Jinsi uchaguzi wa Serikali za Mtaa ulivyochafuliwa Iringa!!

Izo ni moja ya changamoto zilizo jitokeza, ila kwa waliojiandikisha waende wakachague kiongozi kwakua awa viongozi wa serikali za mitaa ni muhimu na ndio tunaofanyanaokazi kilasiku uku kwenye mitaa yetu muhimu wao ni zaidi ata ya wabunge ambao tuna onana nao marachache sana katika miaka mitano ya utumishi wao.

Hizo ni changamoto au ufedhuli, yote hayo ni kusaka ushindi wa kishindo bila kushindana. Uhanithi mtupu. Na hizi siasa za kishenzi ni za jiwe, hiyo tabia anayo toka akiwa mbunge na waziri, na ndio mbinu alizokuwa anatumia ili kupita bila kupingwa, huku akihadaa umma kuwa anakubalika.
 
Screenshot_20191108-222422-picsay.jpeg
 
Wapinzani hawakutumia busara kujitoa Wamekosea sana

Wafikirie upya
Waliepusha kubambikiwa kesi wakae ndani hadi upite uchaguzi mkuu hivo wameruka mtego wa maelekezo wanyimwe fomu nao wataleta vurugu kudai fomu kisha watabambikwa uhaini au uvunjifu wa mali hivo wakamatwe wote waozee ndani.Wamejifunza kesi waliyonayo chadema
 
Walioharibu mchakato mzima ndio wenye busara? Jipeni moyo tu mmejifhihirisha wazi hadi kwenye grassroot nia yenu. Uzuri wananchi wengi wanaona na sio kusikia au kuambiwa. Hata wana ccm waaminifu wameona mizengwe. Mioyo yoa inajua lakini wamefunga midomo tu
Wapinzani hawakutumia busara kujitoa Wamekosea sana

Wafikirie upya
 
Izo ni moja ya changamoto zilizo jitokeza, ila kwa waliojiandikisha waende wakachague kiongozi kwakua awa viongozi wa serikali za mitaa ni muhimu na ndio tunaofanyanaokazi kilasiku uku kwenye mitaa yetu muhimu wao ni zaidi ata ya wabunge ambao tuna onana nao marachache sana katika miaka mitano ya utumishi wao.
Utachagua nini wakati hamna cha kuchagua? Wenyenchi wameshatuamulia watu wa kutuongoza. Tuombe amani idumu katika mazingira haya magumu.
 
Kulikoni ccm kuumizwa au kusikitika kujitoa kwa upinzani ilitakiwa washangilie kuupata ushindi wa kishindo.Nadhani wanahofia zaidi kunyimwa misaada kwa uonevu juu ya udhalimu wao toka kwa wafadhili.Ssm inaogopa wafadhili japo uwaita mabeberu kuliko kuogopa na kuheshimu wapigakura
 
Sawa lakini eataochaguliwa wanaweza kuishi kama mtoto wa kambo ndani jamii ileile
Waliobaki wanatosha kuendelea na uchaguzi, sio lazima kila chama kishiriki hizi chaguzi.

Kuna vyama viliamshwa usingizini vikatoa tamko kushiriki bila hata kuwa na wagombea, kwasababu tu CHADEMA ilijitoa.

Mbona uchaguzi mdogo singida hawakujali vyama vingine kutoshiriki?!

Waliopo waendelee tu.
 
Waliepusha kubambikiwa kesi wakae ndani hadi upite uchaguzi mkuu hivo wameruka mtego wa maelekezo wanyimwe fomu nao wataleta vurugu kudai fomu kisha watabambikwa uhaini au uvunjifu wa mali hivo wakamatwe wote waozee ndani.Wamejifunza kesi waliyonayo chadema
Kuna watu walitaka CHADEMA wapambane ili ifike mwakani watu wote muhimu wa CHADEMA wawe mahabusu wamekamatwa!!
 
Imenichukua muda mrefu sana kuandika uzi huu, nimekuwa nikiwaza kama wale waliohusika kuuchafua huu uchaguzi ni watu wenye akili timamu ama la. Wengi wanazungumzia uchaguzi huo kiujumla lakini mimi nizungumzie eneo la Manispaa ya Iringa nilipokuwepo.

Kwanza imeshangaza sana ilikuwaje wakati wa kuandikisha kila kituo kilikuwa na ulinzi lakini wakati wa kuchukua na kurudisha fomu ulinzi huo uliondolewa. Kitu gani kilikuwa kinalindwa wakati wa kuandikisha na ni jambo gani lilisababisha polisi waondolewa wakati wa kuchukua na kurudisha fomu.

Vurugu za kunyang'anya fomu zilifanyika kwenye Ofisi za watendaji wa kata, inakuwaje mtendaji wa kata ambaye ni mlinzi wa amani asitoe ripoti kwa polisi kwamba kwenye kituo chake kuna uvunjivu wa amani?

Kwenye kituo cha Mwangata "D" mwandikishaji wa Orodha ya wapiga kura aliondoka kituoni mara mbili kwa siku tofauti akiwa na daftari la wapiga kura na kurudi baadae na daftari lake baada ya masaa mawili. Ofisa wake alipopewa taarifa akadai ni lazima kuwe na Ushahidi, Inawezekanaje Ofisa wa Polisi anayelinda kituo hicho asione kama huo ni uhalifu?

Ofisi ya Kata Ipogolo aliyeingia kupora fomu alifahamika na kuripotiwa polisi ingawa hajakamatwa mpaka leo. Mwanachadema aliyemfukuzia mshirika wa mporaji fomu huyo yeye ndiye aliyekamatwa na kufikishwa kituo cha polisi kwa tuhuma ya kufanya shambulio la kudhuru mwili.

Kata ya Gangilonga kulikuwa na kundi la watu zaidi ya 30 walioshinda kwenye ofisi ya Kata hiyo kwa siku zote 7 na kuzuia watu wa vyama vingine kuchukua fomu. Tukio liliripotiwa Polisi lakini hakuna hatua zilizochukuliwa.

Siku ya Jumapili na Jumatatu karibu watendaji wa kata zote hawakuwepo Ofisini kwao. Inakuwaje Waziri ataje asilimia ya vyama kugombea wakati kwenye kata zingine vyama vingine vilizuiwa kuchukua fomu kwa njia za kihalifu na hajachukua hatua kwa watendaji waliofanya hivyo?
Kwa hiyo haya ndio tuyaamini kuwa ndio ukweli kamili juu ya uchaguzi wa enero husika bila upendeleo wa mlengo flani? Najaribu kuwaza kwa maandishi!
 
Baba au mama ukiona mtoto wako mmoja anamuonea ndugu yake ni lazima umkemee useme acha! Ukikaa kimya huku unaangalia huyu anaeonewa atakuelewaje?
Hao waliokua wanazuia watu wa vyama vingine kuchukua form mlishindwa kuwapa kichapo au wahehe siku hizi na nyie mnavumilia ujinga ujinga.
 
Kwa hiyo haya ndio tuyaamini kuwa ndio ukweli kamili juu ya uchaguzi wa enero husika bila upendeleo wa mlengo flani? Najaribu kuwaza kwa maandishi!
Barua yangu ya kuelezea jambo hili kama nakala iko kwa Jafo na Mkurugenzi anayo. Au niiweke hapa ndiyo uamini?
 
Hayo yote yanazidi kudhihirisha ni jinsi gani ambavyo CCM ni majambazi mpaka kwenye uchaguzi.
 
Back
Top Bottom