MINOCYCLINE
JF-Expert Member
- Apr 2, 2015
- 8,018
- 16,801
ANGALIZO
Nitakayoyaandika (Kuyaeleza) hapa ni Maoni na Mtizamo wangu Mimi All - Rounder na sikulazimishi uukubali bali uheshimu tu tafadhali.
PONGEZI
Nisiwe mchoyo wa Pongezi kwa Mafanikio haya makubwa ambayo kwa sasa Klabu ya Simba imeyafikia ikiwemo Ushindi wake wa jana wa Magoli 3 kwa 0 na pia kuwa na Clean Sheet ya Kutokuruhusu hata Goli 1 katika Michezo yake Minne ya Ligi ya Mabingwa Afrika (CL)
Pia nitoe pongezi zangu nyingi sana kwa Serikali ya Tanzania (kupitia Wizara husika ), Uongozi mzima wa Klabu ya Simba kuanzia Mwekezaji Mohammed Dewji, CEO Barbara Gonzalez, Mwenyekiti wa Klabu Murtaza Mangungu, Msemaji wa Simba Haji Manara na Wanachama, Wapenzi pamoja na Mashabiki wote wa Simba SC na Wachezaji wote wa Simba SC kwa Ushirikiano wao mkubwa ambao umezalisha Mafanikio haya ambayo hayaipaishi tu Tanzania pekee bali hata Afrika ya Mashariki nzima imewakilishwa vyema na Simba SC.
MAPUNGUFU YA KIMSINGI YA KIKOSI
Pamoja na kwamba Simba SC imepata (imefikia) Mafanikio haya ila nisiwe Mnafiki na wala tusifichane kuambiana Ukweli kuwa bado Klabu ( Kiuchezaji na Kiufundi ) ina matatizo ya Kimsingi ambayo kama yasipofanyiwa Kazi haraka kuna Uwezekano Mechi yetu dhidi ya AS Vita Club ambayo Kwangu Mimi itakuwa a Decisive Game basi tukafungwa na Ndoto yetu ya Kutinga Nusu Fainali ikaishia kwa kutokufuzu hata Robo Fainali yenyewe.
Bado Mabeki wa Simba SC wameendelea na tatizo lao lile lile la kupoteza Umakini katika Kukaba, Kujisahau, Kutegeana huku Mabeki wa Kati Wakijichanganya na wa pembeni kupenda kupanda Kushambulia na Kuchelewa kurejea kwa haraka.
Sina shida sana katika eneo la Kiungo kwani wanajitahidi kutekeleza vyema Majukumu yao na huenda hata Mafanikio haya ya Timu Kutokufungwa hadi sasa yamechagizwa na Idara hii Muhimu kwakuwa Mipango yote ya Wapinzani huwa inaharibiwa Kiustadi na Ushirikiano mkubwa wa Viungo wa Kimkakati akina Thadeo Lwanga na Muzamiru Yasin huku akina Miquissone na Chama au Larry Bwalya na Bernard Morrison wakichagiza katika Kuwachanganya Maadui hadi Kuwadhoofisha.
Washambuliaji wa Simba SC hasa Kinara wao wa sasa Chris ' Kopa ' Mugalu, Meddie Kagere na John Boko wanajitahidi mno na tunawapongeza kwa hili ila wana Makosa ya Kiufundi sana ambayo kuna muda yanasababisha hata wawe wanakosa Kizembe zaidi Magoli au kusababisha Timu ishinde kwa taabu au kwa Magoli machache.
CLATOUS CHAMA NI KIKWAZO AONYWE
Wiki kadhaa hapa hapa JamiiForums na katika Jukwaa hili hili niliwahi Kuandika Mada ya Kumsema na Kumkosoa Clatous Chota Chama kuwa anatuchelewesha mno Ushindi kwa Kuremba sana Mipira nikaeleweka namchukia ila nashukuru sasa kuwa Observation yangu kumuhusu imeanza Kueleweka na sasa Sote tunaimba nyimbo moja ya Kukereka ( Kukerwa ) nae.
Naendelea Kusisitiza kuwa Clatous Chota Chama ni Mchezaji very Talented, Intelligent ( Football Genius ) na Playmaker hasa ila ana tatizo moja Kubwa la kutokujua wapi arembe ili kuwapotezea muda Wapinzani ( Timu ikiwa inaongoza ) au wapi anatakiwa achangamke kwa kutoa ( kuachia ) Pasi kwa haraka kwa Wenzake wakiwa katika Striking Momentum ili Timu ishinde.
Kwa aina ya Uchezaji wa Clatous Chota Chama Mimi All - Rounder ningekuwa ni Kocha ningekuwa namchezesha pale tu Timu ikiwa imeshashinda ili kuwapotezea muda Wapinzani au katika zile Mechi nyepesi ambazo najua Simba SC itashinda tu hata kama Ushindi utachelewa ila katika zile Tough Games kamwe sitoweza Kumuanzisha au hata Kumpanga kwani ameshaonyesha kuwa akikutana na Timu inayocheza Mpira wa Nguvu ( Kazi Kazi ) huku Wachezaji wake wakiwa wanafika ( wanagongana ) huwa hafui dafu na Mpira unamshinda.
