JF's impact on Tanzanian Politicts

Ukitaka kujua utamu wa jf utaona members wanatishia kujitoa na wengine wanalalamika lakini hawajitoi uanachama! JF inapendwa si mchezo, wanaodai imekosa mwelekeo hawaachi kila siku kuchungulia humu! Hongereni sana waanzilishi wa JF!

Kwa makisio yako JF inawafikia watanzania wa aina gani? Unadhani umetoa mchango wowote katika ongezeko la kura na viti vya upinzani katika Uchaguzi wa mwaka huu?
 
yote haya ni kweli na ni majeraha ya kushindwa , lakini hasira hizi zitaisha very soon..give it time..ni haki delayed n denied..

Nimependa tathmini yako mama, kwamba hata wenye hasira na JF hawaachi kuendelea kushiriki. Hebu jaribu kutueleza zaidi sababu gani una hasira kiasi hicho lakini unatembelea Hapa kila siku?
 
JF itawezaje kuwafikia watu wa vijijini, ambao kulingana na matokeo ya uchaguzi uliopita wengi bado hawajazinduka?
 
Naafiki kabisa observation yako, kinachokera kuliko vyote ni mods. Pengine tushawishi wabadilishwe? Sasa usishangae baada ya kusema hivi hii thread ikapotea kiaina!

Kinachoifanya JF iwe unique ni MODS, tatizo ni kwamba maelfu ya watanzania wana-access JF, kati yao kuna mami ambao ni wapuuzi kweli ukisoma hata wanachoandika huwezi kuelewa malengo yao nini. Hao ndio wanaharibu credibility ya JF. So can be we blame mods on that? should we get rid of mods to allow few nimwits to ruin the whole forum. Of course not.

In my opinion if we use JF as a platform for exchanging ideas, enlighting ourselves and as forum for educating one another on matters relating ot our country, JF can be better than it is. If we let these nimwits take charger na kuanza kuleta uchadema, uccm, ukabila, udini, uswahili na kuweka utanzania mwishoni, JF itapoteza kabisa maana yake. Kwa mano yangu JF inahitaji Mods zaidi waliomakini zaidi. Kuna threads na posts ambazo hazitakiwi kabisa kuonekana.
 
Kinachoifanya JF iwe unique ni MODS, tatizo ni kwamba maelfu ya watanzania wana-access JF, kati yao kuna mami ambao ni wapuuzi kweli ukisoma hata wanachoandika huwezi kuelewa malengo yao nini. Hao ndio wanaharibu credibility ya JF. So can be we blame mods on that? should we get rid of mods to allow few nimwits to ruin the whole forum. Of course not.

In my opinion if we use JF as a platform for exchanging ideas, enlighting ourselves and as forum for educating one another on matters relating ot our country, JF can be better than it is. If we let these nimwits take charger na kuanza kuleta uchadema, uccm, ukabila, udini, uswahili na kuweka utanzania mwishoni, JF itapoteza kabisa maana yake. Kwa mano yangu JF inahitaji Mods zaidi waliomakini zaidi. Kuna threads na posts ambazo hazitakiwi kabisa kuonekana.

Gurudumu, shukrani kwa kuanzisha hii post; kusema ukweli, tathmini inahitajika ili JF kama chombo cha habari na jukwaa la mijadala kijue kinapoelekea.

Bongolander, yaani umeakisi mawazo yangu. Niliandika makala fupi kuhusu matumizi ya vyombo na vyanzo vya habari kwenye mchakato wa Uchaguzi Mkuu (makala inapatikana hapa: Uchaguzi 2010: Vyombo na vyanzo vya habari). Sehemu ya hiyo makala ni kama ifuatavyo*:

Chanzo cha matokeo na taarifa za matukio

Sijui kama ilikuwa ni busara au la kusitisha zoezi la utangazwaji wa kura za Urais kutoka kwenye kata mbalimbali. Ila nina uhakika unapata picha tete kama matokeo ya awali yangetofautiana kabisa na yale ya Tume ya Uchaguzi.

Bahati mbaya au nzuri, wote tukaishia kwenda Jamii Forums ili kupata taarifa za matokeo na matukio mbalimbali haraka zaidi. Bahati mbaya, mambo yalikuwa kishabiki zaidi na nilisikitishwa na kitendo cha viongozi kuacha watu waandike chochote kile wanachotaka; kiwe na lugha za kukashifu, kusifia, kukosoa, kuelemishana au hata kutoa taarifa tu.

