Jinsi maamuzi mabovu yalivyoifilisi benki ndani ya saa 48, wateja waliomba kutoa dola bilioni 42 kwa siku moja(Mara mbili ya bajeti ya Tanzania)

Hizi mada watanzania wengi hawataki kuzielewa na kujifunza na kila mtu analalamima eti maisha ni magumu
Fedha wamarekani wamewanunulia silaha Ukraine 🤸🤸🤸.Mr.Moskovistch pale alipo anashushia vodka huku akiwa amekunja 4.Akisema safi sana vituo vinavyofuata niii,Berlin na London🏃
 
Tatizo lilianzia mwaka 2003, Rais wa wakati huo, George Bush alisain 'American dream' iliyojumuisha ndoto ya kila Mmarekani awe na nyumba. Masharti yalilegezwa na watu wengi walikopesheka, nyumba nyingi zikajengwa(Biashara ya makazi ililipa sana watu wakawekeza zaidi) na watu kununua kwa mkopo.

Mwaka 2007/08 watu wengi wakashindwa kuendelea kulipa hii mikopo kwa sababu ilitolewa kwa sera kuliko kupima uwezo wao wa kulipa. Kwa kawaida ukishindwa kulipa benki hurudi sokoni na kuuza ili kufidia deni. Wafilisi wakaenda sokoni kwa pamoja, nyumba zikawa nyingi sana sokoni na kawaida vitu vikizidi kuliko uhitaji huwa vinashuka bei, Marekani ikashuhudia anguko kali la bei kwenye sekta ya nyumba na bado zikawa haziuziki kwa urahisi.

Hii ikaleta 'panic' na soko la nyumba likafeli rasmi, kumbuka mzunguko mkubwa wa pesa umeshikiliwa na sekta ya makazi. Mabenki na 'hedge funds' vikaathirika pakubwa. Mwaka 2008 Lehman brothers akadondoka ikiwa ni anguko kubwa zaidi kwenye sekta ya fedha Marekani.

Nchi zilizoendelea mabenki ni muhimu sana kwenye uchumi, kuyumba kwao kukapelekea sekta nyingi kukwama. Watu wakaacha kufanya manunuzi wakilinda walichonacho na wengine wakashindwa kukopa ili kufanya manunuzi. Uzalishaji ukapungua na ajira zikapotea. Mzunguko wa mchakato huu ukapelekea mdororo wa uchumi ukiwa mkubwa zaidi baada ya mdororo uliosababishwa na vita kuu ya pili ya dunia.

Imani yangu umepata mwanga kilichotokea.
Swadakta kabisa mkuu.
Sasa huo mdororo uliathiri vipi nchi za Afrika? Ukizingatia hatutumii sana bidhaa za marekani na sera yao ya makazi haikutugusa.
Kingine tuna lipi la kujifunza kutoka kwenye 2008 crisis na hii ya Silicon Valley Bank ukieleza at individual au social level itakua poa serikali ina washauri wake nadhani. Nawasilisha.
 
Exchange rate inaporomoka inaathiri mpaka importation mwisho wa siku production inapungua

Enheee swali jingine
 
Swadakta kabisa mkuu.
Sasa huo mdororo uliathiri vipi nchi za Afrika? Ukizingatia hatutumii sana bidhaa za marekani na sera yao ya makazi haikutugusa.
Kingine tuna lipi la kujifunza kutoka kwenye 2008 crisis na hii ya Silicon Valley Bank ukieleza at individual au social level itakua poa serikali ina washauri wake nadhani. Nawasilisha.
Uchumi wa Afrika mafungamano yake na uchumi wa dunia sio makubwa kupitiliza hivyo hata kuathirika kwake sio kwa ukubwa huo. Kutokana na manunuzi ya bidhaa kushuka Marekani na sehemu nyingine, Afrika ikaathirika mauzo yake kwenda nje ya nchi na kwa Afrika nchi iliyoathiriwa zaidi na janga hili ni South Afrika, pia masoko ya mitaji baadhi ya nchi yaliyumba pamoja na viwango vya kubadilishia fedha. Pia vitu kama misaada na mikopo naamini vilipungua.
 
Swadakta kabisa mkuu.
Sasa huo mdororo uliathiri vipi nchi za Afrika? Ukizingatia hatutumii sana bidhaa za marekani na sera yao ya makazi haikutugusa.
Kingine tuna lipi la kujifunza kutoka kwenye 2008 crisis na hii ya Silicon Valley Bank ukieleza at individual au social level itakua poa serikali ina washauri wake nadhani. Nawasilisha.
Kuhusu cha kujifunza, kutoka kwenye anguko la 2008 ni muhimu kwa taasisi za fedha kuzingatia uwezo wa wakopaji kulipa mikopo hiyo ili kupunguza kiwango cha mikopo chechefu, kwa mamlaka kuzingatia utaalam kuliko siasa na sera zinazowasha taa nyekundu.

Silicon Valley ni eneo maarufu nchini Marekani ambapo kampuni za kiteknolojia na ubunifu zimejikita huko, hii bank ilikuwa na wateja wa aina moja hivyo kudorola sekta ya teknolojia kukawazorotesha na wao lakini maamuzi yao yakawamaliza. Naamini 'Diversification' ni muhimu kuliko kujikita sehemu moja.
 
Ofisi yetu Tanzania ilifungwa just kwa simu tu na wateja kibao wakiwa wapo bado dirishani wanaendelea na huduma. Daaaah iliuma sana kwa kweli
Kwahiyo ikabidi msitishe huduma!!
 
Swali jingine ni kuhusu mortgage. Hapa bongo mortgage inafanyika kweli mkuu au haipo na soko lipo kweli
Ipo, mfano NHC walishawahi kujenga nyumba na kuzilink na mabenki. Unaenda benki unakopa mkopo wa nyumba ambayo huwa ni ya muda mrefu. NHC wanakupa nyumba wanalipwa na benki, wewe unamalizana na benki.
 
