Jinsi Nilivyojifadhili Chuo cha kati na sasa chuo kikuu bila backup yoyote

Street brain

JF-Expert Member
Oct 24, 2022
608
808
Habari Wana Jf🚀 Stori Yangu ya Maisha – Safari ya Kupambana na Changamoto!

Hello wana jf! 🙌 Leo nataka kushare na nyinyi hadithi yangu ya maisha – jinsi nilivyopambana na masomo huku nikicheza "survival mode" kama mchezaji wa kweli! 😎 Bado siko kwenye “hero” level, lakini niko njiani, na nataka tushiriki hii journey pamoja. 🎯

Mwanzo wa Safari Yangu
Mimi ni kijana kutoka familia ya hali ya chini, ambapo hata kupata chakula cha mara mbili kwa siku ilikuwa changamoto. Lakini ndoto yangu ya kusoma haikukata tamaa. Baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka 2020, nilichaguliwa kujiunga na chuo cha uhasibu huko Babati, Manyara, kusoma Accountancy. Ada ilikuwa TZS 883,000 – hela ambayo kwa familia yangu ilikuwa kama kutaka kuomba mvua ikanyeshe dhahabu! 😅

Hali nyumbani ilikuwa ngumu. Baba yangu, ambaye alipata ajali miaka ya nyuma, alikuwa akifanya kazi za kupita nayo tu, na mama ndiye aliyekuwa mpambanaji wa kweli. Hakuna aliyesoma katika ukoo wetu, hivyo mimi nilikuwa wa kwanza kuyakanyaga maeneo ya chuo – kwa neema za Mungu.

Ili kulipa ada, niliingia msituni kukata mkaa. 🪓 Hii siyo kazi rahisi, lakini nilipambana hadi Oktoba 2020, nikapata karibu TZS 1.5M. Hela hiyo ikawa mtaji wangu wa kuanza maisha chuoni. Bila ndugu wala jamaa huko Babati, nilisafiri peke yangu, nikijua Mungu ndiye atakayeamua hatima yangu. 🛤️

Changamoto za Wazazi Wangu
Wazazi wangu walitamani niende shule, lakini hawakuwa na uwezo wa kulipa ada. Sikuwa nataka kuwapa stress, kwa hivyo niliamua kujituma peke yangu. Baba yangu alinipa maneno ya kiume: “Wewe ni mwanaume, nenda huko utajua cha kufanya!” Akapiga kiburi chake cha kifua, akasema kwaheri. 😢 Mama na ndugu zangu walinishauri nisome kwa bidii, nisichanganyike na makundi mabaya, na nisivute bangi wala pombe. Waliniambia nikumbuke maisha magumu niliyotoka, na nisije nikawakatisha tamaa.

Safari ya Kuelekea Manyara
Asubuhi moja, wazazi wangu, ndugu zangu, na mimi tulielekea stendi. Nilisafiri kutoka Kigoma hadi Manyara, safari iliyokuwa na changamoto zake. Nilifika asubuhi, nikaenda chuo moja kwa moja na kujisajili. Halafu ikabidi niwapo – hostel au ghetto? Ghetto ikawa chaguo langu kwa sababu ilikuwa nafuu. Nilipata chumba cha TZS 90,000 kwa miezi tatu (TZS 30,000 kwa mwezi). 😎

Nikanunua vitu vya msingi: godoro la 2x6, sufuria mbili, bakuli, jiko la gesi, unga wa 20kg, na dagaa 1kg. Maisha yakaanza! Nilianza kuhudhuria masomo, nikapata marafiki wapya, na nikaweka bidii sana kwenye masomo. Kwa kuwa nilikuwa nimelipa ada ya mwaka mzima, stress ya ada haikunikumba… hadi hela zikaanza kupungua. 😓

Mtonyo Unakata!
Katikati ya semester ya kwanzai, hela zilipungua hadi TZS 30,000. Nilitafuta kazi kwa wiki tatu bila mafanikio. Nyumbani hawakuwa na hata TZS 5,000 za kunisaidia. Stress ilianza kunisumbua, nikaanza kuzeeka nikiwa na miaka 19 tu! 😅 Nilipunguza milo hadi moja kwa siku – unga na dagaa tu. Kulikuwa na siku ambapo unga uliisha wiki mbili kabla ya mitihani (UE), na nyumbani hawakuwa na lolote. Niliwaza sana, nikijiuliza kwa nini nilikuja chuo. 😢

