MBOKA NA NGAI
JF-Expert Member
- Jan 31, 2025
- 228
- 437
Msemaji mkuu wa kisiasa wa AFC/M23, Lawrence Kanyuka, ametangaza kwamba, wanajeshi wa Afrika Kusini waliopewa hifadhi katika kambi ya MONUSCO huko Goma, walitakiwa kuwa kwao kwa sasa, kwa sababu haoni wanachokifanya huko. Na aliongezea kuwa, muda ndo sasa, na AFC/M23 wapo tayari kuwapa njia ya kuondoka.
Jeshi la Afrika Kusini liliingia vitani mashariki mwa DRC, mwaka 2023, kupitia SAMIDRC, ushilikiano ulolenga kuiongezea nguvu DRC,kukabiliana na makundi yakigaidi, na mwisho wa siku walijikuta wakipigania upande wa serikali ulioshirikiana na FDLR,kundi la waasi wa serikali ya Rwanda, linalokabiliwa na tuhuma za mauwaji dhidi ya watutsi mwaka 1994. Ushilikiano huo pia ulikuwemo kundi la Wazalendo,jeshi la Burundi na mamluki kutoka nchi za Ulaya.
Januari mwishoni, vita vikali viliacha mji wa Goma mikononi mwa kundi la AFC/M23, wanajeshi 14 wa Afrika Kusini wakipoteza maisha, wengine walijikuta wamezingirwa na kundi hilo la M23, walilazimika kukimbilia kwenye kambi ya MONUSCO na kuomba hifadhi huko,ili wanusuru maisha yao. Wengine waliokuwa nje kidogo ya Mji wa GOMA(Uwanja wa ndege wa Goma, na mji mdogo wa SAKE), wapo chini ya ulinzi wa M23 mpaka sasa katika kambi zao huko.
Msemaji huyo, ametangaza kuwa, wao wapo tayari kuwapatia njia, lakini uongozi wao uligoma kukubali wanajeshi hao kusafilishwa kupitia Rwanda, na kuongeza kwamba, uwanja wa ndege wa Goma hauwezi kutumika kwa sasa, kutokana na kuharibika kwa njia ya ndege kulikotokana na makombola.
Afrika kusini ilituma wanajeshi zaidi ya 2,900, wakiwemo wa SAMIDRC
Bunge la Afrika kusini,limekuwa likihoji kilichowapeleka,kutokana na ripoti zisizoeleweka zilizotolewa na uongozi wa nchi hiyo, na kuomba wanajeshi hao warudishwe haraka iwezekanavyo.