni wa mumo humo?
 
Kuna mtu anawapa hawa watu database ya number za simu na pia wanatumia bulk sms, maana mimi nina namba za mitandao tofauti, kuna siku nakuta namba mbili za mitandao tofauti zimetumiwa msg moja kwa muda mmoja. Tcra iko shindwa kazi 😡
 
tunashukuru kwa sababu mamlaka husika mwanzo walitoa utaratibu wa kufoward ujumbe na namba kwenda namba maalum ( nmeisahau inaanza 15...) kweli watu tulifanya hivyo tumeshatuma sana ila saivi tatizo limekuwa kubwa kuliko mwanzo yaan asubuhi badala ya kuamshwa na alarm unaamshwa na sms ya jiunge freemason, Mara fufua penzi, mara mimi ni mjomba wako nitumie hela......kaaah ni kero.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom