Kitu kimoja nahisi bado hujanifungua (hujaweka wazi), hizi hisa zinazalishwa vipi, nikimaanisha kampuni inazitoa au inazianzishaje hizi hisa hadi kufikia kipindi ikafikia kuziuza sokoni?
""Mfano- Kampuni yaweza kuwa na hisa 1000, ikaamua kuuza hisa 500 na hisa 500 zikabaki akiba."" kama utaipitia hii mada pale mwanzo kuna maneno haya, ndio maana sikuelewa. Kwani alisema hisa ni umili, sasa inakuwaje hiyo kampuni kwa mfano ikawa na hisa 1000 za kwake? Kwa sababu mimi nikinunua hisa 10 toka kampuni "xc", nitakuwa na hisa 10 toka kwenye hiyo kampuni. Na nikiwa na kamupuni yangu "zm" yenye hisa 10 zitajulikana ni hisa 10 toka kampuni "zm" na si zile 10 za kutoka kampuni "xc". Nadhani sasa nimejitahidi kadri ya uwezo wangu nilivyoielewa mada hii, swali langu ni kwamba mmiliki wa kampuni "zm" alizipataje hizo hisa 10 tofauti na zile alizozinunua toka kampuni "xc"?Kwa hili swali naomba nikuhakikishie kuwa hujaelewa mada nzima
Ni hatuazip na vigezo ktk kusajili kampuni kwenye dse1. Hisa ni nini?
Wengi miongoni mwetu wamekuwa wakitaka kujua HISA ni nini, shauku hii imenifanya nidodose kidogo juu ya hisa kwa faida ya wengi. Kwa tafsiri lahisi HISA NI UMILIKI.
Mtu akisema nina hisa NMB anamaanisha ana miliki NMB. Umiliki huu unajionyesha wazi na bayana wakati wa kufanya maamuzi na kugawana gawio (faida inayopatikana katika kampuni). Mwenye hisa nyingi huwa na sauti au ushawishi mkubwa katika kufanya maamuzi na hupewa gawio kubwa kwa uwiano wa hisa zake.
Mfano- Kampuni yaweza kuwa na hisa 1000, ikaamua kuuza hisa 500 na hisa 500 zikabaki akiba. Wale watakaonunua hizo hisa 500 , wanakuwa wametoa mtaji kwa kampuni na kwa maana hiyo ndio wamiliki. Mwenye kuweza kununua hisa 251 atakuwa amenunua hisa nyingi zaidi kuliko yeyote na anakuwa na nguvu ya maamuzi katika vikao na gawio atapata kubwa kwa sababu ndie aliechangia mtaji mkubwa.
Faida za kuwa na hisa:
1. Unapata fursa ya kuwa mmoja ya wajumbe wa bodi ya wakurugenzi ama moja kwa moja au kwa kuwakilishwa.
2. Mwanahisa anapofariki shughuli za kampuni haziwezi kuyumba kwa sababu jukumu la kazi za kila siku lipo mikononi mwa menejimenti
3. Ni lahisi zaidi kuuza HISA pindi unapoona hauhitaji kuendelea na umiliki
4. HISA ni dhamana (badala ya kuweka nyumba/shamba ili uweze kukopeshwa na taasisi za fedha waweza kuweka dhamana ya hisa zako)
5. Kampuni inapofanya vizuri sokoni ama kwa kutoa huduma/bidhaa bora au kwa kuwa na mipango mkakati mizuri thamani ya HISA hupanda. Wapo walionunua hisa za NMB tshs 600 lakini leo ni zaidi ya tshs 950.
Kwa maana hiyo mbali ya gawio mtu anaweza kuuza hisa kwa bei inayomlipa akilinganisha na bei ya kununulia.
JINSI YA KUNUFAIKA NA SOKO LA HISA
1. Nimeona leo nishare na nyinyi kuhusu soko la hisa na jinsi ya kunufaika nalo.Kwa kifupi kuwa na hisa ni kumiliki sehemu ya kampuni au kuwa mmiliki wa kampuni hiyo kwa maana hiyo unakuwa na nafasi ya kushiriki kufanya maamuzi ,kupata faida au hasara katika kampuni hiyo.
