Jeshi la Polisi lataja wahusika wa mauaji Kibiti mkoa wa Pwani

Na umenotice kitu? Eti wahusika haujawakamata na hata hauonyeshi kua upo kwenye kilele cha kumkamata lakini unamtangaza jina, hii inanikumbusha jamaa fulanj alitaja watu majina weeee na ikaishia hapo hapo.
Kuna ttzo gani hapo? Mbona USA walitangaza picha na jina la Osama bin Laden kabla hawajamkamata. Msijidai kupinga kila kitu
 
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa wa mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .

Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne picha zao zimepatikana .

Akizungumzia hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga ,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .

Alieleza ,jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao .

Kamanda Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraj Ismail Nangalava ,Anaf Rashid Kapera KAPELO ,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .

Wengine ni Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda ,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame .

Kamanda Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri na Omar Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja na ya Faraj na Anaf .

Alieleleza wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .

“Jeshi letu limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi ” alibainisha .

Kamanda Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji cha Nchinga .

Kamanda huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa .

Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi hilo .

Hivi karibuni jeshi hilo lilitangaza kuwa kuna mtandao wa majina ya wauaji 102 ambao wanawasaka hadi sasa ili kudhibiti vitendo vya mauaji vinavyotia hofu wananchi.
Kutoa hizo siri za kijasusi si ni kushindwa kwa zoezi la kuwakamata hao watu wasiokuwa na huruma!. Hapakuwa na haja ya kutoa siri zote hizo wakt ndo wapo kwny target ya kuwakamata!. Taarifa hzo zingetoka tyr walishaangamizwa.
 
Abdurshakur Ngande Makeo, Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda ,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame , Faraj Ismail Nangalava ,Anaf Rashid Kapera,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .
Wenyewe at work! Wazoefu
 
Akili za Makonda albert bashite, kuita wauza heroine siku tano baadaye wenyewe waende

utaratibu huu niwawenye vyeti bandia tu kama Makonda.

unatangaza majina ya wauwaji ili iweje....wakimbie?
 
Na Mwamvua Mwinyi,Pwani

JESHI la polisi mkoani Pwani ,limewabaini baadhi ya mtandao wa watuhumiwa wa mauaji yanayoendelea wilayani Mkuranga, Kibiti na Rufiji wapatao kumi na mbili akiwemo mwanzilishi wa mauaji Abdurshakur Ngande Makeo .

Aidha jeshi hilo linaendelea na msako kuwatafuta watu hao ambao wanne picha zao zimepatikana .

Akizungumzia hali ya kiusalama ya Mkoa kutokana na vitendo vya mauaji vinavyoendelea katika wilaya hizo ,Kamanda wa polisi mkoani hapo,Onesmo Lyanga ,alisema wanaendelea na mapambano na upelelezi kuwapata wahusika wote .

Alieleza ,jeshi la polisi limewabaini kwa majina na picha kwa baadhi yao .

Kamanda Lyanga ,aliwataja watuhumiwa hao kuwa ni Faraj Ismail Nangalava ,Anaf Rashid Kapera KAPELO ,Said Ngunde na Omary Abdallah Matimbwa .

Wengine ni Shaban Kinyangulia ,Haji Ulatule ,Ally Ulatule ,Hassan Uponda ,Rashid Salim Mtulula ,Sheikh Hassan Nasri Mzuzuri na Hassan Njame .

Kamanda Lyanga ,alieleza kwamba ,Saidi Ngunde inadaiwa anaishi Ikwiriri na Omar Abdallah Matimbwa anaishi Dar es salaam ambapo picha zao wanazo pamoja na ya Faraj na Anaf .

Alieleleza wengine nane bado picha zao hazijapatikana hadi sasa .

“Jeshi letu limebaini hayo kwa kushirikiana na wasiri wetu huku tukiendelea na uchunguzi zaidi ” alibainisha .

Kamanda Lyanga alisema ,watuhumiwa hao ,wamegundulika kuwa hupendelea kutembelea maeneo ya kisiwa cha Simbaulanga ,kisiwa cha Saninga kijiji cha Nchinga .

Kamanda huyo ,alifafanua kijiji kingine ni cha Mfesini kata ya Nyamisati na maeneo mbalimbali ya wilaya za Kibiti ,Rufiji na Mkuranga.

Jeshi hilo linatoa wito kwa jamii kutoa ushirikiano kwa siri kufichua watuhumiwa kwani wanahatarisha hali ya usalama kimkoa .

Limetangaza bingo ya kumpatia sh. mil .tano yeyote atakaefanikisha zoezi hilo .

Hivi karibuni jeshi hilo lilitangaza kuwa kuna mtandao wa majina ya wauaji 102 ambao wanawasaka hadi sasa ili kudhibiti vitendo vya mauaji vinavyotia hofu wananchi.

Mrisho gambo hayupo kweli kwenye hiyo list
 
Halafu kwa kutaka kuyaridhisha masikio na matarajio ya waTanzania, eti majina yote yaliyotajwa ya kiislamu, something smells fishy here. Am not falling for this shit, hii ni quick cover up guys kama kawaida yao.
Ingekuwa vema ungeyataja ya kwako baada ya uchunguzi wako..!! Sbbu mauaji haya sidhani kama yanakubalika kama wamekosea kuwataja baada ya uchunguzi wao njoo na majina yako baada ya uchunguzi wako.
 
Back
Top Bottom