Labda unaweza ukanipinga kwa kusema hiyo ndio ‘demokrasia' ya kweli, kila mtu ana uhuru wa kutoa maoni na mawazo yake.

Kumbuka, hivi vyombo vya habari vinakuja na dhamana, hasa pale watu wengi wanapovitegemea kupata taarifa nyeti. Visipotumiwa ipasavyo ndio hapo tunashuhudia majukwaa muhimu yakigeuzwa kuwa vyombo vya propaganda; na kushindwa kutupa picha halisi.

Lakini kulikuwa na watu wachache ambao hawakuchoka kuulizia "data" au "namba" kila mtu alipoleta taarifa. Jiulize, hao ni sehemu gani ya jamii yetu? Watu wangapi hupenda kuhakiki taarifa au habari fulani?

Mwishowe, kwasababu wengi wetu hatuwezi kufikiri wenyewe na kuuliza maswali ya msingi, tunaishia kwenda kwenye vyombo ambavyo vinaakisi mawazo yetu tu. Hatupendi kusikia mawazo mbadala ambayo hayatufurahishi. Yaani, kwa maneno mengine, tunapenda kwenda sehemu ambazo zina watu wenye mawazo kama yetu tu.

Hebu fikiria, tuwe na majukwaa mawili ambayo yana wachangiaji wenye fikra na mawazo (namaanisha porojo) yanayokinzana kabisa. Kila kundi litaamini wanachojadili kila siku kwa dhati. Itakuwaje hawa watu wa makundi husika wakikutanishwa mitaani?

Naamini Uchaguzi wa mwaka 2015 utakuwa una mwamko zaidi. Na kama hatutarekebisha kasoro zilizojitokeza - hususan jinsi ya kuripoti - basi tutaishia pabaya.

... Na hata watu Tanzania walikuwa wanajadili mambo kama hayo. Kwamba, ili uweze kuelewa vizuri kinachoendelea, ulikuwa hauna budi kuwa na akili inayoweza kuchuja taarifa. Hapa naongelea:

1. Hata kama unatumia JF kupata taarifa, basi uwe na uwezo wa kutafuta maoni ya hao wachache ambao wanaonekana wako "critical".

2. Ukishazipata, tafuta taarifa zaidi ili kuhakiki ulichosoma pale.

Sasa, unadhani Watanzania wangapi wanaweza kufanya hivyo? Kumbuka, hii ni ishu nzito mno; taarifa fulani zinaweza zikazaa maandamano na ghasia, au hata kuchafua/kuharibu shughuli za mchakato mzima wa uchaguzi.

Wale watoto walioanzisha fujo Tandika unadhani ilikuwaje? Mpaka polisi wakaamua kuwaachia; kulikuwa na watoto wa mpaka darasa la pili. Walikuwa wanafanya nini pale?

Majimbo mangapi yalikuwa yanajadiliwa JF? Yanazidi 80? Kati ya 239.

Je, uliona taarifa zozote kuhusu vituo vya uchaguzi Kurasini ambapo wasimamizi walikuwa wanasinzia? Kwenda kuulizwa, kumbe wao walianza shughuli mapema na wapiga kura walikuwa wachache sana. Ilipofika saa saba mchana wakaamua kupumzika tu.

Habari kama hiyo inaweza kutafsiriwa tofauti na majukwaa tofauti. Nina uhakika unaweza ukaotea jukwaa gani litasema nini.

Pia, wangapi wanaelewa kuwa JF ni jukwaa la mjadala tu? Wakati mule kulikuwa na watu ambao walikuwa kwenye vituo kadhaa wakilinda kura. Huyu mtu aliyekuwa kwenye kituo cha kupiga kura si ni chanzo cha taarifa? Au ni chanzo cha mjadala tu?

Ukiwa na blog au chanzo cha taarifa kinachotembelewa na watu 10 – 100, sawa. Lakini ukiwa unatembelewa na watu 10,000 kwa wakati mmoja, ujue tayari una dhamana...

*Nisameheni, niko mzigoni na siwezi kuandika upya kwa kirefu...
 
