Jiondoe kwenye kifungo kisicho na ulazima

Kuna sababu zinafanya watu kuwa kwenye vifungo vya ndoa/mahusiano na kushindwa kujitoa.
- Utegemezi kiuchumi, hili limekuwa likiwakumba baadhi ya wanawake, wapo katika mahusiano na hali inakuwa mbaya kwa kupigwa, matusi, kuharibiwa saikolojia na hata kubakwa. Wanashindwa kujitoa kwenye mahusiano mabovu kwa vile ni tegemezi kuanzia kula mpaka vitambaa vya wakati wa hedhi. Wanaume zao nao wanachukua kama fursa kuwanyanyasa.
- Woga wa kuonekana wameshindwa, sidhani kama kuna mtu anatamani kuitwa "failure", hata katika mahusiano hakuna anayependa kuonekana ameshindwa. Wapo wanoona inatosha, waendelee na maisha mengine, lakini wengine hawawezi. Kumbuka binadamu tuna tabia tofauti, malezi tofauti, uvumilivu na ustahamilivu tofauti. Hivyo sio kila mtu anaona kuwa suluhisho ni kuachana.
- Sababu ni nyingi, lakini pia mtu utabadilisha watu hadi lini, imagine mtu yupo 40's au 50's kila uchao ni kubadilisha wapenzi coz huna furaha.
Furaha yako hailetwi na mtu mwingine, bali ipo moyoni mwako.
 
Dah Hongera kaka Eli79 Umeongea mengi sana ambayo nadhani ni sababu kuu za watu kushindwa kujiondoa katika vifungo
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…