JF Hip-hop frestyle battle

Mkuu lini utatupia hapa mistari ya hiphop inayohusu papuchi?
Sinaga Role model,nipo nipo,
Am look alike, kwa mikogo niko simple,
Wanazimika na wowooo,
Mi nazimika na bow wow,
Machizi nawapa michongo, kidogo dogo ma ex migongoo,
Am Realy nigger nawakomesha ile mbaya, wanakomaga mambwiga na Sauti kibaba ubaya,
Niko macho leta battle, nikuchalaze kwa kidogo nilicho nacho,
Ado ado naenda chato, soon ni mjini na Dar yatabaki macho,
Mi sio king wa free style ameshakufa,
R.i.P mangwair maana kitambo umepumzika,
Tumekuzika bado machozi yanachuluzika, umetuacha na majonzi na nyimbo twazuuzika,
Tunajificha tuna hide ID, mchozi bado yanatoka haki hazitusaidii,
Na vipi ben atatoka saa nane kwa time hii,
Ama kitambo ameshakufa na tuandike R.I.P.


Nani anataka battle na Mr Zero hapa.

CC Zero IQ


CC Zero IQ
 
Mbishi nakomaa kwenye hili game
Kitambo nasambaa natamba kwa kila sehemu
Wasiyonikubali kaa mbali
Najijua
Shilawadu kwa bongo ni kama udalali wanasumbua

Wanapima hivi viiinaa,
bado hawafikii
Jf yote mi ndiyo bora Mc
Marufuku kunikoti kama hauwezi freestyle, hisiya za Joti dhidi ya Mpoki Bepari, Natusua nikitua mi Alamasi we ni Zari,
Hizi zama za Magu usidis uepuke shari

Jemedari
Wa mistari kuntu
Ukishindwa ikopi kwenye daftari kwa uthubutu

Na vichwa vimejaa mashudu
MMU kamwe siwezi kuihusudu
Ni sawa na kula kibudu
Na hiyo ni haram niite Dudu
Konki
Ni nani asiye nifaham

Sauti ya vinanda
Kaa mbali brother kaka
Utapakatwa ukiendekeza udananda
Matapishi, wengi yanawatoka
Kwa wangu ubishi, napangua hoja bila ya kuropoka
RT wanani alert
Airplane catchs fire,
ni Iran
usisumbuke ukasema Ulaya
 
On the other side, hii chapter ni new nai' emphasize,
Besides
Mi ndo baba lao, na transfer energy kwangu hakuna umeme wa mgao

The new Tesla, nikianza kutesa wanateseka
Wanasanda, na
wanakula na mueleka

Sikiza hii fasihi, kasi yake ni kubwa ili tuwe pamoja inabidi uwe na bidii
Anga limekuwa jeusi
A.K.A Dudu killer ila kwa colour siyo nyeusi
Ukipotea kwenye njia mi ni dira oh you see!
Nguvu yangu ni kubwa haihitaji kiko-si

Strictly kwenye beat ni bad boy kwenye flow
Hii game ni kubwa kwa battle hatuto draw
Daily nipo high kwa cash na sipo low
Mi ni AC motor na change we DC uta' blow
 
Kindaki nicheki mi jamaa, kwenye uwanja wa vita makamanda hatuna unaaa
Sanaa
wana beep halafu wanajiachia ndani ya mtiti skamatiki kama nmeshikwa na ukichaa
na wana skip
Huu ni moto wa kigogo, wanaji pimp kwa ufeki mashori mixer mikorogo
Hii ni ngumu kichwa shudu umeingia ulingo wa Mbogo
Gusa unase
Mi mkombozi njoo nikutakase, ukicheka na popo subiri wakutomase
Uzi umelala kiubishi nautawala fake Mcs wamesha bounce na swagga zao za kikajala
Walijifanya chambo wamekuwa mbuzi wa kafara, uzushi kapuni kipaji hakipotei kimasihara
Naliamsha dude, after faraday ni Tesla
flow ya kielektroniki rege ipeleke kwa lucky Dube
Mistari ya moto na inawapa mkong'oto, hii ni sumu ya panya inayoua mpaka viroboto
ya moto mama analeta ya moto band
ukigusa full mnara na sibagui hata iwe stand, Kitaa kinaniita muhuni
nanena lugha chafu, sionekani kiurahisi nimejichimbia kama siafu.
 
