..... HATA mchongoma ANAJUA KWANINI AFRICA NI MASIKINI!!
SteveD.
"...Kiwi cha yule ni chema cha;hata ulimwengu uwishe kwani Kivuli cha fimbo hakimfichi mtu jua!"
...naomba unitafsirie maneno yako ya chini, lugha yangu hii sitobisha, saa nyingine inanichenga vibaya sana, na mambo huwa noma kweli kweli kama mafumbo yananijia kutoka kwa wataalam wa lugha kama wewe. Naomba nitangulize shukrani.
SteveD.
Je, wabunge wanapochaguliwa kila mmoja akikatiwa shilindi milioni 50 ya kuzuia kula rushwa itamtosha ili afanye kazi yake yaani ni bonus ya kuchaguliwa...
Nimekaa najiuliza ni jinsi gani watumishi wa serikali kuanzia wa ngazi za chini hadi za juu kabisa wanaweza kuibia serikali na serikali isitambue au ishindwe kuchukua hatua? Inawezekana vipi watu wakawa wanachota fedha za umma kama kuchota maji kwa kata na wakazimeza hata bila ya kuzitafuna? Bila ya shaka kuna mbinu mbalimbali ambazo zinatumika na wajanja hao kula fedha za umma "bila kunawa". Hivi ni mbinu gani zinatumika kuuibia serikali bila ya hata kukamatwa?
NB: Mada hii haina lengo la kufundisha wizi au mbinu za kuuibia serikali bali inataka kuonesha ni mbinu gani zinatumika kuubia serikali. Kama unataka kujua jinsi ya kula fedha za umma, tafadhali jiunge na utumishi wa serikali kwani wapo watu ambao watakuwa tayari kukupa somo "live" as you go along.
Maajabu kesi ya Balozi Mahalu
By Marshy Abdu | Published 10/6/2007 | Habari za Kitaifa | Unrated
Maajabu kesi ya Balozi Mahalu
na Happiness Katabazi
UPANDE wa mashitaka katika kesi ya kuhujumu uchumi inayomkabili aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Italia, Costa Ricky Mahalu na mwenzake, umekiri kwamba hakuna mlalamikaji katika kesi hiyo.