Gurudumu, shukrani kwa kuanzisha hii post; kusema ukweli, tathmini inahitajika ili JF kama chombo cha habari na jukwaa la mijadala kijue kinapoelekea.

Nimefuatilia makala zako hizo ulizounganisha hapo juu. nadhani tuna mtazamo mmoja na ndiyo maana naamini inahitajika tathmini ya JF. pamoja na mapungufu uliyoorodhesha kwenye makala za VijanaFM, nadhani, na pamoja na upungufu mkubwa wa critical minds ndani ya JF kama ulivyoeleza, naamini lazima kuna mazuri mengi yaliyosababishwa na mijadala hapa JF hasa ukiitathmini kutokea mbali kabla ya kipindi cha kampeni.

ningefurahi kusoma tathmini yako ya JF kwa kipindi kabla ya kampeni na sasa baada ya kampeni kwani wakati wa kampeni umeshaandika kwa kina katika VijanaFM. Pia ningefurahi kusoma tathmini yako ya JF nje ya uchaguzi. kwa upana kuhusu sera na utawala bora.
 
kuna wanachadema humu! huwa wanakurupuka na sasa wanabagua watu kidini na kimaeneo! usipime kabisa, to aneno baya kuhusu chadema ndio utaona hiyo impact yake unayoisema,

JF ipo siku zote, impact yake imekuwa positive, ila kuna wachache wanaiharibu na kumwaga upupu humu ndani ambao ni aibu kabisa, though wanakuwa wamefikia maximum level ya kufikiri kwao,
Waberoya can't you contribute anything without mentioning Chadema or Zitto shame on you.
 
Haswaaa, Gurudumu.

Nadhani wengi tunaelewa jinsi JF ilivyokuwa kabla ya vuguvugu la uchaguzi kuanza. Palikuwa pametulia na mara nyingi mtu ulikuwa unaondoka na kitu kinachofanya ufikirie. Sisemi kuwa lazima kila jamii au kikundi cha watu kiwe na watu wengi ambao wana hoja na fikra zinazojitegemea. La hasha. Ila uwiano unatakiwa uwe sahihi; ushabiki ukizidi ndipo hapo mantiki na lengo la jukwaa kama hili hupotea.

Hii homa ya uchaguzi/siasa itapungua tu, na wale manguli wa JF, wenye misimamo yao binafsi kwenye siasa na maisha kwa ujumla, watarudi na kuacha maoni yao zaidi (kama ilivyokuwa awali) -- kwasababu mambo ambayo huanzisha "ushabiki" yatapungua. Hiyo haina mjadala (unless ishu nyingine kama za EPA zijitokeze kwenye hii miezi miwili ijayo... lakini na zile nazo zinahitaji kupembuliwa pia, na watu hawana budi kuuliza maswali ya maana).

Mi' hofu yangu ni vipindi vya uchaguzi kwasababu ni hulka ya wengi mno hisia kuchukua mkondo.

Kwa kumalizia tu, nia yangu ilikuwa ni kujadili matumizi ya vyombo na vyanzo vya habari kwa ujumla; na JF ina nafasi kubwa mno.. kuna wakati ulikuwa unapata "taarifa" hapa kabla hata ITV hawajairusha hewani! (Kuna makala nyingine inayomhusu Makame: http://vijana.fm/2010/11/23/uchaguzi-2010-2/.) Na kadri siku zinavyoenda tunajifunza kuwa wahariri na magazeti mengi yanafungamana na pande fulani-fulani, kuliko labda wengi tulivyokuwa tunafikiri. Hii ni tete mno na inaweza kutupeleka pabaya tusipokuwa makini. Ni mtazamo wangu tu... Najua wengi hawawezi kukubaliana na hoja zangu.

Mi' nipo hapa kila siku, ila ninakuwa mzigoni... Na kwenye ishu zinazonigusa sana huwa nachangia. Nitaendelea kutathmini JF baada ya uchaguzi kwa miezi kadhaa na tutajulishana mitazamo yetu.

