Jeshi la kujenga taifa JKT litutumie Vijana kwa maslahi ya jamii zetu

PLATO_

Senior Member
Jan 25, 2020
115
223
Siku hizi kumekuwa na wimbi kubwa sana la vijana wanaopenda kujiunga na jeshi la kujenga taifa hasa wale wa mujibu wa sheria huwa wanajaa mno.

Ijapo kuwa jeshi hili halitoi ajira, lakini vijana wengi huwa wanapenda kuomba nafasi za kujitolea ili mradi tu watimize ndoto zao na wengine huamini kama ipo ipo tu, Na hata baada kukusa nafasi huwa wanauweka uzalendo mbele na kuvitumia mpaka mkataba unapokwisha.

Jeshi ni Tajiri wa rasilimali watu tena wenye ujuzi tofauti tofauti, kuna mafundi ujenzi, umeme, seremala, walimu, madaktari etc.

Lakini mnatutumiaje? Mbona kunashule hazina Madawati na sisi tupo? Kama tatizo ni miti mbona serikali inamisitu? Mbona shule hazina Nyumba za waalimu Madarasa vyoo na sisi tupo? kama tatizo ni kufyatua tofali mbona ndio kazi zetu. Bado kunasupport ya wananchi lakini sielewi tunakwama wapi.

Lakini pia ingependeza kila Kanda iwe na shule ya jeshi Watoto wanatakiwa kuanza kufundishwa uzalendo wakiwa wadogo maana vitoto vya 2000 vimekuwa vimabroila kama mnavyoviona wenyewe🤣🤣 (jokes)

Ndio shule za kikanda kwanza na ajira mpya zitazalishwa. Alafu nawaza "hivi kwanini msiamue kila mwalimu anaeajiliwa sharti awe mwanajeshi hapo mnakuwa mmepiga ajira 2 mara 1. ni kukaa tu na wizara basi mnayajenga. sio ualimu tu hata sekta nyingine

Mpaka miaka ya 2080 unaweza kukuta almost nusu ya wananchi ni wanajeshi. Uzalendo hapo unakuwa ni wa kutosha. usalama kila kona.

Au basi maana limekaa kama wazo la kijinga vile😂😂
 
Wazo lako zuri sana Kamanda, na lengo la JKT ni kumfanya kila kijana wa ki-Tanzania awe mzalendo na mkakamavu (asili ya uaskari). Ilivyokuwa zamani kila kijana aliyefika kidato cha 6, au chuo baada ya kidato cha 4, basi JKT ilimuhusu (kwa lazima/mujibu wa sheria). Na ukikwepa JKT ilikuwa huwezi kujiunga vyuo vikuu vya umma! Vijana waliokomea drs 7 na kidato cha 4, hawa mtaani mgambo (Jeshi la akiba) iliwahusu. Kwa mtindo huu kila mwananchi alikuwa na 'element' za kiaskari!

Wazo la vijana wa JKT kutumika kuimarisha miundombinu ya shule zetu (madarasa, vyoo, madawati, nk), ni la kufanyia kazi kwa hakika.
 
Back
Top Bottom