unajoke public your so funy eti kwenye game kitambo na unafanya mambo/


hivi ilikuwa mwaka gani..?naona yuda eskaliot umeamua kumwaga shombo/

hivi inawajua bad evil wacha izo porojo,unayakumbuka mafuta ya kimbo/

kipindi hicho hata haukujua write verse ulikuwa kirikuu tena mtoto wa mama wa kambo/

achana na kasumba na uache hizo siasa kama mbunge aliyekosa jimbo/


Sent using Jamii Forums mobile app
mwana wangwe full gangwe
Kimashairi bado mdogo rudi home ukajipange
lichezee jiji ila usimchezee Makonda, Zero Brain ukimgusa mwana fasta nakubonda
nipo faster! ni jet Mc
naunguruma nipo imara chama bora ni Simba Fc
nna A plain Makaveli kwenye flow, we ni F plain wa kufeli kwenye flow
una damu ya Kinafeli lazima nikulaze store
Nipo high everyday usidhani ntakuwa low
Nakupoteza kwenye dira nakufuta hautorudi tena
Hutosikika kama siasa ya bongo na Mrema, verse moja upo hoi mi mpaka kumi sijahema
Kwa shombo zako za kuflow unanuka unakuwa mnato, mamende tupo full tunakuja kiminyato

Kulikoni unaingia kina usichokiweza
Hili chama la wana ukizingua tunakumeza
Hip hop ina wenyewe, na wenyewe ndiyo sisi
Kaa mbali mama mkwe uepuke Ibilisi
Kwa vina vingi kato sitokuwa Mufilisi
Chama lipo on zingua tukuanzishie mafisi
 
wanajifanya kuchana,
hafu wote hawana vina,
yo MCs moyo wanatiana,
naja kuwabana,
mbavu wanajua na wanajuana.

pumbavuuuu, kuweni tu mashabiki,
labda mtupe tu shavu, so lazma mshike biki,

we are not making lavu,
lyrics is so hot like from zebaki.
I divide those MCs in halves,
we're after talent and not luck.

ni hayo tu,
nitakuja kuwapigisha miayo round two,
kama huamini kasome mathayo tu.

am real mc, with a lot of lyrics.
I have depth, like blacksea.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hip hop sio ndumba, kwangu hip hop ndio mchumba,,
Nishavamia mwenye nyumba,, kaeni mbali wazee wa pumba,
Mi çoment mirefuu, et mnaita ndio michano,,
Endeleeni kucheza rafu, kitakachowapata Mimi simoo,,,,,!!
 
1.Freestyle za nikkimbishi na godzilla wakiwa clouds 2008 mwenye nazo azitupie hapa nmeztafta bla mafanikio

2.nay wa mitego - mitego mp3 mwenye huu wmbo tafadhari
 
Mama Samia,
Narudia tena sema Mama Samia,
Mkuu jemedari ndio Mama Samia,
Toka mwanzo nyota iling'aa,
Wapo waliotaka na wala hawakufaa,
Magu akakuona na flag ikapaa
Hadi sasa we ndio kifaa, nyota ya mchezo yaan superstar
Umesimama imara ndio mama wa taifa
Nikupe sifa au nikuombee shifa,
Leo tena mama Mwanza umekiwasha,
Kisa Machinga DC na DED umefurusha,
Hawakuelewi hawa bado wanazingua,
Kitaa kinakuelwa wewe ndi mama mlezi,
Tunasubiri na mkeka tusikie pongezi
Ukisha tuondelea tu yule boya ndezi,
Hakika mama akulinde mwenyezi.

Mapigo 16
 
Back
Top Bottom