MODS hawana budi kukaa kitako na kutathmini mwenendo wa JF... Sio vizuri kukaa pembeni na kutoa mimacho kuangalia malengo ya JF yakichakachuliwa na ushabiki.
 
stoooooppp jf ni platform huru ambayo inakusanya opinions basing on what is actually happening pia jinsi tulivyo. kama kuna watu wanaoongea punba, acha wacheue pumba zao, kama ni wapika kangara na tujue wako wangapi, kama ni wale wadini pia tuwatambue kwa proportion.

unless otherwise mtaturudisha kule kule kwa michuzi!!! ukisema kikwete mdini anakasirika hakurushi hewani. kwanza nadhani blogu ya michuzi ilianzishwa kupotezea jamii forum...

mafanikio ni makubwa sana. ondoa mambo ya moderations humu. halafu sio siri huu mtandao utangazwe hata kwenye magazeti. it is really the thinking foundation!
 
hamna bana thread ikiwagusa wakubwa zao wanakupa BAN...Kuna mtu alimwita spika mteule ana sura kama kinu kapigwa BAN ya milele..sasa si uonevu huo au ni kujipendekeza kwa MODs kwa wakuu wa serikali


Chezo hapa Mods wasilaumiwe, naamin kwa maana yoyote ile hayo maneno ni yatapewa tafsiri ya matusi. Nia ya JF si kusambaza matusi bali taarifa kwa manufaa ya nchi yetu. Hata matusi yangeelekezwa kwako naamini usingejisikia vizuri!
 
SN,

unajua nakubaliana na mengi unayoyasema. Nimekuwa na maswali mengi kwenye hii thread ambayo wahusika bado hawajajibu, sijaelewa sababu bado.

Kutoka kwako, hebu nisaidie, unadhani JF inawafikia wanawake kwa idadi sawa na wanaume? Unandani watu wa vijijini wanafikiwa kwa idadi sawa na wa mijini? Unadhani inawafikia watanazia wa viwango vyote vya elimu kwa uwiano?

Nitafurahi zaidi kupata majibu kutoka kwako au mwana JF mwingine yeyote
 
stoooooppp jf ni platform huru ambayo inakusanya opinions basing on what is actually happening pia jinsi tulivyo. kama kuna watu wanaoongea punba, acha wacheue pumba zao, kama ni wapika kangara na tujue wako wangapi, kama ni wale wadini pia tuwatambue kwa proportion...

Haya, angalia takwimu zifuatazo...

Waliojiandikisha kupiga kura ni takribani milioni 20. Waliopiga kura ni kama milioni 8. Tanzania ina watu zaidi ya milioni 40. Watanzania - waishio Tanzania - ambao wanatumia mtandao hawafiki hata laki 8 (hiyo takwimu inajumuisha hata wale wanatumia mtandao mara moja kwa mwezi).



...Kuhusu magazeti, Mwananchi na Raia Mwema walikuwa wanafanya vizuri. Lakini, unajua Mwananchi huuza nakala ngapi kwa siku? Niliulizia, nikaambiwa siku ambapo wanauza kuliko kawaida idadi ya magazeti haizidi 36,000 (Chanzo: Mwananchi) Unaweza ukazidisha hiyo namba mara 10-20 ili kujumuisha wale wanaoazimana, au mara 100 kujumuisha wanaobadilishana taarifa kwa njia ya maongezi… Taarifa kwa njia ya maongezi itakuwa inapoteza ule ukweli au ukamilifu…



Kweleakwelea, tafadhali nifahamishe 'proportion' ya wadini Tanzania, kwa kutumia vielelezo hapa JF au mitaani. Majimbo mangapi yalikuwa yanajadiliwa JF kwenye kipindi cha uchaguzi? Yanazidi 80? Ilikupa picha halisi ya mambo Tanzania kwa ujumla?
 
Kutoka kwako, hebu nisaidie, unadhani JF inawafikia wanawake kwa idadi sawa na wanaume? Unandani watu wa vijijini wanafikiwa kwa idadi sawa na wa mijini? Unadhani inawafikia watanazia wa viwango vyote vya elimu kwa uwiano?

Nitafurahi zaidi kupata majibu kutoka kwako au mwana JF mwingine yeyote

Ujue tukishaelewa na kukubali ukweli kuwa JF ni jamii fulani, basi mambo yatakuwa rahisi mno... Yaani, utajadili mambo hapa, lakini ukisafiri ukaenda Mwanga, Songea, Ifakara au Sumbawanga huko kuwaona wazee, basi utapata ile "perspective"; tusijifungie, tuchungulie Tanzania kwa ujumla inaendeleaje. Nadhani na wewe ndio unachojaribu kusema.

