Yusufu R H Sabura
JF-Expert Member
- Jun 26, 2020
- 342
- 471
Nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
Sura ya tano ya ilani ya chama cha mapinduzi 2020-2025 imeeleza, kwanza mafanikio iliyoyapata katika sekta ya ulinzi na usalama katika awamu ya utekelezaji iliyopita, kisha ikaeleza ni mambo gani itayafanya katika sekta hiyo ikiwa chama kitapata tena ridhaa ya kuliongoza taifa letu.
Katika uzi huu mfupi, ikiwa ni mwendelezo wa threads za bampa to bampa kuelekea uchaguzi mkuu wa 2025, nitajaribu kuangazia ibara moja tu kati ya ibara nyingi zilizomo ndani ya msahafu huo wa chama cha mapinduzi. ibara ya 105 kifungu kidogo (a) na kifungu kidogo (m).
105. Katika miaka mitano ijayo, Chama Cha Mapinduzi kitaendelea kuhimiza
serikali zake kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi yetu, raia wake na
mali zao ili kudumisha umoja, mshikamano, amani na utulivu ambazo ni
tunu kuu za Taifa letu. Katika kufikia malengo hayo, Chama kitaelekeza
Serikali kutekeleza yafuatayo:
(a) Kuimarisha ulinzi na usalama wa nchi na mipaka yake ili kudumisha
Muungano, kulinda Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, umoja,
mshikamano, amani na usalama wa raia na mali zao;
Katika utekelezaji wa kifungu kidogo (a), serikali ya chama cha mapinduzi imefanya yafuatayo;
*Serikali imeongeza nguvu kazi kwa kutoa vibali vya ajira kwa majeshi yote tangu tu Rais Samia alipoingia madarakani. Sote ni mashahidi tuliposikia ajira hizi zimetoka tulizishambulia kwa namna ambayo haijawahi kutokea. Tumeomba ajira JWTZ, TANPOL, TANPRISONS, pamoja na FIRE. Yote hii ni kuhakikisha kwamba ulinzi na usalama unaimarika katika taifa letu.
*Kuendeshwa kwa mazoezi ya utayari yanayofanywa na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), mfano wa mazoezi hayo ni pamoja na;
-Mazoezi ya utayari wa majeshi ya EAC
-Zoezi KAA TAYARI na
-Mazoezi ya pamoja kati ya Jeshi la Wananchi na Jeshi la Ukombozi la China.
*Uongezwaji wa magari ya kijeshi pamoja na ndege vita , hili tumelishuhudia kwenye kilele cha maadhimisho ya miaka 60 ya JWTZ.
Hii yote ni dhamira njema ya Chama cha mapinduzi katika kuliongoza taifa hili.
Kifungu kidogo (M)
(m) Kuendeleza ushirikiano na vyombo vya ulinzi na usalama vya nje
ya nchi pamoja na taasisi mbalimbali za kimataifa (Interpol) katika
kukabiliana na kupambana na matishio ya kiusalama na makosa
yanayovuka mipaka hususan ugaidi, makosa ya kimtandao (cyber-
crime), uharamia, utakatishaji fedha haramu, biashara haramu ya
madawa ya kulevya, usafirishaji haramu wa binadamu, ujangili na
bidhaa bandia;
Katika kulitekeza hili, tumeshuhudia JWTZ, polisi na magereza yakifanya joint cooperations na majeshi ya nje ili kufikia goli. tumeona pale mazoezi ya pamoja ya nchi zinazounda umoja wa EAC, lakini pia hivi karibuni katika kuadhimisha miaka 60 ya JWTZ tumeona zoezi kubwa kabisa la kimedani kati ya JWTZ na Jeshi la Ukombozi la China. hii yote ni kuhakikisha amani inakuwepo ili mambo mengine yaende bila kukwama.
Mafanikio ya jitihada hizi ni amani na utulivu tunaoendelea kuufaidi kama watanzania. Amani ndio msingi wa kila kitu kuanzia haki za binadamu, haki za kiraia, haki za kiuchumi na haki za kisiasa. Kwa utekelezaji huu, hili halina ubishi kuwa wananchi wanakwenda kuamua nani ni nani katika chaguzi kuu zinazokaribia, niwaibie siri tu, safari hii wapinzani watang'olewa meno bila ganzi.
Aidha serikali ya Rais Samia iendelee kuvisimamia vyombo vya ulinzi na usalama katika kudumisha amani ya taifa letu kwa kuzingatia ukweli kuwa, tunaelekea katika chaguzi kubwa mbili na za moto kwelikweli, vyombo vya ulinzi vikae macho kwani ni katika milango hiyohiyo maadui huweza kupenyeza na kuleta political dis orders kwa manufaa yao binafsi.
Asante na Kazi Iendelee.
Yusufu R H Sabura
0750883466/0717934194.