Benchi la Ufundi ama limuonye au limrekebishe abadilike japo nimeanza kuona ni kama vile Clatous Chota Chama ama anaogopwa au Ufalme wake ndani ya Kikosi unamfanya kuwa ni Untouchable na above the whole Team hivyo na Yeye pia kujawa na Kiburi, Jeuri na hata Dharau kwakuwa anajua hakuna wa kumwambia Kitu kwani ameshaziteka Akili za wanasimba wote.
UKWELI MCHUNGU KUHUSU AS VITA CLUB
Hapa wala tusidanganyane kwa tunaojua Mpira au hata tu Kucheza na kuwa Wafuatiliaji wazuri wa Mipira tutakubaliana kuwa hakuna Mechi ambayo Simba SC itapata Usumbufu, Shida na Taabu kama hii itakayocheza na AS Vita Club tarehe 2 April, 2021.
Kwa Mtu aliyewatizama walipocheza Mechi zao na Al Ahly na hata ile ya dhidi ya Simba SC kwao Congo DR atakubaliana nami kuwa hawa Jamaa wapo vizuri tena katika kila Idara na wanaupiga mwingi mno huku Silaha yao Kubwa ni Kucheza Kitimu zaidi tofauti na Simba SC ambayo muda mwingi wanacheza Kibinafsi zaidi.
Kwa Mapungufu ya Kimsingi ya Simba SC ambayo nimeyaelezea vyema tu hapo juu kama hawa AS Vita Club wakija Dar es Salaam ( kwa Mkapa ) na Kucheza Mpira wao ninaoubatiza ' Pira Nguvu, Pira Mbio, Pira Ufundi na Pira Pumzi nyingi ' kuna Uwezekano Simba SC ikafungwa ( japo siombei ) goli zaidi hata ya Moja. Tuwe Makini nao sana tafadhali.
NINI KIFANYIKE?
Kuanzia sasa (leo) Simba SC hasa Benchi la Ufundi liweke Mkakati mzito wa namna ya Kukabiliana na AS Vita Club ambao Mimi All - Rounder nawaogopa hata kuliko Al Ahly.
Mapungufu yote niliyoyaainisha hapa katika huu Uzi wangu yafanyiwe Kazi na Wachezaji wa Simba SC ikiwezekana katika hiyo ( hii ) Mechi wajitoe Maradufu kwa Kupambana Uwanjani ( wakiweza hata Kufia Uwanjani ) ili tushinde au ikishindikana basi tutoke nao Sare (Suluhu ) tu ambayo itatuvusha kwenda Robo Fainali.
SAIKOLOJIA
Nashauri kuelekea Mechi hii Muhimu na ya Kimaamuzi kwa Simba SC basi apatikane haraka Mtu wa Saikolojia ili aweze Kuwajenga vyema Kiakili Wachezaji wetu kuelekea Mechi yao na AS Vita Club.
Kiufundi Saikolojia nayo ina nafasi kubwa sana katika Mafanikio ya Timu hivyo hili lisipuuzwe na lizingatiwe kwa Umakini mkubwa sana. Wachezaji wa Kiafrika ( hasa ) wa Kitanzania tunawajua wenyewe katika nyakati kama hizi hivyo Saikolojia ni Muhimu Kwao.
HITIMISHO
Mpaka hapa ilipofika sina Shaka na Simba SC na najua itafanya vyema tu ila kupeana Ushauri na Tahadhari si Jambo baya kama sehemu ya Uanamichezo na Upendo kwa Timu husika.
Uongozi endeleeni kutoa Motisha zenu ( Pesa ) kwani hii nayo nina uhakika imechangia Mafanikio haya ya Simba SC kwani Wachezaji wana uhakika mkubwa wa Ustawi wao wa Kiuchumi.
Mwenyezi Mungu aipiganie Simba SC, aibariki zaidi na ifanikiwe kushinda Mechi yake hii Muhimu dhidi ya As Vita Club ili itinge Robo Fainali na tujipange zaidi kuelekea katika Lengo Mama letu la kufika Nusu Fainali kwa Msimu huu.
OMBI
Naomba Uzi huu kwa aliye karibu na Uongozi wa Simba SC au Benchi la Ufundi au Bodi ya Simba SC au Haji Manara awafowadie ili na Wao wauone na wausome nikiamini kuna mema na mazuri tu ya Kiushauri watayapata hapa.
Na wale ambao huwa mnapenda Kuchukua Mada hapa JF na Kuzichapisha ( Kuziweka ) katika Magazeti yenu au Mitandao yenu mbalimbali ( siyo JamiiForums ) tafadhali mkipenda Kutumia hili Bandiko langu kuweni Waungwana kwa kunipa Credit ( Acknowledging ) na pia Kuutaja huu Mtandao wa JamiiForums kuwa ndipo umetoa Uchambuzi huu.
Inakatisha tamaa pale Mtu anapotumia muda wake mwingi, Akili zake za Kiuchambuzi na Kimtizamo pamoja na Maarifa kisha unaikuta Taarifa ( Habari ) yako imechapishwa ( inatumika ) Kwingineko na wakisema ni yao. Ni matumaini yangu makubwa hili litazingatiwa kama ambavyo All - Rounder nimeshauri na kulitahadharisha pia. Sikatai Kutumika ila Credit from the Source ifanyike tafadhali.
Kila Ia Kheri
Wenu All - Rounder ( alias ) Brainiac