Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)

Genius Man

JF-Expert Member
Apr 7, 2024
993
2,285
Kitendo cha Jeshi la Polisi kuzuia waandishi wa habari kutozungumza na wanasiasa huu ni ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu, vyombo vya habari na ni uvunjifu wa demokrasia na sio maelekezo ya katiba ya nchi ni uhalifu wa kutumia silaha.

Waziri wa Ulinzi na kamanda mkuu wa jeshi la polisi wanapaswa kujiuzulu na kushtakiwa kwa kushindwa kuongoza jeshi kwa miongozo ya kisheria tuliyo iweka.

Katiba yetu inatupa ruhusa kila mtanzania anayohaki ya kuzungumza mda wowote saa yoyote hakuna sehemu wanaposema tusizungumze kwenye mikutano ya nishati, lakini pia katiba yetu inawapa uhuru vyombo vya habari kuzungumza mda wowowte na saa yoyote haisemi wasizungumze kwenye mikutano ya nishati.
 
Waandishi wa habari sio magaidi wala wanasiasa sio magaidi jeshi la polisi kuzuia mazungumzo yale linakuwa limefanya kitendo cha kihuni kwenye nchi kwa kuzuia wajibu wa watanzania waliopo kwenye vyombo vya habari na siasa kuzungumza wale sio magaidi wala wahalifu ni watanzania.

Kwa mienendo ya uvunjifu wa kisheria ambayo kinyume cha kwenda kinyume na sheria za nchi kwa yoyote ni uhalifu sina imani na jeshi hilo pamoja na serikali inayoliongoza jeshi hilo kutekeleza matukio ya kihalifu.
 
Back
Top Bottom