From Sir With Love
JF-Expert Member
- Sep 13, 2010
- 2,076
- 3,804
Mimi namwamini Mungu muumba Mbingu na Nchi. Japo haitoshi kwa kusema namwamini kwa sababu Biblia ninayoisoma inasema hata mashetani hutetemeka litajwapo jina LA Mungu.
Naomba nisiwe mdini natoa tu nilichosoma kwenye Biblia kwa sababu sina sehemu nyingine ya kujifunza haya.
Baada ya shetani kutaka kujitukuza na kumpindua Mungu. Basi Mungu alimtupa shetani na malaika zake ambao ndiyo majini duniani. Kwanini Mungu hakumfunga shetani? sijui. Tukifika mbinguni tutamuuliza.
Hawa malaika wa shetani ndiyo majini. Sasa hapa ndo wengi tuna imani tofauti. Mimi sihitaji msaada wa majini kwa sababu ninachokihitaji Mungu aliye mbinguni anauwezo wa kunipa.
Kwa sababu mtu halazimishwi kumuabudu Mungu aliye juu basi wengine huhitaji msaada wa majini. Ukihitaji msaada wa majini kuna malipo utakayolipa. Aidha kwa sadaka au vinginevyo.
Nataka kusisitiza majini yapo kabisa kabisa. Ukikataa hata yenyewe yanashangaa. Ni kama vile unaambiwa mke wako ni mzinzi tumemwona sehemu halafu ukawa unakataa.