Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kutoa mwito wengine wafanye hivyo ili tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimmsingi sasa yanayohitaji kufahamiana na kukutana.
Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.
Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.
Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . )
Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.
Kabla sijaendelea mbele Mtsimbe ningependa unifafanulie hiyo sentensi hapo. Maana ulipowakaribisha wana JF hukusema hivo. Hivi unadhani ya kwamba Wana JF wote ni Graduates? Ama tutafall under Honorary maana hata kwa corporate hatuingii.
Nangoja ufafanuzi!
Watanzania ni lazima tujifunze tabia ya "kupeana shavu". Tusiangalie tu jinsi sisi tutakavyonufaishwa na jumuiya bali pia tuangalie jinsi sisi tunavyozinufaisha jumuiya hizo.
Sijaona ubaya wa rais wa TPN kualika watu kujiunga na TPN, kwanini baadhi yetu tuna mawazo hasi kwa kila jambo linalotolewa bila hata kufikiri? Hivi ni lini watz tutajifunza kuwa negative thoughts kills, and will never take you anywhere! Huu ni wito wa hiari kabisa kama unaona kuna jambo halifai kuna njia za kistaarabu za kuuliza na wa kumuuliza amejitokeza na sio kumattach kila mtu, "After all not everything is for everybody", kama huu si uwanja wako kuna pengine pa kukufaa. Mambo mengine yanadhihirisha wazi upeo tulionao katika maisha, kumbuka " Being positive or negative are habits of thoughts,that have a strong influence in life"
Mzalendo mwenzangu Zemarcopolo nashukuru sana kwa kututia moyo.
Kitu ambacho ni ningependa kuweka wazi ni kuwa TPN haiko pale kwa manufaa ya watu wachache au kikundi fulani cha watu. Kwa wale walio wanachama wanaweza wakahakikisha hili. Tumeona kutoka ndani ya TPN watu wakianzisha makampuni, Wengine wakipata kazi, wengine wakipata mikopo maalumu nk.
Najua Wanataaluma wengi wamekata tamaa kwa jinsi mambo yanavyokwenda kimaendeleo. Nia yetu wote ni kuangalia ni namna gani Wanataaluma tunaweza kuungana na kutumia fursa zilizopo kujiletea maendeleo makubwa bila kujitumbukiza katika siasa kama TPN na hatimaye kuleta maendeleo ya nchi.
Sanctus,
Shukrani kwa kuitumia JF kufikisha ujumbe. Kwangu hii inamaanisha unatambua kuwa JF inaweza kutumiwa pia kwa shughuli hiyohiyo ya kuwaunganisha wataalam wetu (nadhani nikiwemo mimi) kwakuwa JF si siasa tu pia tunaweza kuitumia kwa malengo tofauti tofauti.
Aidha, nakushukuru kwa ujasiri wa kufikisha hoja kwa hekima kubwa!
MTZ Mwenzetu umeeleweka,huo ni mwaliko ambao kila mtu ana hiari yake kwa utashi wake kuamua.
Kama hupendi, basi achana nao kuliko kutoa lugha isiyochujwa.Binafsi niliwahi kuwaona wakijieleza TBC1 Kipindi cha asubuhi cha Jambo Afica huyo MSIMBE na akina dada wawili,mmoja kiswahili kilikuwa kinampa shida kweli,anapendelea ngeli
Ohooo! Makubwa haya...
Nitakuja... Ngoja nione huko TPN kuna nini... Ila suala la kutumia majina halisi Mtsimbe sijajua una lengo gani haswa? Unawatakia Wapambanaji mema ama?
Kutumia hizi Alias doesn't mean watu ni waoga, hapana. Ni katika kuhakikisha yale ambayo tunashindwa kufanya tukilinda maslahi yetu na wale tegemezi kwetu yanakuwa wazi!!! Hata kama tunapambana na Wadhalimu kama Wazalendo, we gotta take care of our own! JF mwendo ule ule...
Nikitoka TPN ntawa na mengi!!!
Mtsimbe uko sawa rai yako ni endelevu na naiunga mkono.
Jamani kujumuika ni mwanzo, kuendelea kukaa pamoja ni hatua na kufanya kazi pamoja kama WANA TPN ni mafanikio.
Wamataaluma tumeanza kujumuika na sasa tuendelee kukaa pamoja ili tufanye kazi na hatimaye tufanikiwe.
BIG UP TPN founders, good idea.
I don't feel that way, sorry!
Hili jina "Tanzania Professionals Network" silipendi. Nina mashaka kuhusu members composition, mf. wangapi wanatoka mikoani? Kuna elements za ELITISM hapa.
Nilifuatilia kujua TPN ni nini na kwa nini mtu ajiunge. Nilichokiona hakifanani na unachokisema. Naamini TPN ilianzishwa kwa malengo mazuri, lakini nawaona ninyi kama bunch of people who joined kila mmoja akiwa na ka-mission kake kichwani. Halafu website yenu imekaa kisanii, I think you are withholding information.