Unanunuaje Hisa?
Hisa katika soko la hisa dare s salaam huuzwa na brokers kama orbit securities, na wengineo wapo wengi tu ila hawa ndio ninawafahamu. Unaweza pata taarifa zaidi kupitia website ya soko la hisa la dare s salaam www.dse.co.tz.
Faida za kununua hisa;
i) Hisa hukuwezesha kupata gawio la faida ya kampuni hiyo ikiwa itatangaza faida .
ii) Ukiwa na mwanahisa unaweza kutumia cheti cha hisa (share certificate) kuombea mkopo, ingawa hili ni jambo geni kwa Tanzania .
iii) Hukulinda dhidi ya anguko la thamani ya fedha kwa kuwa fedha huwa na tabia ya kupoteza thamani unaponunua hisa inaweza kukulinda kwa kuwa hisa huwa na tabia ya kupanda thamani kutokana na kuongezeka kwa bei ya hisa.
iv) Unaweza nunua na kuziuza wakati wowote.
Jinsi ya kununua hisa kwa kampuni unayohitaji;
Unapofika kwenye soko la hisa la dare s salaam kuna makampuni mengi yaliyoorodheshwa kuuza hisa zao mfano CRDB, NMB, USL, DCB, KCB, SWISS PORT, TBL, TTP na nyingine nyingi.
Sasa ni kampuni ipi ununue hisa ni vyema ukaangalia mambo yafuatayo;
i) Performance ya kampuni. Mfano kampuni kama inafanya kazi vizuri kwa weledi na inamategemeo ya ukuaji wa kampuni hiyo kama kutanua matawi, kuongeza product au kukua kwa biashara katika kampuni hiyo basi hiyo ni kampuni nzuri mfano.
Ukisikia kampuni imetanua soko lake kama CRDB ilivyofungua matawi nchi za nje inamaana ya kuwa faida ya kampuni hiyo itaongezeka na hivyo gawio linaweza kuwa kubwa na wewe kupata faida na pia bei ya hisa itaweza kuongezeka hivyo utapata faida pia pindi ukiamua uza hisa zako.
ii) Bei ya hisa na uimara wake (stable share price) kuna kampuni ambazo bei zao za hisa wakati wote ni nzuri kwa maana hazishuki sana au mara kwa mara na pia zina tabia za kuongezeka mfano TBL , SWISS PORT, TCC.
iii) Wakati wa kununua hisa . ni muhimu pia kuangalia ni wakati gani unanunua hisa mfano. Wakati ambao hisa ndio zinaingizwa au kuuzwa kwa mara ya kwanza kwenye soko la hisa bei huwa ni ndogo sana na baada ya hapo mara nyingi bei huongezeka ingawa kuna wakati hushuka pia .
Lakini bei ya hisa hupanda kushuka kutokana na nyakati katika mwaka mfano ifikapo mwishoni mwa mwaka na mwanzoni mwa mwaka bei hushuka na kuwa ndogo zaidi ila katikati ya mwaka bei huanza kupanda kwa kasi kubwa zaidi
iv) Uwepo wa taarifa nzuri katika Sekta iliyo kampuni hiyo au katika kampuni hiyo. Mfano imekuwa ikisikika kuwa benki ya CRDB itakuwa inatumika kulipia mishahara ya baadhi ya wafanyakazi wa serikali basi siku ukisikia imeingia mkataba huo au imeanza kutumika kulipia mishahara hiyo basi nenda kanunue hisa hizo haraka kwani bei ya hisa itaanza kupanda na pia gawio la faida litakuwa kubwa.
