Jeshi la Polisi Dar lakusanya Tsh milioni 918 ndani ya siku 10

Mmmmh, natamani kulisifia jeshi la polisi kipindi ambapo fine zitakosekana kwa madereva kutokuwa na makosa barabarani. Lkn kwa pesa hiyo kamanda Mpinga umeshindwa kazi. kazi ya mapato ni ya TRA sio polisi.
 
Ni mpuuzi tu anaweza kuunga mkono upuuzi huu, hapo umezalisha nini? ukiwa na akaunti 2 ukaamua kuhamishia pesa kutoka akaunti 1 kwenda nyingine sijui kama utajisifia sasa akaunti yako imenona!
 
Sasa PRA ndio inajaribu kuziba gap la bandari....ndio maana wanatakiwa kukamua kamuaa kila kituu kinachopita mbele yao! Target wafike mil 100 kwa siku.......watagawa hizo machine Tanzania nzima kazi iwe moja tu hadi tu park magari wataanzisha kodi ya parking hata ndani ya fence.......maana hakuna vyanzo vipya ubunifu umeishia kwa Mipango.....na Prof Faru Maghembe (Utalii)
Ukiona hivyo ujue kua watanzania wengi ni wazembe na hawataki kufuata sheria za bara barani!
 
Police revenue Authority ni wakusanyaji wazuri wa mapato. Nadhani kamanda Sirro anafaa kuwa waziri wa fedha kwa hii serikali ya Hapa nguvu tu!
 
Mimi majuzi tu nilipigwa faini kwa siku tatu mfululizo. Lakini siku ya tatu nilitoa kwa hasira mpaka yule askari akaniomba radhi na kuniambia siyo matakwa yao bali ni agizo kutoka hewani na wanatakiwa kukaa na kitabu cha Notification kwa siku tatu tu, huwezi unabadilishwa Idara .

Tutaendelea kuumizwa sana
ulitenda kosa hukutenda????
 
Hesabu ndogo tu ....50 x 30000=1,500,000/= .....halafu zidisha x 30=45,000,000 x 318=??....
 
Ukiona hivyo ujue kua watanzania wengi ni wazembe na hawataki kufuata sheria za bara barani!

Unavyoongea inaonyesha wewe si mtumiaji wa chombo cha moto, katika mazingira ya kawaida makosa madogo madogo hayepukiki na wao wapo wakiombea watu wafanye makosa, kumbuka lengo hapa kupata hela kwa hiyo hata iweje trafiki wakikuamulia lazima haitakosekana sababu. Baada ya viwanda kushindikana sasa mapato ya serikali lazima yatoke kwa wananchi kwa namna yoyote ile
 
Huu ni ujambazi wa mchana kweupe! Milioni 91 kwa siku! Duh!

Mimi majuzi tu nilipigwa faini kwa siku tatu mfululizo. Lakini siku ya tatu nilitoa kwa hasira mpaka yule askari akaniomba radhi na kuniambia siyo matakwa yao bali ni agizo kutoka hewani na wanatakiwa kukaa na kitabu cha Notification kwa siku tatu tu, huwezi unabadilishwa Idara .

Tutaendelea kuumizwa sana

Police Revenue Authority
 
Kama tukiendelea hivyo hakutokuwa na ulima ya kukopa na kuwa ombaomba.
Hongera kwa ubunifu huo
Kwangu mimi napongeza maana upumbavu ulizidi kwa madereva
Sasa haya mapato yanainfluence vip uchumi wa nchi? Kama tunajitekenya fulan hv unatoa pesa mfuko wa kulia unaweka wa kushoto..... Sawa penati zipo na ziiendeleeee sio kwa kukomoana lkn pia TRA na police wagundue adhabu productive na vyanzoo vingine vya mapato ambavyo vitastimulate uchumi wa nchi
 
Safi sana. Watu wameanza kuendesha magari kwa heshima barabarani.

Ila kuna kosa moja kubwa linalosababisha vifo ambalo polisi hawaonekani kulishughulikia bado. Ni kupita gari lililopo mbele yako sehemu isiyoruhusiwa. Hili kosa hutendwa sana kwenye barabara za nje ya mji na kila unaposikia basi limegongana uso kwa uso na lori huwa ni sababu hiyo. Don't overtake where the midline is bold
 
Watanzania wengi wamepoteza maisha yao kutokana na madereva wengi kutokufuata sheria za barabarani. Nchi nyingi tu hutoza hizi faini na ni chanzo kizuri sana cha kufanya barabara zetu ziwe salama zaidi. Safi sana kwa uongozi wa JPM kuvalia njuga kila nyanja kufanya kile ambacho walipa kodi wa nchi hii wanakihitaji.

BTW wanatakiwa sasa kutumia hizi pesa kununua speed cameras pamoja na vitendea kazi imara kuboresha usalama wa walipa kodi. Pamoja na 24 hrs surveillance cameras kwenye miji yetu kuondoa vibaka nk.
 
h
Kuna ka 30k changu wiki hii, nimeumia zaidi kuona hii taarifa
hata mimi aisee,halafu kosa lenyewe sasa....kwakweli nilimlaani sana kimoyomoyo kuwa ipo siku yatamkuta zaidi ya hiyo 30k yangu.halafu linakupa risiti huku linachekacheka....aargh!
 
Safi sana. Watu wameanza kuendesha magari kwa heshima barabaran.

Ila kuna kosa moja kubwa linalosababisha vifo ambalo polisi hawaonekani kulishughulikia bado. Ni kupita gari lililopo mbele yako sehemu isiyoruhusiwa. Hili kosa hutendwa sana kwenye barabara za nje ya mji na kila unaposikia basi limegongana uso kwa uso na lori huwa ni sababu hiyo. Don't overtake where the midline is bold
Augustine Moshi, oh my god ..... .. how are you? Aiseee mkuu nakukubali sana tangu mwanzo wa hii Forum (Jambo) habari za siku nyingi? Sijaona michango yako kwa muda mrefu aisee. Natumaini upo salama sana dah! God bless and have a wonderful day. Good to see you mate.

Dua la kuku halimpati mwewe.
 
Back
Top Bottom