Jinsi ya kushiriki katika Uwekezaji Huria (Venture and Angel Investment)

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,675
6,046
Habari za wakati,

Ni matumaini yangu kwamba mu wazima na mnaendelea vyema katika utendaji wa shughuli zako na ujenzi wa nchi.

Leo nimeleta mjadala mfupi kuhusu maneno ambayo tumezoea kuyasikia ambayo ni Venture Capital na Angel Capital.Ukifanya utafiti wa haraka wa google utaona maana ya maneno haya kwa lugha ya kiingereza na leo nataka tuyajadili kwa kiswahili.

Katika kufanya kazi na wajasiriamali moja kati ya jambo ambalo nimekutana nalo ni uhitaji wa mtaja,ukosefu wa mtaji na uhaba wa mtaji.Kwa kiasi kikubwa kila mjasiriamali niliyekutana naye amekuwa akihangaishwa na swala la mtaji.Wakati mwingine kukosa mtaji kunawafanya wakose biashara kubwa,wakose fursa ya kukua na wakati mwingine wakose ujasiri wa kufanya maamuzi ya msingi kuhusu biashara yao.

Asilimia kubwa ya wajasiriamali hutegemea mtaji kutoka katika akiba zao binafsi,msaada kutoka kwa ndugu,mauzo ya rasilimali zao na mikopo kutoka taasisi za kifedha.Ukitazama vyanzo vyote hivi vya mitaji utaona kabisa kwamba vyote vinapunguza wigo wa mjasiriamali kupata mtaji wa uhakika.Hali hii inapelekea kupote kwamawazo mazuri ya biashara ambayo yanaweza kubadili kabisa uelekeo na hali za maisha ya jamii yetu.

Katika kufanya kazi na wajasiriamali,imetokea nikashirikiana nao hasa katika hatua ya kutafuta fedha.Mara nyingi nimekuwa nikijaribu kuwaonesha na kuwasaidia katika kutumia taasisi za kifedha kama mabenki ya biashara katika kupata mitaji.Changamoto kubwa ni kwamba kwenye taasisi za kifedha hakuna namna ya kupata mtaji bila kwanza kuwa na uhusiano wa kibenki na kuwa na historia ya kibenki hasa miamala.Lakini pia kuna swala la Dhamana na changamoto nyingine za kukosekana uelewa kuhusu bidhaa na huduma zinazotolewa na mabenki hali ambayo inapelekea wajasiriamali wengi kushindwa kufahamu na kutumia huduma hizo.

Sasa leo nataka tuzungumze kuhusu SOKO HURIA LA MITAJI ambapo kwa muktadha wa mjadala huu nitakuwa nazungumzia Angel Capital na Venture Capital.Kimsingi hizi zote ni namna ambazo biashara zinapatiwa mtaji.Tofauti iliopo ni kwamba Angel Investor anakuwa ni mtu ambaye ni tajiri au ana kipato cha ziada ambaye anatoa mtaji kwa biashara changa kabisa ambayo haikopesheki ila ina uwezo wa kukua wakati Centure Capital ni kundi la watu ambao wanaunganisha Fedha zao kwa pamoja na kuamu kuwekeza katika biashara changa na zenye uwezo mkubwa wa kukua.

Vitu kama Vicoba vinaweza kufanya kazi kama VC iwapo tu wataamua sasa kutumia VICOBA vyao na kuvisimmamia kama mifuko ya uwekezaji hasa kwa kutumia mbinu za kisasa za kutambua na kusimamia mawazo ya biashara.

Kama kichwa cha mada kinavouliza Je unawezaji kushiriki katika Uwekezaji Huria?