Lakini sikukata tamaa. Niliingia mtaani, nikapata kazi za saidia fundi. Nilipata TZS 7,000 kwa siku pamoja na msosi. Nilikaa wiki na siku tatu nikifanya kazi hiyo, lakini Jumatatu ilifika na kulikuwa na mtihani! Sikuwa nimesoma, lakini nikaingia chumba cha mitihani na kufanya mtihani “fresh”. 😅

Matokeo ya semester ya kwanza yalipotoka, nilipata “A” tano na supplementary moja(communication skills). GPA yangu ilikuwa ya juu kabisa darasani – nikajipa moyo! Semester ya pili, fundi wangu alianza kunikubali kwa uchapakazi wangu. Alinipigia simu hata nikiwa chuoni, nikaacha masomo na kwenda kufanya kazi. Nilipambana na coursework na mitihani, nikapata “A” nne, B+ moja, na supplementary moja (costing).

Likizo ya Miezi Minne
Likizo ndefu ilipofika, nilitumia fursa hiyo kutafuta hela za diploma. Nilipata fundi aliyenilipa TZS 10,000 kwa siku pamoja na msosi. Nilikuwa nimeanza kujua baadhi ya mambo ya ujenzi, hivyo alinikubali sana. Kabla ya kufanya mitihani ya supplementary, nilisoma kwa bidii. Mitihani ya communication na cost accounting ilikuwa ngumu, lakini nilifaulu zote – na nilikuwa mmoja wa watu wachache waliopita somo hayo kati ya wote maana kama costing nilichomoa mwenyewe 🙌

Baada ya hapo, niliendelea na kazi za ujenzi. Nilipata hela ya kutosha kulipa ada ya diploma na kodi. Nilipofanya field training katika shirika fulani, walinikubali sana kwa uchapakazi wangu. Walinilipa posho nzuri, na baada ya field kumalizika, walinikubali nibaki nao! 😎 Hii ilinipa hela ya kutosha kulipa ada ya mwaka mzima na kodi. Niliporudi chuoni, chakula kilikuwa hakikuwa shida, na niliweka bidii sana kwenye masomo.

Kuhitimu Diploma! 🎓
Siku ya mtihani wa mwisho wa diploma, nilikaa chini na kulia kwa hisia. 😭 Nilifikiria changamoto zote – jinsi nilivyopambana peke yangu bila msaada wa ndugu wala jamaa. Nilimaliza diploma ya uhasibu na GPA ya 4.5/5! Hii ilikuwa ushindi wa kweli. Lakini baada ya kuhitimu, nikaapa kutoendelea na degree kwa sababu ya uchovu wa kupambana.

Kuingia Mtaani na Biashara
Nikaanza kutafuta kazi, lakini ajira ilikuwa ngumu kupata. Hata kujitolea ilikuwa changamoto! 😅 Nikapiga kazi za mjengo na kazi nyingine za vibarua hadi nikapata TZS 900,000. Niliamua kuanza biashara – ama kuuza matunda au viatu vya mtumba. Nilichukua muda kufanya utafiti kabla ya kuanza. Lakini…

Ulaghai wa “Ndugu” 😡
Mnamo Agosti 2023, baba yangu akanipigia simu akisema amekutana na “ndugu” yake anayesema kuna kazi za serikali (TRA). Jamaa alidai ni mhasibu wa TRA na akaniambia nitume CV yangu. Alisema hata kama matokeo ya diploma hayajatoka, atanipa kazi yenye mshahara wa TZS 1.5M. Akaniambia lazima “ahonge” TZS 2M, lakini yeye atachangia TZS 1M na mimi nitoe TZS 1M. Nilimwambia sina hela, akasema nitoe TZS 800,000. Ingawa iliniuma, nilikubali na kutuma hela hiyo pamoja na CV yangu. 😞

Wiki zilipopita, jamaa hakupokea simu zangu. Nilipompigia kwa namba nyingine, alipokea, na nikairekodi mazungumzo yetu (bado nina rekodi hiyo!). Yule jamaa aliniibia hela yangu, na kazi sikupata. Nilivunjika moyo sana, na baba yangu aliumia akidhani yeye ndiye sababu. Lakini mimi ni mpambanaji – niliacha lipite, lakini nikaapa siku nikimpata huyo “ndugu,” sitajua nitamudu vipi! 😤

