Son of the Soil
Member
- Nov 16, 2007
- 21
- 0
Heshima mbele!
Mkuu Kitila asante kwa majibu mazuri, asante kwa watoa hoja wengine. Mimi yangu ni machache tu. Siamini kama kweli tumefika mahali tunasema tumeishiwa kiasi hichi na kusema kuwa hatuna cha kujitete au hata kuweka kitu mezani. Mimi ni Mtanzania na nitakufa na utanzania wangu:
1. Tanzania haiwezi kuendelezwa na wageni:
Tokea uhuru tulijua hili na tukajipanga vizuri kujiendeleza. Heshima yetu ilikuwa ni kupambana na umaskini ujinga na maradhi. Hizi ni sera murua na imara. Sitazungumzia azimio la Arusha, ila nitasema kuwa hatuwezi kuwa na sera bora yenye vipaumbele zaidi ya hivyo. Tatizo letu siku hizi tumekuwa watu wa tofauti sana. Tumeahirisha kufikiria na kuwa wepesi wa kuchukua sera zinazoitwa bora kwa vigezo vya wakubwa zetu. Kwa lugha ya Kitila ni Umalaya wa hali ya juu. Hivi kweli jamani tunaweza kuambiwa shida yetu na watu wengine? Hivi ukiumwa mguu kwa kiatu kukubana, maumivu unayoyasikia anaweza kuyajua mwingine kweli? Hivi tumekuwa fukara wa fikra kiasi hiki? Halafu anajitokeza mkuu wa nchi anasema tatizo letu ni kuwa hatuna wasomi/wataalaum wa kutosha! Mimi ni msomi na mtaalamu katika eneo langu, naomba nisihesabiwe kwenye kundi la wataalamu uchwara aliowataja mkuu wetu.
2. Ni kufilisika kimawazo kuamini kuwa ngome ya jeshi la marekani ni maendeleo kwetu.
Mimi siamini kama watoa hoja walikuwa wanamaanisha au wanatania. Kweli sijui imani hiyo wameitoa wapi. Jamani ngome ya wamerekani ni kwa ajili ya maslahi yao tu, hayatuhusu kiuchumi. Kama tunataka kweli kutengeneza ajira za maana kwa watu wetu, njia iko wazi za kiuchumi siyo hii! Kama tunakubali ngome hiyo iwe kwa sababu nyingine lakini siyo imani kuwa tutapata ajira kwa watu wetu.Hivi hatujifunzi kuwa uwekezaji uchwara ni sababu mojawapo ya sisi kubaki na nakisi ya fedha na kufilisiwa kirasilimali? Tuamke jamani na tujadili mustakabali wa taifa letu.
Ama kweli hoja ya Kitila ya nguzo na maadili ya kitaifa inajidhihirisha kuwa ya lazima. Tazama leo tunatetea ngome ya wamareakani kwetu eti kwa hoja ya ajira! Naomba wengine wasitusikie, maana itakuwa haki yetu kupigwa mawe.
Hivi kutoa mfano wa watanzania wanaofanya kazi ubalozi wa marekani kama mfano si ni kujitukana mwenyewe! Naomba tujenge hoja za lutengeneza ajira za kudumu na zenye staha kwa watu wetu ili tuendelee. Tukimeza kasumba ya kudhani kuwa wazungu wana uwezo zaidi, akili zaidi na kwa hiyo ni watu wazuri zaidi tutaumia. Mimi nasema tujenge uzalendo. Hivi kuna mtu anaweza kujenga hoja ya kukubali upuuzi kama ule wa mtafiti mzungu? Mimi naungana na Kitila, wakati nafanya utafiti wangu nilipata wakati mgumu sana wa kuonyeshwa nyaraka ambazo si za siri. Mpaka nikashtaki mahakamani na kupewa am,ri ya mahakama (Court Order) kuwalazimisha watu wa serikali waniruhusu kuziona nyaraka hizo. Tena hata siyo za siri.
Ukweli ni kwamba maendeleo siyo uchawi na tunaweza bila wazungu.
Heshima mbele!.