Replica
JF-Expert Member
- Aug 28, 2017
- 1,664
- 8,799
Silicon Valley Bank inayosifika kuwa muhimu kwa kampuni za kiteknolojia hasa zinazoanza na kukua imedondokea pua na kuwa benki ya pili kubwa nchini Marekani kudondoka tangu kumaliza kwa mdororo wa uchumi wa mwaka 2008.
Mdororo wa 2008 ulianzia nchini Marekani baada ya mabenki mengi kuporomoka kutokana na kuporomoka soko la nyumba ambazo sehemu kubwa zilitokana na mikopo ya mabenki iliyopelekea sheria kali kutungwa kudhibiti sekta ya fedha Marekani. Anguko hili linahisiwa kutengeneza sheria nyingine.
Nini kimetokea
Mwaka 2022 benki ilianza kupata hasara baada ya ukuaji wa 250% miaka mitatu nyuma. Sekta ya teknolojia ilipungua kasi ilhali sehemu kubwa ya madeni ya benki hiyo yalikuwa kwenye sekta hiyo ya teknolojia.
Menejiment ya Bank ikaamua kuuza hati fungani zenye thamani ya dola bilioni 21 kwa hasara ya dola bilioni 1.8 na kuibua maswali kuhusu uwezo wake na ufanisi wake. Labda walilenga kuwahakikishia wawekezaji kwamba wana mtaji imara lakini hali hiyo ilipokelewa tofauti.
Watu na makampuni wakaanza kutoa fedha zao kwenye benki na ndani ya saa 48 benki ikapata upungufu wa mtaji kuweza kujiendesha kulingana na sheria za Marekani. Ijumaa asubuhi wateja walitoa maombi ya kutoa dola bilioni 42(Zingatia bajeti ya Tanzania ya 22/23 ni dola bilioni 18) na benki ikashindwa kukidhi maombi hayo.
Punde wathibiti wa Califonia walifika kwenye benki hiyo na kuifunga huku ikiwekwa chini ya uangalizi wa FDIC ikimaanisha benki hiyo iko mbioni kufilisiwa ili kuwalipa wateja wake.
=====
UPDATES - March 13
SERIKALI YAWAHAKIKISHIA WATEJA PESA ZIKO SALAMA
Serikali ya Marekani imesema wateja wa Benki iliyofungwa ya Silicon Valley wataweza kuzifikia pesa zao zote kuanzia leo Jumatatu, ikisisitiza haitatumia pesa za walipa kodi kuinusuru kama ilivyokuwa mdororo wa 2008. Serikali imesema inachukua maamuzi ya haraka na yenye ufanisi kulinda uchumi wa Marekani kwa kuongeza uaminifu wa umma kwenye mfumo wa kibenki.
Mfumo wa kibenki wa Marekani unabaki imara kwenye msingi imara sehemu kubwa kwasababu ya mageuzi makubwa baada ya mdororo wa kiuchumi wa 2008 ambapo taratibu zilianzishwa kulinda sekta ya mabenki.
Masaa machache kabla ya taarifa hiyo, waziri wa fedha wa Marekani, Janet Yellen alisema hawatafanya 'bailout' kwa benki hiyo. Baada ya kuanguka kwa Lehman Brothers mwaka 2008 wadhibiti waliyataka mabenki kuwa na mtaji wa ziada kukabiliana na matatizo pindi yakitokea.