Degree na Maisha ya Arusha
Baada ya matokeo ya diploma kutoka, nikaamua kusoma degree katika Institute of Accountancy Arusha (IAA)baada ya kupata mkopo wa TZS 600,000. Lakini maisha ya Arusha yalikuwa tofauti na Manyara – gharama za maisha zilikuwa za juu! Hela ya mkopo haikutosha kulipa ada, kodi, na chakula. 😓

Sasa niko mwaka wa pili wa degree yangu, naishi kwa neema za Mungu. Kupata kazi hapa Arusha ni ngumu sana. Nimepambana hadi nimeamua kuandika hii stori hapa ili niombe msaada wa kazi. Nina diploma ya uhasibu, niko fresh kwenye kompyuta, na kazi za nguvu nazipiga bila aibu! Nataka kazi yoyote – iwe ya kutumia akili au nguvu – ilimradi ni halali. 🙏

Ombi Langu
Kama kuna mtu anajua kazi yoyote ndani ya Arusha – iwe kumwagilia bustani, kazi za ujenzi, au kazi ya uhasibu – naomba mnisaidie. Nina uwezo, bidii, na moyo wa kujifunza. Tafadhali nipigie DM au nipatie barua pepe kwa: clementedward49@gmail.com. 🚀

Ahsanteni sana kwa kusoma hadithi yangu!Nawashukuru kwa kunipa nafasi ya kushare. Kama unaweza kunisaidia na kazi au ushauri, usisite kuniandikia.
clementedward49@gmail.com
 
Sijaelewa hapo kwenye mkopo wa 600,000.

HESLB ndiyo walikupa mkopo wa ada laki sita?

Kama ndivyo maana yake ukipata ada automatically unakuwa umepata 'boom' (meals and accommodations) ambayo kwasasa haipungui 630,000 kila baada ya siku 70 hivi.

Je, hilo 'boom' umeshindwa kujipangilia kulipa ada kidogo kidogo ndani ya semester na ukabaki na akiba kidogo kwa ajili ya matumizi mengineyo?

Maana nilisoma na washkaji walikuwa wanapata 'boom' pekee hawakupata ada hata senti lakini wali manage kulipa ada na wakajibana kupata hela ya matumizi.
 
Habari Wana Jf Stori Yangu ya Maisha – Safari ya Kupambana na Changamoto!

Hello wana jf! Leo nataka kushare na nyinyi hadithi yangu ya maisha – jinsi nilivyopambana na masomo huku nikicheza "survival mode" kama mchezaji wa kweli! Bado siko kwenye “hero” level, lakini niko njiani, na nataka tushiriki hii journey pamoja.

Mwanzo wa Safari Yangu
Mimi ni kijana kutoka familia ya hali ya chini, ambapo hata kupata chakula cha mara mbili kwa siku ilikuwa changamoto. Lakini ndoto yangu ya kusoma haikukata tamaa. Baada ya kumaliza kidato cha nne mwaka 2020, nilichaguliwa kujiunga na chuo cha uhasibu huko Babati, Manyara, kusoma Accountancy. Ada ilikuwa TZS 883,000 – hela ambayo kwa familia yangu ilikuwa kama kutaka kuomba mvua ikanyeshe dhahabu!

Hali nyumbani ilikuwa ngumu. Baba yangu, ambaye alipata ajali miaka ya nyuma, alikuwa akifanya kazi za kupita nayo tu, na mama ndiye aliyekuwa mpambanaji wa kweli. Hakuna aliyesoma katika ukoo wetu, hivyo mimi nilikuwa wa kwanza kuyakanyaga maeneo ya chuo – kwa neema za Mungu.

Ili kulipa ada, niliingia msituni kukata mkaa. 🪓 Hii siyo kazi rahisi, lakini nilipambana hadi Oktoba 2020, nikapata karibu TZS 1.5M. Hela hiyo ikawa mtaji wangu wa kuanza maisha chuoni. Bila ndugu wala jamaa huko Babati, nilisafiri peke yangu, nikijua Mungu ndiye atakayeamua hatima yangu.

Changamoto za Wazazi Wangu
Wazazi wangu walitamani niende shule, lakini hawakuwa na uwezo wa kulipa ada. Sikuwa nataka kuwapa stress, kwa hivyo niliamua kujituma peke yangu. Baba yangu alinipa maneno ya kiume: “Wewe ni mwanaume, nenda huko utajua cha kufanya!” Akapiga kiburi chake cha kifua, akasema kwaheri. Mama na ndugu zangu walinishauri nisome kwa bidii, nisichanganyike na makundi mabaya, na nisivute bangi wala pombe. Waliniambia nikumbuke maisha magumu niliyotoka, na nisije nikawakatisha tamaa.