Mfano mwingine ni kwa kampuni ya SWISS PORT kampuni hii inadeal na mizigo kwenye viwanja vya ndege,nafikiri taarifa ya kutanuliwa kwa uwanja wa ndege ya Dare s salaam inafahamika hivyo ni wakati mzuri kununua hisa wakati huu kwani pindi uwanja utakapokamilika basi kampuni itakuwa na biashara kubwa bei ya hisa itaongezeka na faida pia
v) Wingi wa makampuni katika soko la hisa. Mfano kuna mabenki zaidi ya matano hii inamaana benki hizi zinagombea wateja hii ni kwa wateja wote wale wanaowahudumia na wale wa kwenye soko la hisa hivyo bidhaa zao zipo za kutosha na bei itakuwa ya kawaida mambo ya demand na supply. Kwa bei ya leo kampuni inayoongoza ni TCC- 17000, TBL 15000, JHL 10620, SWISS 6600,ACA-6540. Makampuni haya yote yanafanya shughuli tofauti na bei zake ni nzuri zaidi.
Ushauri kwa wanaotaka kununua hisa;
Kama unahela ya ambayo umeiweka tu mahali ukiwa na lengo la kufanya kitu baada ya mwaka au miezi kadhaa ijayo nenda soko la hisa kanunue hisa za SWISSPORT kwa jinsi bei inavyoongezeka kuna uwezekano mkubwa mwakani muda kama huu bei ya hisa yake moja itakuwa mara mbili zaidi ya bei ya sasa, kwa kifupi ukija kuuza hisa ulizonunua wakati huu basi mwakani zitakuwa mara mbili zaidi kudeclare interest mimi ni mwanahisa tu wa soko la hisa la Dar es salaam.
Nakaribisha na wataalamu wengine waweze kuchangia kuboresha zaidi.
1. Je kama kampuni ikipata hasara na mimi napata hasara?
na kwa mfano nikitaka kujua faida nafanyaje?
Sure mkuu Co. Ikipata hasara na wewe unapata hasara, shareholders ikitokea Co. Imefilisika wao hua wa mwisho kulipwa kwenye kile kinachobakia baada ya wengine kua wamelipwa!!
Jinsi ya kujua faida kuna namna mbili kupitia dividend/gawiwo na capital gain sijui kiswahili tunaiitaje! Faida kupitia gawiwo unalipata pale kwa mfano unamiliki hisa 5000 then Co. Ikatangaza kwenye kila hisa 1 utapata gawiwo la sh.100 then hapo utapata faida ya(5000×100)= sh.500,000# mkuu na Capital gain ni pale kwa mfano ulinunua kila hisa 1 kwa sh.500 na unahisa 5000 then ulitumia(500×5000)= sh.2,500,000 kama mtaji wako so ikitokea leo ukauza hisa zako na kila hisa ukauza kwa sh.1000 manake itakua ni 1000×5000(idadI ya hisa unazomiliki)=5,000,000 then faida yako hapo ni ile pesa uliyopata kipind umeuza hisa zako 5,000,000 kutoa pesa ulizonunulia hisa zako 2,500,000=2,500 000 pole kwa maelezo marefu mkuu wangu!!
HASARA ZA HISA
1. Hasara ni pale unapokuwa na hisa chache kwani unakuwa kama unasindikiza wengine. Gawio unapata dogo na unakuwa huna ushawishi katika maamuzi. Hasara nyingine ni pale kampuni inapofanya vibaya, thamani ya hisa hupungua, waweza nunua hisa 1 kwa tsh 1000 ukauza 500 au hela zako zikazama. Ni vyema kupata ushauri wa kitaalamu kabla ya kununua HISA
2. Ni kwa nini HISA za CRDB zilishuka thamani?
Nitachangia kidogo...
Kwanza kabisa,ningependa pia kusema kuwa hisa, zikiwa kama sehemu ya umiliki wa kampuni, soko lake ni kama la bidhaa nyingine yeyote..mtu atakubaliana na mimi kuwa kuna sababu zaidi ya moja inayoweza kupelekea kupanda au kushuka kwa bei ya bidhaa fulani sokoni wakati fulani.