Kama nilivoeleza hapo juu kitu ka Vicoba kinaweza kuwa chanzo kizuri ila katika kutaka kuweka mambo vizuri nilitembelea baadhi ya taasisi za kifedha na kuzungumza nao kuhusu huduma zao.Taasisi nyingi za kifedha hutoa mikopo kwa hivi vikundi ka Saccos na Vicoba kwa ajili ya kuwakopesha wanachama wao lakini pia wakati mwingine huwakopesha wanachama moja kwa moja.Baada ya kutazama hili nikajiuliza Je hatuwezi kuazima mbinu kutoka katika huu mfumo kwa lengo la Uwekezaji katika mawazo ya Biashara na kuyapatia Mitaji?Tutasimamiaje?

Kwanza kutakuwa na Kikundi cha Wawekezaji(Mtajipa Jina na hata kujisajili BRELA kam UBIA),Pili kutakuwa na Taasisi za Kifedha au Bank kwa ajili ya Usimamizi wa maswala ya Fedha.Mwisho kutakuwa na Facilitators ambao hawa watakuwa na utaalamukuhusu masuala ya Fedha,Biashara,Uchumi na Ujasiriamali na Mwisho kutakuwa na Wajasiriamali.Mjasiriamali anaweza pia kuwa sehemu Wawekezaji.

Wawekezaji wanaweza kuwa ni wafanyakazi au wafanya biashara ambao wanaweza kuwa na utayari wa kuwekeza kiasi fulani cha fedha kila mwezi/kila robo mwaka au kila mwaka.Bank watakuwa na Mfumo wa Usimamizi wa hizi Fedha na kuwapatia wajasiriamali fedha hizo kwa mfumo salama na wa uhakika Mfano(Overdraft).

Kwa nini Overdraft?Overdraft inahakikisha kwamba Mjasiriamali anawajibika katika usimamizi wa Fedha kwani inatokea sana pale ambapo mjasiriamali anapopewa Kiasi cha Fedha kwa mfumo wa Cash basi umakini wa utumiaji na usimamizi wa fedha unakuwa chini,Ili ukimpati overdraft kwanza inakuwa na limit pili matumizi yake yanaweza kusimamiwa kwa kuzingatia vigezo vya kibiashara kama vile mikataba,tender na matumizi mengine.Lakini pia inaweza wekewa kiwango cha maximum kulinganana Budget yake ya uendeshaji hivyo kuondoa uwezekano wa kutumia zaidi.

Facilitators kazi yao ni kutoa utaalamu wao kwa pande zote ni kuibua Red Flags,Hawa ni Auditors na Managers wa Mahusiano kati ya Wajasiriamali na Wawekezaji na wanahakikisha kwamba daima kuna kuwa na uhusiano mzuri baina yao na pia kutoa maoni katika maswala mbalimbali.

Wajasiriamali kazi yao ni kuandaa na kutengeneza bidhaa/huduma au mawazo ya bidhaa au huduma na kuonesha ni kwa kiasi gani wanaweza kuyafanya mawazo hayo yatekelezeke kwa kuzingatia uwezo wao binafsi,fursa zilizopo n.k.

Kama nilivoeleza hapo mwanzoni nimechokoza Mjadala.Mjadala ambao naamni kwamba kuna wataalamu zaidi ambao wanweza kutoa maoni ambayo yatajenga.

Je wewe unafikiri ni njia gani ambazo tunaweza kuzitumia katika kuhamasisha uwekezaji huria na upatikanaji wa mitaji huria?Karibu tujadili

Je unahitaji huduma za ushauri na uelekezi kuhusu biashara yako?Je unahitaji kuanzisha Biashara mpya,kusajili kampuni?Wasiliana nasi kwa email:masokotz@yahoo.com au PM

Muwe na siku Njema.
 