Safari ya Kuelekea Manyara
Asubuhi moja, wazazi wangu, ndugu zangu, na mimi tulielekea stendi. Nilisafiri kutoka Kigoma hadi Manyara, safari iliyokuwa na changamoto zake. Nilifika asubuhi, nikaenda chuo moja kwa moja na kujisajili. Halafu ikabidi niwapo – hostel au ghetto? Ghetto ikawa chaguo langu kwa sababu ilikuwa nafuu. Nilipata chumba cha TZS 90,000 kwa miezi tatu (TZS 30,000 kwa mwezi).

Nikanunua vitu vya msingi: godoro la 2x6, sufuria mbili, bakuli, jiko la gesi, unga wa 20kg, na dagaa 1kg. Maisha yakaanza! Nilianza kuhudhuria masomo, nikapata marafiki wapya, na nikaweka bidii sana kwenye masomo. Kwa kuwa nilikuwa nimelipa ada ya mwaka mzima, stress ya ada haikunikumba… hadi hela zikaanza kupungua.

Mtonyo Unakata!
Katikati ya semester ya kwanzai, hela zilipungua hadi TZS 30,000. Nilitafuta kazi kwa wiki tatu bila mafanikio. Nyumbani hawakuwa na hata TZS 5,000 za kunisaidia. Stress ilianza kunisumbua, nikaanza kuzeeka nikiwa na miaka 19 tu! Nilipunguza milo hadi moja kwa siku – unga na dagaa tu. Kulikuwa na siku ambapo unga uliisha wiki mbili kabla ya mitihani (UE), na nyumbani hawakuwa na lolote. Niliwaza sana, nikijiuliza kwa nini nilikuja chuo.

Lakini sikukata tamaa. Niliingia mtaani, nikapata kazi za saidia fundi. Nilipata TZS 7,000 kwa siku pamoja na msosi. Nilikaa wiki na siku tatu nikifanya kazi hiyo, lakini Jumatatu ilifika na kulikuwa na mtihani! Sikuwa nimesoma, lakini nikaingia chumba cha mitihani na kufanya mtihani “fresh”.

Matokeo ya semester ya kwanza yalipotoka, nilipata “A” tano na supplementary moja(communication skills). GPA yangu ilikuwa ya juu kabisa darasani – nikajipa moyo! Semester ya pili, fundi wangu alianza kunikubali kwa uchapakazi wangu. Alinipigia simu hata nikiwa chuoni, nikaacha masomo na kwenda kufanya kazi. Nilipambana na coursework na mitihani, nikapata “A” nne, B+ moja, na supplementary moja (costing).

Likizo ya Miezi Minne

Likizo ndefu ilipofika, nilitumia fursa hiyo kutafuta hela za diploma. Nilipata fundi aliyenilipa TZS 10,000 kwa siku pamoja na msosi. Nilikuwa nimeanza kujua baadhi ya mambo ya ujenzi, hivyo alinikubali sana. Kabla ya kufanya mitihani ya supplementary, nilisoma kwa bidii. Mitihani ya communication na cost accounting ilikuwa ngumu, lakini nilifaulu zote – na nilikuwa mmoja wa watu wachache waliopita somo hayo kati ya wote maana kama costing nilichomoa mwenyewe

Baada ya hapo, niliendelea na kazi za ujenzi. Nilipata hela ya kutosha kulipa ada ya diploma na kodi. Nilipofanya field training katika shirika fulani, walinikubali sana kwa uchapakazi wangu. Walinilipa posho nzuri, na baada ya field kumalizika, walinikubali nibaki nao! Hii ilinipa hela ya kutosha kulipa ada ya mwaka mzima na kodi. Niliporudi chuoni, chakula kilikuwa hakikuwa shida, na niliweka bidii sana kwenye masomo.

Kuhitimu Diploma!
Siku ya mtihani wa mwisho wa diploma, nilikaa chini na kulia kwa hisia. Nilifikiria changamoto zote – jinsi nilivyopambana peke yangu bila msaada wa ndugu wala jamaa. Nilimaliza diploma ya uhasibu na GPA ya 4.5/5! Hii ilikuwa ushindi wa kweli. Lakini baada ya kuhitimu, nikaapa kutoendelea na degree kwa sababu ya uchovu wa kupambana.