Katika organisations zilizoko hapa Tanzania au nje ya nchi; ninyi tuwafananishe na organisation ipi?
Kabla sijaendelea mbele Mtsimbe ningependa unifafanulie hiyo sentensi hapo. Maana ulipowakaribisha wana JF hukusema hivo. Hivi unadhani ya kwamba Wana JF wote ni Graduates? Ama tutafall under Honorary maana hata kwa corporate hatuingii.
Nangoja ufafanuzi!
Yaani, hata km Bill Gates angelikuwa Mtanzania, asingeliweza kujiunga na tovuti hiyo. Au kwamba wenye mawazo ya kimaendeleo ni "graduates" tu! FUNNY!!
Mzalendo Mwenzangu Mzozo, ukiangalia katika katiba ya TPN imeandika hivi juu ya members, nanukuu:
ARTICLE THREE
3.1 MEMBERSHIP.
Membership of the Organization shall be open to:
3.1.1 Individuals who is of sound mind and attained the age of majority who are interested in furthering the work of the Organization and who will be appointed and approved by the Executive Committee and who have paid for the registration fees and annual subscription laid down from time to time by the Executive Committee. Must be Tanzanian Graduates from Higher Learning Institutions within or outside the country with a POSITIVE ATTITUDE, and;
3.1.2 Any corporate or unincorporated association or body which is interested in furthering the Organization's work and that has been approved by the Executive Committee and has paid for the registration fees and annual subscription (any such body is being called in this constitution "member organization").
3.1.3 Honorary Membership given to other individuals, groups or Corporate which supports the Vision, Mission and Objectives of Tanzania Professionals Network.
Ufafanuzi:
Lengo kubwa la kwanza ni kuwaunganisha Wanataaluma wote tuwe na sauti moja katika mambo ambayo taaluma moja peke yake isingeweza kuyashughulika, huku Agenda kubwa ikiwa "Financial Empowerment and Wealth Creation for Professionals".
Kwa sasa katika nchi yetu tulikuwa na pengo kubwa kwa kuwa vyama vingi vya Kitaaluma vilikuwa vinashughulikia mambo yanayohusu taaluma zao. Sasa kwa kupitia TPN tunaweza kuwa na Agenda ya Pamoja "Cross-Cuttin Issues".
Lakini hii haina maana kuwa wasio graduates hawawezi kuwa wanachama kwa kuwa wote wanaingia kupitia katika 3.13. hapo juu.
Ukiangalia katika katiba ya TPN ambayo inapatikana katika Website ya TPN under Resource Centre (http://www.tpn.co.tz/download.html), tunayomadhumunini ambayo yanawalenga wengi ambao siyo lazima wawe graduates.
Hata hivyo kuwa Graduate peke yake siyo tiketi ya kuwa mwanachama, tiketi yako ni ile commitment yako ya kupenda maendeleo na kuwa na "Positive Attitude"
Naitwa Sanctus Mtsimbe na naomba niungane na wana JF wengine waliojitambulisha kwa majina yao halisi na kutoa mwito wengine wafanye hivyo ili tuweze kuungana na kufanya mambo ya kimmsingi sasa yanayohitaji kufahamiana na kukutana.
Nimekuwa msomaji mkubwa wa JF toka mwaka 2007 na leo nimeona ni vema nami nijitokeze kuandika machache. Napenda kuishukuru na kuipongeza JF na uongozi na wanachama wake kwa kazi kubwa na nzuri manayoifanya katika kuleta changamoto mbalimbali.
Napenda kutoa mualiko rasmi kwa kuwakaribisha wana JF wenye mtazamo na mwelekeo wa kupenda maendeleo ya kweli kujiunga katika Mtandao wa Wanataaluma Tanzania (Tanzania Professionals Network, TPN). TPN ni mtandao unaowaunganiasha wanataaluma wa fani mbalimbali bila kujali nafasi au vyeo vyao ikiwa na madhumuni ya kuwezeshana Wanataaluma na Wananchi kwa ujumla kiuchumi na kifedha.
Kwa kuwa michango mingi ya Wana-JF ni kwa ajili ya maendeleo na ustawi wa Watanzania na Nchi kwa ujumla (Kitu ambacho TPN pia inafanya), karibuni sana tuweze kuungana na kuonana katika mikutano ya mara kwa mara ambayo ina lengo la kuboresha maisha yetu.
Kwa taarifa zaidi, tafadhali tembelea tovuti ya www.tpn.co.tz (Bado tovuti inaboreshwa . . . )
Na kama kuna ufafanuzi wowote unahitajika, tafadhali tuwasiliane kupitia barua pepe president@tpn.co.tz au +255-754-833-985.
TPN inatofautiana vipi na vyama/asasi nyingine za kitaaluma kama TLS, TAA, ERB, TAMWA, TAWLA, NBAA,CPT, MEWATA, ... Au ndio katika zile jitihada za kila mtu awe na ka-NGO kake?