Inaweza kuwa ni sababu ya kupungua/kufurika kwa bidhaa husika sokoni, kuwepo kwa bidhaa shindani bora zaidi, hisia ya wateja kuhusu kukosekana kwa bidhaa hiyo hapo baadaye na hivyo kutaka kununua kiasi kikubwa leo na kadhalika....
Primarily,ni kwamba bei ya hisa sokoni inakuwa determined solely na demand vs supply ya hisa at a time ni kweli kabisa. Lakini je, ni nini kinachopelekea mtu kutaka kuuza au kununua hizo hisa na hivyo kuathiri kiasi hicho cha demand/supply ya hisa sokoni at a time? Sababu ni nyingi..mfano:
1) Current company profits - Kuna watu wanaodhani kuwa kampuni ikipata faida kubwa mwaka huu kuliko uliopita basi itakuwa inafanya vizuri na hivyo wanaamua kuwa sehemu ya wamiliki na hivyo kutaka kununua hisa zake. Hata hivyo faida ya sasa ya kampuni inaweza isiwe kipimo tosha cha uzuri au ubaya wa kampuni.
Mfano, kwenye hii case ya CRDB, inawezekana faida yake kubwa imetokana na vyanzo visivyoweza kujirudia mwakani (one - off transactions) kama kuuzwa kwa baadhi ya assets zake n.k..mwekezaji anapoona kuwa kampuni imeshindwa kutengeneza faida kwenye ile biashara yake kuu, basi ataona kuwa uwezo wa kampuni kutengeneza faida utakuwa mdogo pia huko miaka ya mbele na hivyo kutaka kuuza hisa zake.
2) Company prospects/Investment plans (Mipango endelevu) - Kampuni inaweza kutengeneza faida nzuri leo, lakini kwa kulinganisha mipango mikakati yake ya muda mrefu, faida yake haitaongezeka kwa kasi kama ile ya washindani wake wa karibu. Kwa matarajio ya kupata faida zaidi baadaye, mwekezaji anaweza kuamua kuuza hisa zake na kununua za kampuni nyingine yenye mipango yenye faida zaidi huko mbeleni.
3) Decline in company's market share - Wawekezaji siku zote hutaka kuweka pesa zao pale ambapo wanahisi zitakuwa na faida kubwa zaidi. Kampuni inaweza kuwa imepata faida leo, lakini ukubwa/umahiri wake kwenye soko lake la bidhaa ukawa unapungua taratibu. Hivyo wawekezaji wataona uwezekano wa kutengeneza faida zaidi ikiwa watawekeza kwenye hiyo kampuni nyingine inayoonyesha ukuaji wa soko lake la bidhaa ingawa hapa walipowekeza sasa kumepatikana faida pia.
4) Temporary buyers/sellers - Masoko ya hisa duniani kote siku hizi yametawaliwa na watu wanaotaka kununua hisa na kukaa nazo kwa muda mfupi tu mpaka hapo bei itakapopanda kidogo ili wauze wapate faida, halafu wanunue nyingine na kuuza tena kwa mtindo huo huo. Hii inaweza kuwa kweli kwa case ya CRDB pia.
Kwamba hawa wawekezaji waliopeleka sokoni walikuwa wanasubiria kampuni itangaze gawio la faida kwa mwaka (dividends), wachukue faida yao halafu wauze hisa zao na kupeleka sehemu nyingine. Utashangaa kuwa kuna watu huwa wanawekeza ada za shule za watoto wao kwenye hisa na wakati wa kulipa ada ukifika inabidi tu wauze ili walipe ada..no matter what!
5) Wawekezaji kulipa mikopo - hii hutokea mara nyingi wakati kampuni nzuri ikiingiza hisa zake sokoni kwa mara ya kwanza. Wawekezaji huweza kuchukua mikopo benki, kununua hisa na kukaa nazo, na kuziuza pindi bei inapopanda sokoni (au wakati wowote muda wa kurejesha mikopo hiyo benki unapofika, bila kujali bei ya hisa sokoni wakati huo!)
