Jeshi la Polisi linawashikilia watu wawili waliosikika wakimhoji mtoto aliyejitambulisha kwa jina la Evaristo katika moja ya picha jongefu zilizosambaa katika mitandao ya kijamii.
Pia, Jeshi hilo limesema linamshikilia mtoto huyo na kuendelea na uchunguzi wa maelezo yaliyozungumzwa naye katika kipande hicho cha video akijinasibu kwa wizi wa watoto.
Katika kipande hicho cha video, mtoto huyo alisikika akijinasibu kwa wizi wa watoto akishirikiana na wenzake watatu kwa kuwarubuni kwa pipi.
“Nimeshateka watoto sita hadi sasa, wameshakufa,” alisikika mtoto huyo akihojiwa na watu wawili ambao zilisikika sauti zao kwenye video hiyo.
Taarifa ya kushikiliwa kwa watu hao imetolewa leo Jumatatu Agosti 26, 2024 na msemaji wa jeshi hilo, David Misime.