Bill
JF-Expert Member
- Oct 5, 2007
- 9,248
- 10,010
Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kutoa mwito wengine wafanye hivyo ili tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimmsingi sasa yanayohitaji kufahamiana na kukutana.
Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.
Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.
Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . )
Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.
Huyu Jamaa asituchanganye, maana naona hana sera, yeye a invite watu kisha anyamaze. Ikiwa usalama wa Taifa wamekosa mbinu za kujua wanaJF wanaolipua mabomu kwa ajili ya kuliokoa taifa lao ni akina nani ni bora atafute mbinu zingine na sio hii ya zama za mawe.
Haiwezekani nijitambulishe kwa jina langu kisha nimwagie upupu Fisadi Rostam au Lowasa kisha waniache. Hiyo TNP ni bora ukailekeza kwa Mafiosadi waliokutuma, sisi tuna professional body zetu kama NBAA au NBMM bado ziantufaa.