Hii mada ni nzuri sana aiseee nimekuelewa.
Imechukua wiki moja mada kusomwa na kuchangia.Imenipa Picha kwamba Bado Tanzania ni taifa la Wachuuzi na Sio wawekezaji.Hapa nilipo natafakari ni namna gani tunaweza kufanya Taif letu kubadilika.
Nimefurahi kama andiko langu limekupa taarifa
 
Hii idea imesukwa vizuri Sana, tatizo ni jamii tuliyopo watu wanaelimu ndogo Sana kuhusiana na uwekezaji.
Vicoba kuwa venture capital firm inaweza ikawa fresh Ila swali ni itafanyikaje Sera na Sheria za nchi zinazungumziaj vicoba vinafanyika zaidi na wajasiriamali wadogo wenye elimu ndogo Sana mama muuza matunda utamwelezeaje kwamba aweke hela asubiri biashara ikuwe ndio aweze kupata faida wao wanataka Ile mwisho wa mwezi apate chake aendelee kuzungusha biashara yake.
Je Kuna Sheria Tanzania inayomlinda mwekezaji wa vicoba,rejea Mr kuku na wengineo wakiweza kukusanya kiasi kikubwa serikali hiyo hiyo inawapokonya watu wanabaki na vilio.nachoona Sheria za nchi za uwekezaji ziwekwe vizuri na jamii ipewe elimu kuhusu uwekezaji na biashara ndio tutaweza kujikwamua.sasa ivi naona Kuna mwamko watu wanaanza kujifunza ujasiriamali wa kuzalisha bidhaa mbalimbali na viwanda vidogo vimeibuka lkn bado uzalishaji tu hautoshi kufanya biashara isimame Kuna vitu vingi vya ziada mfano marketing,human resource management ukizingatia tz asilimia kubwa ni unskilled labour,how to rise fund km ulivopendekeza angel investors,venture capitalist na hata namba ya kulist company zao kwenye big financial markets ikiwemo stocks na bond bado watz wengi hatuna uelewa wa ivi vitu.wengi wanaamin mtaji unapatikana kwa kufanya saving,kijibana ndio njia pekee lkn mwisho wasiku wanakuja kuathiriwa na emergence na inflation inapelekea Nguvu walizutumia kuwa bure.elimu elimu, elimu na Sera nzuri ndio zitalifikisha taifa linapostahili
 
Hii idea imesukwa vizuri Sana, tatizo ni jamii tuliyopo watu wanaelimu ndogo Sana kuhusiana na uwekezaji.
Vicoba kuwa venture capital firm inaweza ikawa fresh Ila swali ni itafanyikaje Sera na Sheria za nchi zinazungumziaj vicoba vinafanyika zaidi na wajasiriamali wadogo wenye elimu ndogo Sana mama muuza matunda utamwelezeaje kwamba aweke hela asubiri biashara ikuwe ndio aweze kupata faida wao wanataka Ile mwisho wa mwezi apate chake aendelee kuzungusha biashara yake.
Je Kuna Sheria Tanzania inayomlinda mwekezaji wa vicoba,rejea Mr kuku na wengineo wakiweza kukusanya kiasi kikubwa serikali hiyo hiyo inawapokonya watu wanabaki na vilio.nachoona Sheria za nchi za uwekezaji ziwekwe vizuri na jamii ipewe elimu kuhusu uwekezaji na biashara ndio tutaweza kujikwamua.sasa ivi naona Kuna mwamko watu wanaanza kujifunza ujasiriamali wa kuzalisha bidhaa mbalimbali na viwanda vidogo vimeibuka lkn bado uzalishaji tu hautoshi kufanya biashara isimame Kuna vitu vingi vya ziada mfano marketing,human resource management ukizingatia tz asilimia kubwa ni unskilled labour,how to rise fund km ulivopendekeza angel investors,venture capitalist na hata namba ya kulist company zao kwenye big financial markets ikiwemo stocks na bond bado watz wengi hatuna uelewa wa ivi vitu.wengi wanaamin mtaji unapatikana kwa kufanya saving,kijibana ndio njia pekee lkn mwisho wasiku wanakuja kuathiriwa na emergence na inflation inapelekea Nguvu walizutumia kuwa bure.elimu elimu, elimu na Sera nzuri ndio zitalifikisha taifa linapostahili
Mkuu nafurahi kwamba andiko langu umelielewa na umetoa mchango mzuri wa wazi na wa uhakika.Labda niseme tu kwamba mimi ni sehemu ya jamii na haya uliyosema ni sahihi kabisa kwamba kuna changamoto kwenye jamii yetu kuhusu uwekezaji,akiba,biashara na faida.Nakubalina na wewe kwamba tunalo tatizo katika elimu na tunalo tatizo katika desturi za jamii yetu.Ukitaka kuelewa hili jaribu kutazama idadi ya watu ambao wana Bima hata za maisha,mali binafsi, n.k. Wengi Bima hizi wanakata ama kwa sababu ya kulazimika kwa mujibu wa sheria au kwa sababu ya kuwa na uelewa au hofu mfano full cover ya Magari.

