JKT yatangaza majina ya vijana waliohitimu Kidato cha Sita 2021 wanaotakiwa kujiunga na JKT kwa Mujibu wa Sheria

xz0r_africa

JF-Expert Member
Jan 6, 2014
316
313
Jeshi la Kujenga Taifa (JKT), limechagua vijana waliohitimu elimu ya sekondari kidato cha sita kwa mwaka 2021, kutoka shule zote za Tanzania Bara kuhudhuria mafunzo ya JKT kwa mujibu wa Sheria.

Vijana waliochaguliwa wamepangiwa katika kambi za JKT Rwamkoma - Mara, JKT Msange - Tabora, JKT Ruvu - Pwani, JKT Mpwapwa Dodoma, JKT Mafinga - Iringa, JKT Mlale - Ruvuma, JKT Mgambo na JKT Maramba -Tanga, JKT Makuyuni - Arusha, JKT Bulombora, JKT Kanembwa, na JKT Mtabila - Kigoma, JKT Itaka - Songwe, JKT Luwa na JKT Milundikwa - Rukwa, JKT Nachingwea - Lindi na JKT Kibiti- Pwani na Oljoro JKT- Arusha.

Wahitimu wenye ulemavu wa kuonekana kwa macho (physical disabilities) waripoti katika kambi ya JKT Ruvu iliyopo Mlandizi mkoani Pwani ambayo ina miundombinu ya kuhudumia watu wa jamii hiyo.

majina nimeshare folder kwenye google drive kwa sababu web ya jkt inload sana bofya hapa ku view kwa sasa
 
binafsi nimepita huko for 2 years. kule sio kutesa as you think.
tena siku izi wamepunguza dozi maana wanajua watarudi uraiani. its more of national service
Nilkuwa Ruvu and then Rwamkoma during 1978. Najua kabisa ni some sort of national service, but things have changed, parents have to cater foe some upkeep like mavazi, pocket money etc which were given free during our time! Kama nagaramia , why go there? ndiyo hoja yangu...
 
Yaani JKT mnalipia wazazi? Sio freshi majirani. Hiyo ni kazi ya serikali, basic needs zote ukiwa ndani!
 
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
  3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  7. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
 
Nilkuwa Ruvu and then Rwamkoma during 1978. Najua kabisa ni some sort of national service, but things have changed, parents have to cater foe some upkeep like mavazi, pocket money etc which were given free during our time! Kama nagaramia , why go there? ndiyo hoja yangu...
sioni sababu ya kwenda JKT, mateso tu with no rewards
 
Exactly there is no rewrd t all. Ni kuwaongezea wazazi ghrama. Look here"

JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
  3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  7. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
 
JKT linawataka vijana hao kuripoti wakiwa na vifaa vifuatavyo.

  1. Bukta ya rangi ya ‘Dark Blue’ yenye mpira kiunoni (lastic), iliyo na mfuko mmoja nyuma, urefu unaoishia magotini, isiyo na zipu.
  2. T-shirt ya rangi ya kijani (Green Vest)
  3. Raba za michezo zenye rangi ya kijani au blue.
  4. Shuka mbili za kulalia zenye rangi ya blue bahari.
  5. Soksi ndefu za rangi nyeusi.
  6. Nguo za kuzuia baridi kwa waliopangiwa mikoa yenye baridi.
  7. Track suit ya rangi ya kijani au blue
  8. Nauli ya kwenda makambini na kurudi nyumbani.
Wah, kazi kwao wazazi...
 
Kama mtu asipokwenda jkt kwa kujibu wa sheria, atapata hasara gani na faida zake ni zipi kielimu? Naomba kujua hilo kabla sijafanya maamuzi
 
Kuna ulazima WA kuripoti kambi na mkoa uliopangiwa tu? Au unaweza kuripoti kambi yoyote? Na kuripoti kambi yoyote utapokelewa?
 
Back
Top Bottom