Pre GE2025 DSM Joh Makini: Kama hutajiandikisha utakuwa unawapa nafasi wengine wakufanyie maamuzi

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
4,049
13,865
Akitoa maoni kuhusu mchakato wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Nchini unaoendelea Dar es Salaa, Msanii wa Bongo Fleva, Joh Makini amesema:

Ni haki ya Msingi ya Mwananchi aliyetimiza vigezo, kama hutajiandikisha utakuwa unawapa nafasi wengine wakufanyie maamuzi, wewe unatakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka, shiriki, Uandikishaji sio suala la kupata Kitambulisho pekee bali kushiriki katika kufanya maamuzi ya Kikatiba na Kidemokrasia.

1742559743218.png

Soma, Pia
 
Kwani Tanzania kuna uchaguzi ?Tulipeleka maoni yetu Dodoma lakini tulishangaa tunazuiliwa Kwa mitutu ya bunduki Sasa huko kujiandikisha Kwa faida ipi wakati maoni ya watanzania waliowengi jamyaki??
 
Tatizo linalofanya watu wengine wamekuwa wazito kujiandikisha ni kwa sabu ya ukweli usiofichika kuwa kwa sasa hivi hapa Tanzania kura haina maana wala thamani tena, kwa utaratibu uliobuniwa na CCM mwaka 2019 na 2020 ambao ndiyo unatumika hadi sasa kama tulivyoshudia November 2024 wa kuengua wapinzani na kuiba kura na mshindi halali kutotangazwa kuwa ameshinda. Ni kupoteza muda kwenda kushiriki zoezi la kupiga kura wakati unajua kuwa Tume inakuja na matokeo yake mfukoni.Mimi kadi ninayo lakini kamwe sitakaa nipoteze muda wangu kupiga kura. Hata wanaojiandiksha wengi wanataka kupata tu hicho kitambulisho.Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kupoteza muda wake kupanga foleni tena juani au kwenye mvua kupiga kura. Ni CCM na serikali yake ndiyo imeondoa maana halisi ya kupiga kura. Inatumika karibu nusu Trilioni kwa ajili igizo la kupiga kura, ni bora tu hiyo hela ingeelekezwa kwenye huduma nyingine za maendeleo kuliko kuzitia kiberiti kwa uhuni unaoitwa uchaguzi.NO REFORM NO ELECTION.
 
Akitoa maoni kuhusu mchakato wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Nchini unaoendelea Dar es Salaa, Msanii wa Bongo Fleva, Joh Makini amesema:

Ni haki ya Msingi ya Mwananchi aliyetimiza vigezo, kama hutajiandikisha utakuwa unawapa nafasi wengine wakufanyie maamuzi, wewe unatakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka, shiriki, Uandikishaji sio suala la kupata Kitambulisho pekee bali kushiriki katika kufanya maamuzi ya Kikatiba na Kidemokrasia.

Soma, Pia

Maamuzi hayatokani na kura kwa sasa sijui kwanini hamuelewi. Maamuzi yanatokana na Makada ambao ni viongozi wakisaidiana na polisi na usalama wa taifa wanaiba kura. Kura yako kwa mazingira ya sasa haina maana yeyeote
 
Tatizo linalofanya watu wengine wamekuwa wazito kujiandikisha ni kwa sabu ya ukweli usiofichika kuwa kwa sasa hivi hapa Tanzania kura haina maana wala thamani tena, kwa utaratibu uliobuniwa na CCM mwaka 2019 na 2020 ambao ndiyo unatumika hadi sasa kama tulivyoshudia November 2024 wa kuengua wapinzani na kuiba kura na mshindi halali kutotangazwa kuwa ameshinda. Ni kupoteza muda kwenda kushiriki zoezi la kupiga kura wakati unajua kuwa Tume inakuja na matokeo yake mfukoni.Mimi kadi ninayo lakini kamwe sitakaa nipoteze muda wangu kupiga kura. Hata wanaojiandiksha wengi wanataka kupata tu hicho kitambulisho.Hakuna mtu mwenye akili timamu anaweza kupoteza muda wake kupanga foleni tena juani au kwenye mvua kupiga kura. Ni CCM na serikali yake ndiyo imeondoa maana halisi ya kupiga kura. Inatumika karibu nusu Trilioni kwa ajili igizo la kupiga kura, ni bora tu hiyo hela ingeelekezwa kwenye huduma nyingine za maendeleo kuliko kuzitia kiberiti kwa uhuni unaoitwa uchaguzi.NO REFORM NO ELECTION.
Yule kichaa waliemuokota akichunga mbuzi huko porini ndio alinajisi demokrasia hapa nchini na waliorithi wanakenua na kuendeleza huo uhuni TU!
 
Prof.Tinaijuka amesema wazi kabisa,akimaanisha kwa hali ilivyo sasa hivi,hakuna kura itakayoamua nani awe Rais,Mbunge wala diwani.Huyo Joh Makini asiwe kama haijui katiba ya nchi yetu yasasa.
 
NETO waungane na CHADEMA, wapilie msumari kwenye NO REFORM NO ELECTION, hizo trillions of money zinazotarajiwa kufanya mazingaombwe,ziajiri waalimu.
 
Hata ukijiandikisha maamuzi yanafanywa na watu wengine, rejea👇😃

Yule kichaa waliemuokota akichunga mbuzi huko porini ndio alinajisi demokrasia hapa nchini na waliorithi wanakenua na kuendeleza huo uhuni TU!
Katika jambo ambalo namlaani Mkapa ni hili la kutuachia yule mwendawazimu, Mapdri na Maaskofu wa Kikatoliki walimuonya kuwa huyo ni kichaa akamkingia kifua.
 
Akitoa maoni kuhusu mchakato wa Uandikishaji na Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura Nchini unaoendelea Dar es Salaa, Msanii wa Bongo Fleva, Joh Makini amesema:

Ni haki ya Msingi ya Mwananchi aliyetimiza vigezo, kama hutajiandikisha utakuwa unawapa nafasi wengine wakufanyie maamuzi, wewe unatakiwa kuwa sehemu ya mabadiliko unayoyataka, shiriki, Uandikishaji sio suala la kupata Kitambulisho pekee bali kushiriki katika kufanya maamuzi ya Kikatiba na Kidemokrasia.

Soma, Pia
 
Attachments

  • 5811771-84b12f6d5ff81d807821a183416ac2ed.mp4
    648.4 KB
Huyu hajui lolote kuhusu chaguzi za nchi hii, aendelee kuandika mistari ya rap
 
Back
Top Bottom