Jipu ukaguzi wa magari UK

Chris lukosi kaingia CCM ili awaibie watanzania. kazi ya CCM ni kuwaibia maskini tu. Vizuri watanzania wote wakapinga dhuluma hii ya wana CCM.
 
Hilo kweli ni tatizo kubwa. Inaniuma sana sababu cos nimeagiza gari toka UK, natakiwa niwalipe Serengeti £150 kwa ukaguzi wao wakati limekaguliwa na wataalamu Kwa £50.
Sasa ni kwanini gari moja likaguliwe mara mbili?
Kwanza linakaguliwa na MOT ambao ni wataalam na wana viwango vya juu kuliko TBS, then likaguliwe tena na watu ambao siyo wataalam tena kwa gharama kubwa. Kwanini TBS isifanye makubaliano na MOT ili ukaguzi wa MOT ndo uwe kithibitisho cha ubora wa gari kabla ya kulileta Tanzania?
 
Serikali hii ni serikali isiyokuwa na ubabaishaji na inayojali maslahi na haki za wanyonge zinazochukuliwa na wachache wenye nguvu.

Ombi letu kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu ni kulichukulia hatua stahiki jambo hili.
 
Mbona hili jipu ni rahisi kulitumbua kuliko munavyofikiria. Pigeni simu HM Revenue & Excise Dept na Consumer watchdog muwape details za hawa watu wawachunguze

1. Wamekata leseni ya kufanya hiyo kazi kutoka kwa Ministry of Transport?
2. Wanao wataalamu waliokubalika kufanya hiyo kazi?
3. Hiyo kazi wanaifanya kweli?
4. Wanalipa kodi kutoka kwenye kipato chao?
5. Fee wanayo charge ni proportional na kazi yenyewe?

Wao watawachunguza kwa kuwapelekea gari bovu na kwa ujinga wao watalipasisha. Wataishia hapo. Mimi nilifikiri kusafiri ndio kusoma kumbe bado mmelala tu. Am very dissapointed. Kama hamuiwezi hiyo kazi nipeni mimi hizo details zao nikufanyieni. Uliwahi kumsikia Mandela akilalamika kwa Peter Botha alipokuwa akinyanyaswa?

Pia kuna wale akina Chris Collins na Matt Allwright wa BBC kipindi cha Warchdog wanaweza kupewa info zote na wakafuatilia.

Unaweza kuwatafuta kupitia link hii- Watchdog - BBC One
 
Lukozi ni Verified User hapa, please jibu hizi tuhuma. waeleze watanzania je ulipataje hiyo tender, Revenue sharing yenu ikoje? Ni kweli huna wataalamu? Na ni kweli unapatikana sehemu moja tu hivyo kuwalazimu kutembea umbali mrefu kuja kuhakiki kari ofisi zenu.

JK aliwahi kusema "Uongo Ukirudiwa rudiwa huwa Ukweli" sasa kuna wanaosema ni uongo mara kwa mara bado haujawa ukweli?

LUKOZI AMKA
 
Jamaa soon atarejeshwa Bongo.... na sikuhizi amekuwa sio mzungumzaji kabisa jf amepoa... kweli ukizoea vya bure vya jasho hutoviweza
 
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim jipu kubwa la UK ni la ukaguzi wa magari.

Kuna upotevu mkubwa wa pesa za serikali ambapo TBS wamewapa kampuni ya ubabaishaji inajiita Serengeti Global. Kwa kawaida UK kila gari linakuwa na kibali cha MOT (Ministry Of Transport) ambacho gharama yake ni Pound 35 hadi 45 tu, na ukaguzi wa kupata kibali hiko hufanyika garage.

Cha ajabu hawa wanaojiita Serengeti Global inayomilikiwa na Bwana Lukosi wanatoza Pound 150 kitu ambacho si sahihi, gharama ni kubwa mno na wala hawana garage ya kufanyia ukaguzi wa magari. Wanakwenda nyumbani kwa mwenye gari na kufanya ukaguzi bila wataalam kasha wanabandika sticker.

Serikali ya awamu ya tano inajali sana maslahi ya Wananchi wake hususan masikini, tunaomba muushughulikie wizi huu unaoendeshwa na hii kampuni ya Serengeti Global
Swali la kujiuliza hapa ni sababu zipi zimeifanya GoT isitambue/accept MoT (ambayo ni serikari mwenza) na itambue ukaguzi wa walanguzi.
 
