Strong ladg
Senior Member
- Jul 15, 2021
- 102
- 277
Afrika Kusini ilipata uhuru mwaka 1994 kutoka kwa utawala wa ubaguzi wa rangi, je ni kwanini? Miongoni mwa sababu zilizochangia ni ubaguzi wa rangi katika mataifa ya Ulaya na Marekani pamoja na vita baridi.
1. UBAGUZI WA RANGI
Wapigania uhuru wa Afrika Kusini walipuuzwa walipojaribu kuomba msaada katika nchi za Magharibi mfano Marekani na Uingereza. Hii ni kwa sababu, ubaguzi wa rangi ulikuwa wa kiwango kikubwa hivyo basi mataifa ya Magharibi hayakuona sababu ya kuwasaidia wapigania uhuru wa Afrika Kusini(weusi) kuutoa madarakani utawala wa watu weupe.
2. VITA BARIDI
Kutokana na kukosa msaada kutoka nchi za Magharibi, wapigania uhuru hawa walienda kuomba msaada kutoka kwa wasovieti. Kutokana na wasovieti kutafuta ushawishi barani Afrika, hawakuchelea mara moja wakaanza kutoa misaada kama silaha pamoja na mafunzo ya kijeshi.
Hili liliwakasirisha na kuwaogopesha viongozi wa mataifa ya Magharibi. Kwa kuhofia kuenea kwa ushawishi wa wasovieti, nchi za Magharibi zikaongeza msaada kwa serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini ili isije kuondolewa madarakani na wapigania uhuru wa Afrika Kusini. Vilevile Marekani na Uingereza zilizokuwa zikiongozwa na Ronald Reagan pamoja na Margaret Thatcher, zilipiga kura ya VETO kuzuia azimio la Umoja wa mataifa kuiwekea vikwazo serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini.
Kutokana na serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini kupewa msaada na nchi za Magharibi, juhudi za wapigania uhuru wa Afrika Kusini zilishindwa kufua dafu. Walikuwa wanapigana na maadui wenye nguvu duniani.
Baada ya tishio la Jumuiya ya kisovieti kuondoka mwishoni mwa miaka ya '80, ghafla nchi za Magharibi zikabadilika. Zikaanza kuiwekea vikwazo serikali ya kibaguzi ya Afrika Kusini, kelele zikaanza kupigwa, makongamano yakafanyika, kampeni mbalimbali zikafanyika, viongozi wakapaza sauti,mashinikizo yakawekwa, ghafla utawala wa kibaguzi uliokuwa mzuri ukageuka ukawa mbaya.
Kutokana na vikwazo pamoja na mashinikizo, hatimaye utawala wa kibaguzi wa Afrika Kusini ukakubali kuachia ngazi .
Hapa ni funzo, mataifa yénye nguvu hayana muda na mambo ya haki za binadamu,demokrasia, utawala bora n.k. Ukisikia wanapiga kelele kuhusu demokrasia, haki za binadamu n.k ujue wanaempigia kelele kakataa kuwa mtumwa wao.