6) Speculative buyers (wanunuzi watabiri) - Hawa ndio wameshamiri kwenye masoko ya hisa duniani kote, na ndio chanzo kikuu cha financial crisis iliyoikumba Marekani miaka ya juzi. Ni kwamba badala ya watu kununua hisa za kampuni kwa sababu ya uwezo wake wa uzalishaji wa sasa hivi, ununuzi wa hisa unakuwa umeegemea zaidi kwenye yatakayotokea kwenye kampuni miaka hata 20 au 100 ijayo.
Kunakuwa na watu wapiga debe, wanaochimba (au kupika) habari za mipango ya kampuni (au ya serikali, itakayoneemesha mapato ya kampuni) hata miaka 10 huko inayokuja. Kwa hivyo basi watu hawa kwa maneno yao wanaishia kusababisha bei ya hisa kuongezeka ama kupungua...
kwa hivyo kwa kujibu swali lako dada Ashadii, kutokana na kuwepo hasa hasa kwa wanunuzi/wauzaji wa hisa wa category namba sita (6) hapo juu, mara nyingi bei ya hisa sokoni haiendani moja kwa moja na ubora wa kampuni kwenye kuzalisha fedha kwa sasa.
Kifupi kuna mambo meengi tu yanayoweza kufanya prospective investors wakaongeza ama kupunguza imani yao kwa kampuni fulani. Ndiyo maana unaweza kuona wakati mtu kama Steve Jobs alipokuwa anakaribia kujiuzulu kama Apple CEO ilibidi kufanyike marketing campaign ya kutosha ku-restore investor confidence na kuwadhihirishia watu kuwa kampuni itaendelea kuwa kwenye mikono salama, itaendelea kupata faida, na hivyo watu hawana haja ya kuuza hisa zao kwa hofu ya kupata hasara huko mbeleni.
In a nutshell, the best way to buy or sell shares is to just act like a smart layman, huhitaji technicalities nyiingi kuhusu sijui faida ama hasara ya kampuni leo, earnings per share, etc...angalia mifano ya maswali anayotakiwa kujiuliza layman hapa:
(a) Twiga/Simba Cement zinazalisha cement? Je cement itaendelea kuwa bidhaa inayohitajika na watu wengi? Je demand yake ni kubwa? Je bidhaa za kampuni zina ushindani mkubwa sokoni? Je kampuni ina uongozi mzuri? kama majibu ni ndiyo badi nunua hisa..lakini mwaka 2014 ukishasikia Dangote Cement imeanza kuzalisha cement kule mtwara kwa kiwango kinachotosheleza demand ya Afrika Mashariki yote,,,you should know it is a sign that Twiga's share of the cement market is about to decline and..may be, may be you need to sell your shares!
(b) Hisa za Precision Air...ilikuwa ni sahihi kabisa kwa watu kununua hisa za Precision Air wakati ambapo kampuni ilikuwa inaoperate kama monopoly, bila mshindani. Hii ni kwa sababu lazima kampuni ingetengeneza pesa tu, iwe isiwe (walau ikiwa na uongozi makini kidogo).
Lakini je, baada ya kuja kwa fast jet, Precision ina uwezo wa kuendelea kutengeneza pesa? Je ina uwezo/mipango gani ya kupambana na hii bei ndogo ya mshindani wake ilhali wote tunajua wateja wanavyopenda kulipa gharama ndogo kuliko kubwa?..haya ni maamuzi ambayo yanaweza kufanywa na a smart layman...trust me,hayo ni muhimu kuliko expert advice...
Na vigezo gani vinazingatiwa ili kampuni iweze kuuza hisaNi hatuazip na vigezo ktk kusajili kampuni kwenye dse
idadi ya hisa ktk kampuni inapatikanaje?Na vigezo gani vinazingatiwa ili kampuni iweze kuuza hisa