Johnson Lukaza na Mwesigwa Lukaza washinda kesi ya EPA

Kwahiyo wamesubiri wakati watanzania Wapo busy na ESCROW ndio mahakama ikatoa maamuzi.

Inaitwa kimyakimya hiyo
 
Nilishasema kwa kadhia ile ya EPA wafungwaji watakuwa ni wale wale Rajabu Maranda na ndugu yake ambao ni scapegoats tu.. Na hata wao ninasikia hawakaagi sana huko gerezani.. Muda mrefu wanaishi hospitalini wakijfanya ni wagonjwa..

Only in Tanzania..
 
Nilishasema kwa kadhia ile ya EPA wafungwaji watakuwa ni wale wale Rajabu Maranda na ndugu yake ambao ni scapegoats tu.. Na hata wao ninasikia hawakaagi sana huko gerezani.. Muda mrefu wanaishi hospitalini wakijfanya ni wagonjwa..

Only in Tanzania..

Only in Tanzania sosoliso
 
Last edited by a moderator:
Hivi kumbe kuna watu walikuwa wanashitakiwa? jamani naomba anayejua anipe ufafanuzi kwani baada ya tukio hili Kikwete alitamka hadharani kuwa wale wote waliohusika na wizi huu wanajulikana hivyo warudishe fedha hizo na tukaambiwa fedha zimerudishwa na zitaelekezwa kwenye Kilimo sasa inakuwaje hawa washitakiwe na hao wengine watakiwe kurudisha?
 
Kweli Tanzania vichekesho haviishi kila kukicha. Huyu Jaji Kiongozi mkasimongwa ndiye aliyeanza kusikiliza kesi hii miaka hiyooo akiwa kama Hakimu. Leo hii mtu huyohuyo anakuja kutolea maamuzi shauri hilohilo kwenye mahakama ya juu (mahakama kuu). Mmmh. Hii imekaa sawa kweli?

Ikumbukwe huyu jaji ni miongoni mwa mahakim waliopata ujaji hivi karibuni.

Dar es Salaam. Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imemuachia huru Johnson Lukaza na mdogo wake Mwesigwa Lukaza baada ya kuwaona hawana hatia katika kesi ya wizi wa wa Sh 6.3 bilioni za akaunti ya madeni ya Nje (EPA) iliyopo Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Akitoa hukumu hiyo jana Kiongozi wa jopo la Mahakimu watatu wanaoisikiliza kesi hiyo, Jaji wa Mahakama Kuu, Edson Mkasimongwa alisema baada ya kupitia ushahidi uliotolewa na mashahidi saba wa upande wa mashtaka na utetezi wa washtakiwa hao anaona upande wa mashtaka umeshindwa kuthibitisha mashtaka pasipo kuacha shaka.

Mashtaka matano yaliyokuwa yakiwakabili hao ni pamoja kula njama, kughushi, kuwasilisha hati za uongo za makubaliano ya kuhamisha deni kati ya kampuni yao ya Kernel Ltd na kampuni Marubeni ya nchini Japan na kujipatia kiasi hicho cha fedha cha Sh 6.3 bilioni kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hukumu hiyo, Jaji Mkasimongwa amesema wamewaachia huru washtakiwa hao katika makosa hayo yote kwa sababu ushahidi wa upande wa mashtaka haukujitosheleza kwa kuwa ulishindwa kuthibitisha kama ni kweli Novemba 2,2003 washtakiwa hao walighushi hati ya makubaliano ya kuhamisha deni la Sh 6.3 bilioni baina ya kampuni ya Kernel Ltd na Marubeni ya nchini Japan ilikuwa ni ya kughushi.

Jaji Mkasimongwa anasema ushahidi unaonesha kampuni hiyo ya Marubeni ya nchini Japan ilikubali kupokea kiasi hicho cha fedha na kwamba washtakiwa wao walipata asilimia tu ya 20 ya fedha hizo na upande wamashtaka hakuwahi kulibishia hilo.

Katika kesi hiyo, Johnson Lukaza ambaye ni Mwenyekiti wa makampuni ya Proin na ni Mjumbe wa Baraza la Chuo Kikuu cha Bagamoyo (UB) pamoja na mdogo wake Mwesiga walikuwa wanatetewa na Wakili Alex Mgongolwa aliyekuwa akisaidiwana na Wakili Alex Mshumbusi.

Baada ya hukumu hiyo kutolewa ndugu wa washtakiwa hao waliaza kulia mahakamani hapo pamoja na mshtakiwa Mwesiga wakiwa hawa amini kilichotokea huku wakisema asante Yesu, asante Yesu.


Chanzo: Mwananchi
 
utafungwaje ukishakuwa na mpunga? baka uone.Kila mtu akisikia kesi yako anaomba urafiki.kuanzia polisi, mawakili wa serekali , hakimu, askari magereza madaktari-----------------sema umepiga mtu uone
 
ukiwa
utafungwaje ukishakuwa na mpunga? baka uone.Kila mtu akisikia kesi yako anaomba urafiki.kuanzia polisi, mawakili wa serekali , hakimu, askari magereza madaktari-----------------sema umepiga mtu uone
na hela hufungwi😂😂😂
 
Back
Top Bottom