Tathmini yangu (ya watu wanaofuatilia mijadala ya siasa na JF) ni ya juu juu sana; ni kuulizia kwa ndugu, jamaa na marafiki tu. Hakika wanaume wengi zaidi huja hapa. Sitashangaa kusikia ni zaidi ya theluthi mbili ya watembeleaji (hilo ni kadirio la chini kabisa!). Vijijini huko hali bado sana... Ukiacha wale wenye internet ofisini, wangapi wana muda wa kwenda cafe kila siku kuangalia nini kinatokea kwenye siasa Tanzania, kila siku? Au hata mara moja kwa wiki? Nazungumzia wa miji mikubwa kama Dar, Arusha, Mwanza na Mbeya.

Lakini hali itabadilika kama nilivyosema -- huu mkonge mpya ukianza kufanya kazi utaona mapinduzi. Ila tutawafikia watani wa jadi kabla ya uchaguzi ujao?

Kuhusu viwango vya elimu, dah, kazi nzito hapo... Lakini hata wachache walioelimika hawafuatilii sana kama wengi tunavyofikiri. Na vijana ndio kabisa mzee -- ukiuliza unaweza ukatokwa na machozi (ingawa watu wanaonekana kuridhishwa na "mwamko" wa vijana kwenye uchaguzi uliopita. Wapiga kura milioni 8 tu? Na hawajui hata Katiba ya nchi ikoje na CHADEMA wanapigania nini? Hawaelewi hata chanzo cha "kelele" za Wazanzibari kwenye masuala ya Muungano? Labda mimi nina high standards; lakini hiyo ndio demokrasia ya kweli, kwa mtazamo wangu).

[Sisi tunatumia Google Analytics kufuatilia nani hasa hutembelea tovuti yetu, wanapendelea vitu gani (tunaona watu wengi hukaa muda mrefu kwenye kurasa/posts fulani), wasomaji wanatoka wapi, wachangiaji wanatoka miji gani n.k. Na sio vibaya JF ikatumia hicho chombo na kutoa taarifa kila wiki/mwezi... Ni cheap sana!]
 
SN,

siyo kwamba una high standards, naona umekuwa mpole kuliko mimi na ndiyo maana nataka kujua hizi kelele na makeke Hapa JF zina impact yoyote? Kwa kifupi umejaribu kusema Kama kuna impact yoyote ni kidogo na kupitia kwa watu wacheche sana wengi wao wanaume na walio na ajira rasmi.

Nitoe siri sababu nimeanzisha hii thread. Moja ni hiyo uliyoisema, asilimia ndogo ya wananchi waliopiga kura ingawa uchaguzi wa mwaka huu upashanaji habari ulikuwa mkubwa kuliko chaguzi zilizopita. Magazeti, tv, blog, simu, mihadhara, gumzo, n.k.

Sababu ya pili, sina ushahidi wowote kwamba tabia za watawala zimebadilishwa na mijadala mikali ambayo imetokea hapa JF (naomba radhi kama nimekosea). Pia sijaona serikali ikitolea ufafanuzi jambo lolote lililojadiliwa hapa JF kama wanavyojibu za magazetini. Je, ina maana audience wa JF siyo significant?

Sababu ya tatu, nilitaka kufuatilia frustration za MM siku moja alianzisha thread hapa akaonesha kugadhibishwa sana na jitihada alizokuwa amezifanya kupitia JF kuamsha uelewa wa watanzania kwa miaka yote hii bila mafanikio.

Hata uchagiaji kwenye hii thread umeona ulivyokuwa kidogo, unaashiria wazi tatizo la wadau wa JF. Fananisha na uchangiaji kwenye thread za uzushi dhidi ya wanasiasa, kama Zitto, kwa mfano.
 
Naelewa, na mimi nina utitiri wa maoni ya aina mbalimbali kuhusu matumizi ya mtandao Tanzania.

Sababu zako nimezielewa...