Tatizo lilianzia mwaka 2003, Rais wa wakati huo, George Bush alisain 'American dream' iliyojumuisha ndoto ya kila Mmarekani awe na nyumba. Masharti yalilegezwa na watu wengi walikopesheka, nyumba nyingi zikajengwa(Biashara ya makazi ililipa sana watu wakawekeza zaidi) na watu kununua kwa mkopo.

Mwaka 2007/08 watu wengi wakashindwa kuendelea kulipa hii mikopo kwa sababu ilitolewa kwa sera kuliko kupima uwezo wao wa kulipa. Kwa kawaida ukishindwa kulipa benki hurudi sokoni na kuuza ili kufidia deni. Wafilisi wakaenda sokoni kwa pamoja, nyumba zikawa nyingi sana sokoni na kawaida vitu vikizidi kuliko uhitaji huwa vinashuka bei, Marekani ikashuhudia anguko kali la bei kwenye sekta ya nyumba na bado zikawa haziuziki kwa urahisi.

Hii ikaleta 'panic' na soko la nyumba likafeli rasmi, kumbuka mzunguko mkubwa wa pesa umeshikiliwa na sekta ya makazi. Mabenki na 'hedge funds' vikaathirika pakubwa. Mwaka 2008 Lehman brothers akadondoka ikiwa ni anguko kubwa zaidi kwenye sekta ya fedha Marekani.

Nchi zilizoendelea mabenki ni muhimu sana kwenye uchumi, kuyumba kwao kukapelekea sekta nyingi kukwama. Watu wakaacha kufanya manunuzi wakilinda walichonacho na wengine wakashindwa kukopa ili kufanya manunuzi. Uzalishaji ukapungua na ajira zikapotea. Mzunguko wa mchakato huu ukapelekea mdororo wa uchumi ukiwa mkubwa zaidi baada ya mdororo uliosababishwa na vita kuu ya pili ya dunia.

Imani yangu umepata mwanga kilichotokea.
Asante sana mkuu.
 
Matatizo ya sasa ya benki yanatokana na Trump kulegeza masharti ya benki za kati na ndogo mwaka 2018.
 
Tafsiri ya inside job, kwa nini bank kubwa hazikuathirika?
Movies kama vile LA big shot, inside job zinajaribu kuelezea kwa hint kilichotokea
Mabenki yaliona fursa,yakaichangamkia,na serikali haiwezi kubali benki kubwa zife,pakaww na bailout
 
Siwezi kwenda deep, Ila niliiona documentary aljazeera ndiyo nikapata picha, walifungwa dagaa, mapapa yakabaki yakafungua biashara mpya, itafute hiyo documentary
Na nadhani thamani ya nyumba pia ilianguka kutokana na supply ya nyumba kuzidi demand kiasi kwamba wamiliki wakawa wanashindwa lipa mikopo na kuziuza haziuziki
 
Ipo, mfano NHC walishawahi kujenga nyumba na kuzilink na mabenki. Unaenda benki unakopa mkopo wa nyumba ambayo huwa ni ya muda mrefu. NHC wanakupa nyumba wanalipwa na benki, wewe unamalizana na benki.
It seems Una idea nzuri na banking sector,uko sahihi kabisa naongezea bank ikipata deposit nyingi,kiasi kikubwa kinaingizwa kwenye short term securities ambayo sometimes ina hasara Bora long term maturity securities
 
Mliosoma uchumi msikae kimya
Tatizo lilianzia mwaka 2003, Rais wa wakati huo, George Bush alisain 'American dream' iliyojumuisha ndoto ya kila Mmarekani awe na nyumba. Masharti yalilegezwa na watu wengi walikopesheka, nyumba nyingi zikajengwa(Biashara ya makazi ililipa sana watu wakawekeza zaidi) na watu kununua kwa mkopo.

Mwaka 2007/08 watu wengi wakashindwa kuendelea kulipa hii mikopo kwa sababu ilitolewa kwa sera kuliko kupima uwezo wao wa kulipa. Kwa kawaida ukishindwa kulipa benki hurudi sokoni na kuuza ili kufidia deni. Wafilisi wakaenda sokoni kwa pamoja, nyumba zikawa nyingi sana sokoni na kawaida vitu vikizidi kuliko uhitaji huwa vinashuka bei, Marekani ikashuhudia anguko kali la bei kwenye sekta ya nyumba na bado zikawa haziuziki kwa urahisi.

Hii ikaleta 'panic' na soko la nyumba likafeli rasmi, kumbuka mzunguko mkubwa wa pesa umeshikiliwa na sekta ya makazi. Mabenki na 'hedge funds' vikaathirika pakubwa. Mwaka 2008 Lehman brothers akadondoka ikiwa ni anguko kubwa zaidi kwenye sekta ya fedha Marekani.

Nchi zilizoendelea mabenki ni muhimu sana kwenye uchumi, kuyumba kwao kukapelekea sekta nyingi kukwama. Watu wakaacha kufanya manunuzi wakilinda walichonacho na wengine wakashindwa kukopa ili kufanya manunuzi. Uzalishaji ukapungua na ajira zikapotea. Mzunguko wa mchakato huu ukapelekea mdororo wa uchumi ukiwa mkubwa zaidi baada ya mdororo uliosababishwa na vita kuu ya pili ya dunia.

Imani yangu umepata mwanga kilichotokea.
Chagua mwenyewe hennesy au jack daniel tajiri ni mm, uliitumia ada ya baba yako vizuri✍🤝🏻🙏

Wote mliosoma uchumi hii mada ni yenu
 
Back
Top Bottom