Jinsi ya kutengeneza mwili bila kuingia Gym

Ndio...au nikurahisishie ...cardio gani effective kuliko zote kabisa
Kubox siyo cardio, ile mtu huifanya baada ya kufanya mazoezi ya kukimbia na kuruka kamba (yaani baada ya kutengeneza pumzi). Ndiyo maana kama mtu ambaye hana msingi wa pumzi akipiga punching bag ngumi nne, aki-bob na ku-weave mara tatu anatoka jasho na pumzi zinampaa.

Kwa uzoefu wangu bado kujogg ni better cardio, ili kuipata the best inabidi uunganishe hizo cardio kutengeneza kitu kimoja.
 
Ahsante,pamoja sana.
 
mimi huwa napiga push up 50 kwa mara moja,ina madhara gani kukunja ngumi?
Mara nyingi madhara ya kukunja ngumu ni kupata sugu kwenye knuckles. Na kiuswahilini uswahilini sumtym polisi wanazingua ukiwa na zile sugu.

Ukitaka kupiga pushup ya ngumi basi vaa sox mikononi. Mikono inabaki smooth ila mifupa kwa ndani ndo inakua na sugu.
 
Sawa sawa kaka so kama unapiga 10 unapumzika kwa dk5

Si ndio unamaana km hiyo
Ongeza sekunde kumi (hivyo badala ya skeunde 10 zitakua 20) katika kupumzika kati ya hizo 10 na 10 zingine. Ukihama namna ya kupiga push up (mfano ulianza za kawaida unataka uhamie za kuweka miguu juu) pumzika kwa dakika mbili.
 
Binafsi enzi hizo nilikua napiga kwa sequence maalum.
Kwanza nilianza kwa kupiga push ups za kutanua kifua. Ambazo unapanga matofali mawili kushoto na kulia kwako au vipande vya mbao kisha unakua mikono waiweka juu na kupiga push-ups huku kifua kikiingia katikati.
Nilikua napiga push-ups 50 na nilienda mizunguko 6.
Break ya round na round nilikua na piga squats 100.

Zoezi namba 2 nilikua napiga push-ups za kubana kifua huku mikono nikiibana level ya mabega napo idadi ya push-ups ni kama round one na reps ni sita.

Zoezi namba tatu hapa nilikua naikutanisha mikono kisha natengeneza shepu kama ya kopa.
Nilikua napiga push-ups 3 in 1(yani kila push ups tatu nilizihesabu kama moja) huku kila nikishuka chini kifua kina gusa ile kopa.
Zoezi hili lilikua maalum kwa kujenga msuli wa nyuma ya mkono, kujenga kifua cha juu na kuziba yale matundu ya shingoni,kuujenga mgongo na kua na mwonekano wa kupasuka pasuka.
Nilikua napiga push-up 20 na round 5.

Baada ya hapo nilipiga Zoezi la kujenga shoulders ambalo mara nyingi niliipigia kitandani.
Unachuchumaa kitanda kikiwa nyumba yako kisha mikono una irudisha nyuma na kushika ubao wa kitanda.
Zoezi hili unapiga taratibu na unatakiwa upige push ups hizi 60 *5.

Ukimaliza unaenda mlangoni na kupiga pull ups kwa ajili ya kujenga msuli wa mbele ya mkono.
Pia weza ligeuza kujenga msuli wa nyuma ya mkono.

Baada ya kushughulikia sehemu zote nilikua napiga zoezi la kutengeneza six packs.
Hili zoezi ni gumu kulielezea ila unakaa chini.
Kisha unainyanyua miguu yako unakua kama V. Baada ya hapo unaweka mikono yako kifuani na kuanza kupeleka miguu mbele kama unasukuma kitu bila kuishusha. Unapiga mbele 30,kushoto 30,kulia 30 then unageuka na kupiga push-ups 100 za basketball ili kujenga misuli ya mkono wa chini, zile nyama chini ya kiwiko chako.

Then unahamia kwenye mazoezi ya miguu ukimaliza unajikumbushia kata mbili tatu za wingchun then unapiga sparring na swahiba wako kujiweka fiti tu.
Tuongezee mawili matatu chief.
 
Aisee kwanza hongera lakini utagundua kua kwa sasa hivi hazikupi tena changamoto.

Kwa spartan fanya kwamba mikono ikishakaa kama ile picha inavyoonesha utakua ukija juu unakua kama unataka kupiga pushap za kupiga makofi (hivyo utakua unanyanyua mikono yako off the ground).
Lakini kila ukinyanyuka mkono uliokua nyuma utaenda mbele, uliokua mbele utarudi nyuma.

Kama bado mkuu, usisite kuniuliza.

Nimeelewa mkuu. Ahsante sana.

Maelezo mazur mkuu, ongeza na haya
1. Kabla ya kuanza mazoez ni vizur ku fanya warm-up ili kuuandaa moyo kwajir ya kusukuma damu haraka.
2. Kumbuka kufanya kujinyoosha (stretching) kabla na baada ya zoez kuepusha kukakamaa(kupoteza mnyumbuliko wa mwili
3. Kumbuka kunywa maji kidogo kabla ya zoez (kama dk30 kabla) Pia baada kufidia maji utakayopoteza kwanjia ya jasho. Kumbuka kupumzika vizur na kupumua vzur
 
Ahsante mkuu nikajisahau nikaandika kama vile nawaandikia wanaojua kila kitu.
 
Wadau kwa anayeona yupo advanced haswa anaweza kuifuata post namba 70 ya Konsciouz.
 
Back
Top Bottom