1. Kuhusu vyombo vya habari, magazeti, redio na televisheni ndio vitu ambavyo vina nafasi kubwa Tanzania. Idadi ya watu wanaosoma magazeti Tanzania inaweza ikakadiriwa kwa kutumia tarakimu nilizozitaja hapo juu (Itabidi uniamini tu, ukihitaji kuhakiki naweza kukutumia PM). Lakini watazamaji wa televisheni na wasikilizaji wa redio ni ngumu kukadiria.

Ukiacha hayo, magazeti ndio yenye "nguvu" zaidi, hasa kwenye mambo na mwenendo wa siasa. Kwa hiyo, binafsi natumia magazeti kama "gold standard"... Na blogs, na vyombo vingine kwenye mtandao vipo nyuma sana.

Ila, kuna waandishi wa habari na hata wahariri wa magazeti wanaokuja hapa mara nyingi tu.

Sijui kama hiyo inasema lolote; kuwa maoni yao yanaathiriwa na mijadala ya JF. Kwa mfano, kuhusu suala la Barabara ya Serengeti, kuna mtu aliweka ripoti zote zile muhimu kutoka TanRoads, ZFS na mashirika mengine hapa JF. Hii ilichukua takribani miezi miwili hadi pale Raia Mwema walipoandika makala moja kikamilifu kuhusu suala zima. Kumbuka, hizo ripoti zilikuwa zimezagaa tu kwenye mitandao... facebook, hapa, na mimi binafsi nimeshawahi kuandika makala kuhusu ile ishu (Utaona links kwenye makala hii: Vijana wa Tanzania tuamke!).

2. Hatuna ushahidi wa dhati wa tabia za watawala kubadilishwa na JF. Ila wanajua kinachozungumzwa; wakati huo huo, wanaelewa kuwa wachangiaji wengi hawako nchini (hata watu mitaani wanajua hilo). Lakini, wanajua ishu yoyote ile ikitokea, kama kuna documents zime-leak, basi zitawasilishwa JF KWANZA. Na waandishi wengine wa habari wanajua hilo pia... Ingawa haya mambo hayatabiriki. Mtu anaweza akatoa taarifa fulani hapa, lakini asiseme amezitoa JF. Ni ngumu sana kusema hadhira ya JF sio significant au haina umuhimu. Ina umuhimu wake mkubwa sana tu, na watu waendelee kutoa mawazo yao bila kusita wala kuogopa.

Ila JF kwa ujumla haitupi picha halisi ya mambo yanayotokea Tanzania (nazungumzia kipindi cha uchaguzi hapa). Lakini hali itageuka na kuwa na ule uhalisia zaidi baada ya miezi miwili mitatu baada ya hii homa kupita -- hasa pale ambapo uchambuzi yakinifu utahitajika.

3. Watu kama MM wasife moyo. Kufikia watu vijijini inahitaji zaidi ya kuacha maoni hapa. Kwa hiyo, nawashauri watu kama hao watafute vyombo vya habari (magazeti) ambavyo vitaweza kuchapisha makala zao. Hii ndio njia pekee waliyonayo. Binafsi nawaomba watu kama hao wasife moyo.

Haya mambo ya kutafuta mabadiliko hayatokei ndani ya mwaka mmoja. Inahitaji miaka mingi, kujipanga na uvumilivu wa hali ya juu. Vikwazo ni vingi mno. Lakini, hata tusipofika tunapotaka, angalau watoto wetu wakija wataendelea; kuliko wao wakija waanze upya kama sisi.

Uchangiaji kwenye thread hii... well, ndio Wabongo tulivyo (kila mtu ana visingizio vyake). Hapa watu wangetakiwa wajipange kila wiki ili kuandika makala nzuri -- tena inaweza ikawa hata kwenye mtindo wa maswali na majibu; mwandishi atakayechaguliwa apewe uhuru wa kuchagua posts (maoni) anayotaka na kujenga hoja yenye mitazamo tofauti. Hiyo itatufikisha mbali.

Usiku mwema jamani!
 