Kuingia Mtaani na Biashara
Nikaanza kutafuta kazi, lakini ajira ilikuwa ngumu kupata. Hata kujitolea ilikuwa changamoto! Nikapiga kazi za mjengo na kazi nyingine za vibarua hadi nikapata TZS 900,000. Niliamua kuanza biashara – ama kuuza matunda au viatu vya mtumba. Nilichukua muda kufanya utafiti kabla ya kuanza. Lakini…

Ulaghai wa “Ndugu”
Mnamo Agosti 2023, baba yangu akanipigia simu akisema amekutana na “ndugu” yake anayesema kuna kazi za serikali (TRA). Jamaa alidai ni mhasibu wa TRA na akaniambia nitume CV yangu. Alisema hata kama matokeo ya diploma hayajatoka, atanipa kazi yenye mshahara wa TZS 1.5M. Akaniambia lazima “ahonge” TZS 2M, lakini yeye atachangia TZS 1M na mimi nitoe TZS 1M. Nilimwambia sina hela, akasema nitoe TZS 800,000. Ingawa iliniuma, nilikubali na kutuma hela hiyo pamoja na CV yangu.

Wiki zilipopita, jamaa hakupokea simu zangu. Nilipompigia kwa namba nyingine, alipokea, na nikairekodi mazungumzo yetu (bado nina rekodi hiyo!). Yule jamaa aliniibia hela yangu, na kazi sikupata. Nilivunjika moyo sana, na baba yangu aliumia akidhani yeye ndiye sababu. Lakini mimi ni mpambanaji – niliacha lipite, lakini nikaapa siku nikimpata huyo “ndugu,” sitajua nitamudu vipi!

Degree na Maisha ya Arusha
Baada ya matokeo ya diploma kutoka, nikaamua kusoma degree katika Institute of Accountancy Arusha (IAA)baada ya kupata mkopo wa TZS 600,000. Lakini maisha ya Arusha yalikuwa tofauti na Manyara – gharama za maisha zilikuwa za juu! Hela ya mkopo haikutosha kulipa ada, kodi, na chakula.

Sasa niko mwaka wa pili wa degree yangu, naishi kwa neema za Mungu. Kupata kazi hapa Arusha ni ngumu sana. Nimepambana hadi nimeamua kuandika hii stori hapa ili niombe msaada wa kazi. Nina diploma ya uhasibu, niko fresh kwenye kompyuta, na kazi za nguvu nazipiga bila aibu! Nataka kazi yoyote – iwe ya kutumia akili au nguvu – ilimradi ni halali.

Ombi Langu
Kama kuna mtu anajua kazi yoyote ndani ya Arusha – iwe kumwagilia bustani, kazi za ujenzi, au kazi ya uhasibu – naomba mnisaidie. Nina uwezo, bidii, na moyo wa kujifunza. Tafadhali nipigie DM au nipatie barua pepe kwa: clementedward49@gmail.com.

Ahsanteni sana kwa kusoma hadithi yangu!Nawashukuru kwa kunipa nafasi ya kushare. Kama unaweza kunisaidia na kazi au ushauri, usisite kuniandikia.
clementedward49@gmail.com
Hayo maisha tunayapitia wengi tuna jiita "self made man" ila una kipaji cha kazi kwanini unalazimiasha kusoma degree wakati hata hiyo diploma inatosha kwa kupata ajira mkuu?, hiyo kasumba ya kusaka mpaka degree inawaponza sanaa mkuu, mwishowe ukikosa ajira utashauriwa kuenda Veta.
 
Hayo maisha tunayapitia wengi tuna jiita "self made man" ila una kipaji cha kazi kwanini unalazimiasha kusoma degree wakati hata hiyo diploma inatosha kwa kupata ajira mkuu?, hiyo kasumba ya kusaka mpaka degree inawaponza sanaa mkuu, mwishowe ukikosa ajira utashauriwa kuenda Veta.
Daaah mkuu sikuwa na namna
 
Sijaelewa hapo kwenye mkopo wa 600,000.

HESLB ndiyo walikupa mkopo wa ada laki sita?

Kama ndivyo maana yake ukipata ada automatically unakuwa umepata 'boom' (meals and accommodations) ambayo kwasasa haipungui 630,000 kila baada ya siku 70 hivi.

Je, hilo 'boom' umeshindwa kujipangilia kulipa ada kidogo kidogo ndani ya semester na ukabaki na akiba kidogo kwa ajili ya matumizi mengineyo?