Waziri Mkuu Mheshimiwa Majaliwa Kassim jipu kubwa la UK ni la ukaguzi wa magari.

Kuna upotevu mkubwa wa pesa za serikali ambapo TBS wamewapa kampuni ya ubabaishaji inajiita Serengeti Global. Kwa kawaida UK kila gari linakuwa na kibali cha MOT (Ministry Of Transport) ambacho gharama yake ni Pound 35 hadi 45 tu, na ukaguzi wa kupata kibali hiko hufanyika garage.

Cha ajabu hawa wanaojiita Serengeti Global inayomilikiwa na Bwana Lukosi wanatoza Pound 150 kitu ambacho si sahihi, gharama ni kubwa mno na wala hawana garage ya kufanyia ukaguzi wa magari. Wanakwenda nyumbani kwa mwenye gari na kufanya ukaguzi bila wataalam kasha wanabandika sticker.

Serikali ya awamu ya tano inajali sana maslahi ya Wananchi wake hususan masikini, tunaomba muushughulikie wizi huu unaoendeshwa na hii kampuni ya Serengeti Global
Kuna alternative nyingine ya kufikisha malalamiko kwa GoT. Jikusanyeni waathirika au chama cha waTz, andika barua ya malalamiko kwa Waziri husika, nakala kwa kitengo cha Diaspora MoFA, Balozi, Waziri Kivuli, Wabunge (as much as you can reach) then wait for reaction.
 
Sasa ni kwanini gari moja likaguliwe mara mbili?
Kwanza linakaguliwa na MOT ambao ni wataalam na wana viwango vya juu kuliko TBS, then likaguliwe tena na watu ambao siyo wataalam tena kwa gharama kubwa. Kwanini TBS isifanye makubaliano na MOT ili ukaguzi wa MOT ndo uwe kithibitisho cha ubora wa gari kabla ya kulileta Tanzania?
Mkuu naona unataka watu wafe kwa njaa!!
 
Mkuu naona unataka watu wafe kwa njaa!!
Hapa kuna chembe chembe za rushwa yaani unatembea masaa manane njiani kwenda kupeleka gari likakaguliwe ukifika huko hawafanyi Ukaguzi wowote, unalipia pesa then unapewa sticker, halafu unarudi kwenu mwendo wa masaa manane tena. Tunacholalamikia siyo tu hizo Pound 150 zinazolipwa bila sababu bali pia hata mafuta yetu kwenda na kurudi umbali mrefu kufuata huduma ya Ukaguzi
 
Mkuu tafadhali weka ushahidi wa madai yako ili kuwe na uwajibikaji kutoka kwako na kwa hawa jamaa.

Unaweza ukaweka Reg za magari husika, tarehe za hio MOT walofanya jamaa na zile MOTs za kihalali.

Halafu kama magari hayo yapo Tanzania basi yatafuatiliwa na kuunganishwa na TBS kama waliyafanyia ukaguzi mwingine.

Tuwe serious na masuala kama haya hasa ya UFISADI.
 
Ukweli huu ni mradi wa watu wachache pale Dar na ikichunguzwa kwa karibu utakuta kuna watu wa ubalozi wanausika kwenye hili kwani ili jibu aliwezekani limeota huku UK wakati tunawatu wa ubalozi wapo.
 
Sisi tunapendelea sana short cut ndiyo maana huyo Jamaa yuko hapo kwa kuwa Siku zote yeye alikuwa anajua bongo Wote ni lalaaaaaa mbele/ nyuma yake wako wasela sasa ungepita wapi wewe Sungura???!!! Reality is.capital, kwani hatuwezi kuishi bila Rusha/ favour??)
 
Haya ni majungu watu wanajitoa kwa sababu ya taifa lao mnaanza majungu ya kuwachafua watanzania tuache majungu si mtaji, pambana kama mshikaji acha fitina na uzushi
Yaani kupeleka gari likakafuliwe na watu wasiokuwa na ujuzi ndiyo majungu? Labda neno majungu lina tafsiri nyingi
 
Back
Top Bottom