Jinsi ya kutumia mafuta kidogo kwenye gari

Vitu vinavyo fanya Gari litumie mafuta mengi ni pale mzigo unapo kuwa mkubwa (Load).

Mzigo huu unaweza kupunguzwa kwa kupunguza baadhi ya visababishi ambavyo si vya lazima.

1. AC: Unapo tumia AC engine lazima itatumia nguvu zaidi hivyo itaunguza mafuta mengi.

2. Unatembea zaidi ya km 45 kwa saa na madirisha umeyafungua , hii utasababisha gari kupambana na upepo hivyo kuongeza mzigo wa gari. Ina semekana kama unatembea kwa speed kubwa na madirisha yapo wazi gari litatumia mafuta zaidi hata kuliko ukiwasha AC.

Mengine watalaam watayaleta.


Ili nisifanye namba moja inabidi nifanye namba mbili. Contradiction.
 
Mimi naona kama sababu zako zinakinzana, yaani lazima upambane na moja wapo.

Mfano;

Natembea 60km/hr inabidi nifunge madirisha ili kupunguza ulaji wa mafuta - hapo itabidi uwashe AC na tunarudi kwenye ishu hiyo hiyo.


Na mimi nimemwambia ili nisifanye namba 1 inabidi nifanye namba 2 ambayo kasema tuepuke!
 
Road bumps pia zinakula mafuta. Tanzania kila barabara ina matutu hii ni dalili ya watu kupungua uwezo wa kufikiri. Nenda Capetown au Gaborone uone barabara kama zina matuta ni mwendo wa zebra na traffic lights tu huku kuna sola lakini magomeni na moroco kila siku kuna mida taa hazifanyikazi. Uwezo wa uelewa kwa watumiaji barabara unahitajika sana. Unakuta kituo cha basi hakuna na bodaboda zimejaa utadhani uko garage. SAFETY ndogo sana.
 
Khaa!! Kuna njia moja ya kuongezea hewa ya hydrojen kwenye hewa inayoingia kwenye injini ya gari. Nilisoma mahali na niliwahi kujaribu, hii inafaa zaidi kama unaenda zaidi ya 100km/h lakini inasababisha backfiring ya engine sikujua kwanini nadhani kunahitajika modification wa mfumo wa engine na usalama wake. Njia hii unaweza okoa hadi 30% ya mafuta
 
punguzeni safari, siku zote piga short cut ways, usijifanye mwema sana kuwasogeza watu kwenye majumba yao, nenda safari uliyokusudia bila kuongeza visafari vingine hata vya hatua 10. Uwe na self disciplinekatika safari zako!
 
Oxygen sensor ni vyema ikawa nzima pia na water/coolant sensor hivi vinapeleka ujumbe kwny control box juu ya utumaji mafuta kwny engine kama vibovu/vimechoka vitaimislead mafuta yataenda mengi kuliko mahitaji tumia mara kwa mara petrol/diesel treatment zinasafisha na kumaitain performace ya engine kwny utumiaji wese pia hakikisha unakuwa na mafuta walau juu ya robo tank pia angalia ukanyagaji wako mafuta endesha taratibu gia zitajibadili hadi kufikia speed unayotaka ukikamua rpm 3 jua mafuta umeyamwaga pwaaaa. Tafuta sweet speed ya gari yako haswa aa utakayokuwa unaona mwnyw inaenda vzr lakini isizidi 110 usiache gari idle kwa kupasha moto au kwa sababu ingine zima au washa nenda
 
Duu namba mbili hapo mkuu nimeipenda sana na ina logic sana . Hebu saidia na pikipiki mkuu wenyewe wafanyeje?
1. Ukiweka windscreen mbele hakikisha unapoendesha hiyo windscreen inakuwa ndefu kuliko wewe, pia akikisha kidevu chako kiko karibu na dashboard ya pikipiki.
2. Usifae koti jacket linaloingiza upepo wakati unaendesha...vaa linalokubana.
3. kama hauna windscreen hakikisha unaendesha ukiwa umetanua kwapa kurahisisha upepo kupita kwa urahisi....! Wengine wataongezea
 
Hesabu zenu zinaonyesha magari ya mikopo, alafu kila mtu ataje gari alilonalo ili nimpatie maujanga ya kwenda kazini na kurudi kwa robo lita. Mimi ya kwangu natumia bodaboda.

Vitu vinavyo fanya Gari litumie mafuta mengi ni pale mzigo unapo kuwa mkubwa (Load).

Mzigo huu unaweza kupunguzwa kwa kupunguza baadhi ya visababishi ambavyo si vya lazima.

1. AC: Unapo tumia AC engine lazima itatumia nguvu zaidi hivyo itaunguza mafuta mengi.

2. Unatembea zaidi ya km 45 kwa saa na madirisha umeyafungua , hii utasababisha gari kupambana na upepo hivyo kuongeza mzigo wa gari. Ina semekana kama unatembea kwa speed kubwa na madirisha yapo wazi gari litatumia mafuta zaidi hata kuliko ukiwasha AC.

Mengine watalaam watayaleta.
 
Mimi naona kama sababu zako zinakinzana, yaani lazima upambane na moja wapo.

Mfano;

Natembea 60km/hr inabidi nifunge madirisha ili kupunguza ulaji wa mafuta - hapo itabidi uwashe AC na tunarudi kwenye ishu hiyo hiyo.

Unapokuwa kwenye high speed, momentum (mass times acceleration) ya Gari inakuwa kubwa zaidi hivyo ulaji wa mafuta unashuka hata kama ukiwa umewasha AC.
 
Ata kufanyia uzinzi kwenye gari pia inaweza kusababisha mafuta kuisha haraka pia.

Hii ni obvious kwa sababu utalazimika kuiacha gari yako kwenye silence kwa muda mrefu kwa ajili ya ac. Ila kuna watu wana machaka yao hata wakishusha vioo inakuwa fresh tu
 
Pia, ukiweza Ku maintain rpm (engine rotation per minute) ya 2 mpaka 2.5 yaani mizunguko 2000 mpaka 2500 ya injini kwa dakika (Tazama mshare wa rpm), basi ulaji wa mafuta unakuwa mzuri zaidi (efficiency).

Sababu ni kwamba unapoilazimisha injini izunguke juu ya rpm ya 3 au zaidi, unafanya valve za mafuta zifunguke zaidi na kuvuta wese la kutosha zaidi ya kawaida.
 
Ukipakia mchepuko na kwenda nao bar wakati nyumbani wanakula misumari mafuta pia yanaenda mengi.

Hii safari ya kwenda na mchepuko sehemu sehemu ndo mbaya zaidi, inamaliza sana mafuta safari zingine zinaibuliwa na michepuko wewe hata hujaipangilia hahahahaha
 
Avoid kuweka mguu kwenye accelerator muda wote, ikiwa kama gari iko kwenye mteremko au ishakolea speed au vyote kwa pamoja basi pumzisha tu mguu wako na uwe stand by kwa either break au mafuta tena.
 
Back
Top Bottom