The Watchman
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 1,114
- 1,862
Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeonya wananchi kutojitokeza katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24,2025 wakati Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lissu akifikishwa mahakamani hapo, likisisitiza atakayejitokeza atashughulikiwa kwa mujibu wa sheria.
Katazo la Jeshi la Polisi kwa wananchi ni kufuatia wito wa Makamu Mwenyekiti wa Chadema, John Heche kuwataka wanachama wa chama hicho na wananchi kufika kwa wingi Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Aprili 24,2025 wakati Mwenyekiti wao Lissu akifikishwa mahakamani kusikiliza kesi ya uhaini inayomkabili.
Heche ameyasema hayo katika mkutano wa hadhara uliofanyika viwanja vya Mbezi, wilaya ya Ubungo Aprili 16,2025 wakati akihutubia mamia ya wananchi waliofika kumsikiliza, akiwahimiza wananchi hao kufika mahakamani hapo bila kuwa na silaha yeyote wala kufanya fujo bali wabebe vitambaa vyeupe na maji.
Akizungumzia wito huo, leo Aprili 17,2025 jijini Dar es Salaam Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Jumanne Muliro amesema jeshi hilo limefuatilia mipango ya viongozi wa chama hicho na kubaini siku hiyo kutafanyika vurugu.
Muliro amesema lengo la vurugu hizo ni kushinikiza mamlaka za kisheria kumwachia kiongozi wao ambaye anatuhumiwa.