Maana nilisoma na washkaji walikuwa wanapata 'boom' pekee hawakupata ada hata senti lakini wali manage kulipa ada na wakajibana kupata hela ya matumizi.
Nina boom pekee kwa mwaka ni 2.4m then ada ni 1.853m ukitoa hapo inabaki kidogo bado kulipa kodi na kula na baadhi ya stationeries, ni ndogo boss wangu
 
Kazi jipe kipaumbele kwasasa kuliko kusoma, hiyo elimu ulio nao inakutosaha kutajirika kama wewe ni mchapa kazi, kama we unapanga kwa ajiliwa hapo ndo umebugi mkuu,
Kuajiriwa hayo ni majaliwa nilikuw na seek kama kutakuwa na vikazi vya day nipige tu ili kwa kipindi hiki nijipange nimalize hizi elimu
 
Sijaelewa hapo kwenye mkopo wa 600,000.

HESLB ndiyo walikupa mkopo wa ada laki sita?

Kama ndivyo maana yake ukipata ada automatically unakuwa umepata 'boom' (meals and accommodations) ambayo kwasasa haipungui 630,000 kila baada ya siku 70 hivi.

Je, hilo 'boom' umeshindwa kujipangilia kulipa ada kidogo kidogo ndani ya semester na ukabaki na akiba kidogo kwa ajili ya matumizi mengineyo?

Maana nilisoma na washkaji walikuwa wanapata 'boom' pekee hawakupata ada hata senti lakini wali manage kulipa ada na wakajibana kupata hela ya matumizi.
Kama ada ni zaidi ya milioni na nusu ni ngumu sana kuafford kama hana msaada nje ya hiyo boom labda kama ada ingekuwa milioni moja kamili....kama vyuo tulivyosoma wahenga wakati huo ada hadi laki 9 au milioni kamili hapo una mkopo 100% dah maisha yanaenda kasi sana
 
May God bless you bro
Mkuu usigang'anie kumaliza degree unaweza kukatisha hata kwa mwaka moja kwanza utafute pesa sisi ambao ni "self made man" kuomba omba misaada ni mwiko kabisa pambana utaweza tatizo akili zako umezifunga kwenye degree, mimi ni lisaafiri ughaibuni na nikajipokea mwenyewe ughaibuni sina ndgu jamaa au rafiki ila nilitomboa tu bila kuomba omba msaada baada ya kumaliza kazi nikapewa offer ya kusoma tena ila nikaona hakuna haja ya kusoma tena pesa ninao, plz think beyond getting a mere degree,
 
Hayo maisha tunayapitia wengi tuna jiita "self made man" ila una kipaji cha kazi kwanini unalazimiasha kusoma degree wakati hata hiyo diploma inatosha kwa kupata ajira mkuu?, hiyo kasumba ya kusaka mpaka degree inawaponza sanaa mkuu, mwishowe ukikosa ajira utashauriwa kuenda Veta.
Kweli. Kuna mshikaji nipo nae around anawsza madigrii tu? Saa anayomawili na bado anawaza lingine? Maisha magumu stress nyingi.
Sisi waafrika kuondoa kasumba vichwani kwetu itachukua mihongo mingi.
Kuna dada mmoja nimemuona tiktok akihojiwa kuhusu uwekezaji wa mifugo.
Anadai toka mwaka 2023 mpaka sasa
Aliweza kununua heka 2 na nusu dsm na kuanza kufuga kuku 100.
Mpaka sasa ana Broiler elf 20000 na kuku za kienyeji 3000.Ana mbuzi ng'ombe na nguruwe zisizopungua 100.
Lau kama Akili kama ya huyu dada ingehamia kwa sisi watanzania tulio wengi tungekuwa mbali sana.
 
Kwa watu wa asili ya kigoma aka waha I have no doubt about your uwezo na bidii Kila eneo la Maisha iwe shuleni ama kwenye biashara,kazi za nguvu ndio mlio na stamina kuliko all tribe.
Nimesoma na waha tabora boys walikuwa wanaongoza Kila darasa vilaza ni hakuna.
Hata ukipata binti wa kiha you won't regret in your life.
Sema Ile sifa ya uchawi inawaharibia ba chuma ulete waha wanayo sana.
Am sure kazi utapata tu.
Kuna Engineer mmoja anaweza kukuunganisha sekta za ujenzi sema contact Kama sinazo.
Yuko hapo hapo mjini.
Hata kazi za temporary pia zinakufaa.
Check mchongo wa scholarship pia ukipata usepe nje itabadilisha your bloodline dogo.
Sijajua if you've passion ya nje .
Sina zaidi
 
Back
Top Bottom