JF ina toa mchango mzuri sana LAKINI imeingiliwa na radicals wa chadema ambao wanakuwa bias kwa kila kitu hivyo wanashindwa kutafakari na kufikiri 'nje ya box' somehow wanaharibu maada kwa vile wanataka habari njema tu kwa chadema hawataki kukosolewa au kuelimishwa, hawataki viongozi au chadema ile challenged kwa vitu vyotevyote wakati mtu unatakiwa kukubali kukosolewa ili ujipime, watu hao ndio hawa wakipewaga nafasi za kushauri viongozi huwa wao ni kushangilia na 'yes sir' na kusema kila kitu safi sana kwa viongozi hata kama mambo yanaenda kombo hivyo kusababisha kuporomoka kwa dola na uongozi.
itapendeza sana kama watu watapunguza ushabiki na kuandika vitu objectively walau asilimia 85, halafu 15% iliyobaki akaweka uchama haitashusha hadhi ya JF na serikali nzima itakuwa inategemea JF kupata maoni fulani fulani kabla ya hata ya kuchukua decision au kupeleka bungeni
 
sio kupotea tu unaweza kupigwa BAN eti una lugha za matusi..MODs wamekuwa vibaraka na wanafanya mambo kwa interest za wakubwa zao huko serikalini..ukiisema serikali tu unaanza kuwindwa na pengine kupigwa BAN...wako emotional sana na hii inaharibu maana ya uhuru wa kuongea
thibitisha kauli yako kwa mifano hai mkuu.
Mie nimeinanga sana serikali inapofanya madudu na sijawahi kupokea hata warning seuse ban!!
 
SN,

habari za asubuhi. Nashukuru sana kwa mawazo katika post yako ya mwisho, very interesting!

Naomba nirejee mawazo muhimu kutoka kwako. Kwamba hadhira ya JF ni muhimu isipokuwa asilimia kubwa wako nje ya nchi. Pamoja na hivyo naamini ni sawa kwa sababu watz walio nje ya nchi wanapata fursa ya kushiriki, isipokuwa pale tu wanapoitisha maandamano. Tatizo la uelewa na ushiriki katika critical thinking liko zaidi vijijini ambako wapo watz wengi zaidi, na JF hawafiki.

Kwamba ziandikwe makala nyingi zaida kupitia magazeti. Shaka yangu ni wasomi wangapi watz wanaosoma makala. Hapa JF tu ukiandika nusu ukurasa watu wanalalama na wengine wanadiriki hata kuagiza wenzao wawasomee!

Sasa, binafsi naamini redio zinafikia watu wengi, hapa tz, kuliko chombo kingine chochote. Shida kubwa ni maeneo ya vijijini, tena. Wakati wa kampeni kuna mikoa walilalamika hawafikiwi na radio, za tz. Pendekezo kwa JF, kama wanaweza kuanzisha community radio kakika maeneo ya namna hii ili kuwafikishia habari zinazopatikana kupitia JF na magazeti ikiwa ni pamoja na kundesha mijadala live.

Nakubaliana na wewe kwamba mabadiliko huchukua muda, hivyo tuwe more creative kusaidia jamii yote bila ubaguzi kupata habari na kushiriki katika mijadala.

Mimi siyo mwandishi wa habari lakini.
 
Boma,

nashukuru kwa mawazo yako. Binafsi sikushtushwa sana na ushabiki uliorindima Hapa JF wa mapenzi ya vyama wakati wa Uchaguzi. Ndio ulikuwa muda wake, na ndo maana ilitokea wakati wa kampeni. Pili elimu ya Tanzania inafundisha watoto kukariri, siyo kufikiri. Tatu, historia ya tz muda mrefu haijawahi kukuza tabia ya kutofautiana kimawazo na mitazamo. Ukitofautiana na wenzako, hasa wakubwa, wewe ni mhaini unataka kumwaga damu.

Majuzi MM alisema anatamani aanze darasa la mantiki humu JF, kusaidia kupunguza tatizo la kuropoka na kutovumiliana
 
sio kupotea tu unaweza kupigwa BAN eti una lugha za matusi..MODs wamekuwa vibaraka na wanafanya mambo kwa interest za wakubwa zao huko serikalini..ukiisema serikali tu unaanza kuwindwa na pengine kupigwa BAN...wako emotional sana na hii inaharibu maana ya uhuru wa kuongea

What are the MODS for then. Ukiochangia mambo ya kipuuzi wakuangalie tu!, nadhani tuwe fair hata baada ya kuwalaumu MODS hao hao wameacha mchango wako uonekane kwa wengine. I think that is fair enough. How many posts are in this forum against the government unregulated?, yet unasema mods wanatumiwa na serikali. You are just being unfair and unconsiderate.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom