Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 8,490
- 14,991
Nip kwenye kutafsiri kitabu cha Malcom X, jamaa maishani mwake kapitia uhuni mwingi sana. Pia alikuwa na marafiki wahuni balaa. mmoja wa rafiki yake huyu aliitwa Sammy The Pimp(Kuwadi Sammy). Hivi ndivyo alikuwa akipata makahaba wa kuwauza.
Sammy alikuwa amempa mimba msichana mmoja huko kwao Paducah, Kentucky. Wazazi wa msichana huyo walikasirika sana hadi ikambidi Sammy kukimbilia Harlem, alipofika alipata kazi kama mhudumu mgahawani. Alikuwa akiangalia mwanamke aliyekuja kula akiwa peke yake, baada ya kugundua kuwa hajaolewa wala haishi na mtu, alifanya mbinu kumzoea. Haikuwa vigumu kwa mtu mjanja kama Sammy kukaribishwa nyumbani kwa mwanamke. Alipofika aliomba kwenda nje mara moja kununua chakula, na alipotoka alienda haraka kuchongesha funguo ya pili. Siku alipofahamu kuwa mwanamke yule amesafiri, alienda na kukomba vitu vyake vya thamani vyote. Kisha baada ya hayo alijitolea kumsaidia pesa kidogo kuanza upya. Huo ulikuwa mwanzo wa utegemezi wa kifedha na kihisia ambao Sammy alijua kuuendeleza hadi mwanamke yule alipokuwa kama mtumwa wake.