Hata hivyo lazima tukubaliana kwamba hizi changamoto ndio tunapaswa kuzifanya ziwe Fursa.Kwa mafno rahisi tu,Ni ukweli usiopingika kwamba kadiri unavyokuwa na idadi kubwa ya watu ambao wamekata BIMA za Maisha,Afya,Biashara etc ndio pia gharama ya Premium inavyoshuka.

Sasa nirudi katika hoja ya Msingi ambayo ndio kiini cha mjadal wetu ambayo ni suala la Venture Capital na Angel Capital Funds.Binafsi hili ni swala ambalo nimeliona kwamba tunalo Tatizo katika mfumo Mzima wa Sera,Sheria na Utamaduni ambao unaongoza hata uelekeo wa Taifa Letu.Watu kama Mr.Kuku ambao Serikali imetumia mwamvuli wa udhaifu wa sheria zetu ama kuwadhulumu wao wenyewe au kudhulumu Maelfu ya Wananchi ambao wamewekeza kupitia kwamba ni dalili ya wazi kwamba Tunayo Serikali ambayo maslahi mapana ya wananchi wake huenda sio kipaumbele chake au likawa ni tatzio la uduni wa uelewa ambao umeathiri Taifa lote kwa ujumla.

Sasa Tufanyeje?Je tukae Kimya?Tuendeleze hizi desturi na kuendelea kubaki nyuma?Je ni hapana ni lazima tuchukue Hatua.Kama watu binafsi na kama Jamii.Kwanza tunaweza kuanza kwa kuandika maandiko kama haya na kuhamamisha mjadala kuhusu Fursa na changamoto kwani kufanya hivyo na kuhamaisha watu wengi wasome na kujifunza ndivyo tunavowezakuhamasisha zaidi mabadiliko.

Kama unavyoona andiko hilo halijapata hamasa ya usomaji kama yalivyo maandiko mengine ambayo kimsingi ni burdani etc.Lakini hali hii inakupa picha ni kwa nini aina hii ya maandiko inakuwa sio maarufu.Ni kwa sababu bado muamko ni Mdogo.

Je Tufanye nini?Kwanza tuendeleze huu mjadala bila kukata tamaa,Pili katika uchache tupeane taarifa kwa ile miradi midogo ambayo imefanya kazi katika mfumo wa VC,AC au hata kwa Mfumo mwingine wowote ule wa mtaji HURIA ambao umeweza kuwa na mabadiliko chanya ili tuweze kuongeza uelewa wa watu na wetu wenyewe na pia ili tuweza kufahamu zaidi kuhusu FURSA na Changamoto na huenda Katika mojawapo ya Jamii tunaweza kupata Suluhu ya Tatizo la Mitaji hasa kwa kutumia Vyanzo vya Mtaji vya ndani.
Andiko hili linaenda sambamba na andiko hili hapa chini.

Fahamu Jinsi ya Kumpatia Mtu Mtaji na Kumasaidia kukuza Biashara yake
Asante na Kila la heri.
 
Back
Top Bottom