Je, Watanzania tumeridhika kabisa na Dharau, Kejeli na Matusi anayotufanyia sasa Tapeli wa Kiimani 'Kiboko ya Wachawi' akitokea huko Kwao Congo DR?

Si Bure, kiboko ya wachawi Kuna pshala alikunyoosha maana sio kwa kunfungukia nyuzi kumi kumi.

Ila wewe wabongo kupigwa umeona ni kwa kiboko ya wachawi tuu? Watu wanajigamba na magoli mkono, kuingia porini, au kutumia bunduki kukiweka chama madarakani na unaona poa tu.
 
Ukiona mayowe mengi ujue ameshaliwa huyo.
 
Kiboko ya wachawi kilichomponza ni ubahili, alikuwa hataki kula na mamlaka.
Pesa zote alizopiga alikuwa anapeleka kwao Congo, mamlaka ikamfuata na kumwambia kuwa ni lazima na sisi utupatie 40% jamaa akagoma kilichofuata mnakijua.

Mwamposa, Kuhani musa na wengine wengi, wote ni kama Kiboko ya wachawi ila hawatoguswa na mamlaka kwakuwa wanapeleka fungu la kutosha baada ya kuwapiga MAZOMBIE.
 
Kwa Mwamposa Yesu yupo pale, kwanza halazimishi mtu kufika Kawe hata kwenye tv unapokea mibaraka, Matomaso ndio wanasafiri mpaka wafike live Kawe.

Ni makosa kumuweka Mwamposa kwenye kundi la kina Kiboko ya Wachawi, ukifuatilia mahubiri yao ni rahisi tu kumtambuwa yupi ni Apostle wa kweli.
 
Kubaini na kukubali udhaifu ndio hatua ya kwanza ya kutatua changamoto yoyote duniani wazungu wanaita ownership of the problem. Kuna matukio kama hayo yalishatokea na yanaendelea kutokea, hivi sasa wakati natoa comment hii Kuna watu wanapigwa lakini hatujifunzi, kwa nini. ?
Kwa hiyo Ili tutatue hili tatizo kwanza bado sisi Watanzania LAZIMA TUKUBALI wengi wetu ni WAJINGA
Angalia yaliyowahusu au yanaowahusu watu hawa

Babu wa Loliondo
Mchungaji Mwingira
Mzee wa Upako
Mchungaji Kakobe
Mtume/Nabii Mwamposya
Sharifu Majini
Kibwetele
Mr. Kuku, Zanzibar
DECI Mabibo
Gwajima
Na wengine

Hao mtaji wao mkubwa ni ujinga wetu. Hawana jinsi wanaweza ku survive ikiwa sisi tutakuwa werevu

Baada ya kukubali sisi ni WAJINGA, then tunafanya nini kutoka ktk ujinga huu ?

Serikali
Inaonekana haina shida na hawa watu na ndio maana wanaendelea ku survive. Kumbuka tukio la Moshi (Mwamposya)baada ya watu kadhaa kufa tulitarajia serikali ingechukua hatua lakini hicho hakikutokea na bado Mshua anatamba kwenye Majukwaa. Tunajiuliza
Kuna udhaifu ktk kusajili haya Makanisa/ Taasisi ?
Kuna rushwa ?
Kuna maslahi ya kisiasa wakuu wetu wanayapata kushindwa kuwachukulia hatua ?
Kuna udhaifu wa Kisheria ambao wanautumia kama uchochoro kiasi inakuwa ngumu kuwawajibisha ?
Ukiangalia tukio la Moshi baada ya kutokea tu. Waziri wa Home Affairs+ RPC wa Kilimanjaro, walikuwa wako tayari kuchukua hatua. lakini walivyomsoma boss wao JPM alionekana Hana shida na Mshua, hivyo jamaa (RPC + Waziri) wakapotezea hii issue
Yale makumi ya watu waliokufa kwenye lile tukio ikaonekana kama kifo cha panya tu
Na hii love affair haikuwa tu kwa Mshua wa Kawe bali ilikuwa kwa Gwajiboy + Mzee wa Upako

Jamii

Bado jamii yetu Iko nyuma ktk masuala ya kuwasiliana/kufunguka juu ya changamoto tunazokutana nazo
Kwa mfano hata humu JF kungekuwa na platform ya watu walioumizwa na matapeli wa aina hii
Motivational speakers kama Nanauka tulitarajia aje na vitu vya kutahadharisha wananchi wa kawaida na mada kwa mfano "UTAJUAJE KANISA/MCHUNGAJI NI MPIGAJI"
Katika suala hili nampa big up Mchungaji Hananja

Media

Kwanza nilipopata tu taarifa za huyo jamaa Kiboko ya Wachawi nikajiuliza media ambayo ilikuwa Ina host vipindi vyake hawa kuwa wanatathmini maudhui yake. ?
Kwa muda gani amekuwa akiendesha vipindi ?
Hapa sasa ndio naamini kwa kiasi kikubwa sana Mauaji ya kimbari ya Rwanda yalichochewa na media especially Radio

Education System

Kwenye mfumo wetu wa elimu za dini yaani EDK(Elimu ya Dini ya Kiislamu) + Divinity zitiwe mada maalum jinsi ya kung'amua Matapeli waliojificha kwenye kichaka cha dini
Lakini pia inaweza ikawekwa hata kwenye Civics/General Studies

Wakatabahu
 
Sasa ni rasmi Watanzania wachache waliokuwa Wakimuamini wametuponza mno Watanzania wote kwa anayotufanyia.
Nape, DC wa Longido, Mchengelwa , rais Samia, Polisi, CCM wote hao mbona wanajitapa zaidi ya huyo kiboko wa wachawinambaye mlikusanyika kwake na kumchangia kwa hiyari yenu?
Tena mlipaswa kumshukuru kwa kuwafungueni macho kwamba wapo wengi kama yeye huko nchini.
Kosa lake kubwa huyo kiboko ya wachawi ni kumu expose waziri wa serikali ya awamu ya nne Ndg. Masha alipoenda kanisani kwake. Kule kumu expose lilikuwa ni shambulio la aibu kwa serikali kama lilivyokuwa lili shambulio la waziri mwingine wa awamu iliyopita Ndg. Shukuru Kawambwa kule Bagamoyo.
 
Mi Kuna mdogo wangu aliniazima gari lake pale kwenye dash board kuna mafuta ya mwamposa, roho ikawa inaniambia yatupe nje, akiuliza utamwambia ulepeleka carwash madogo wameyapoteza labda
Mwisho wa siku nikayaacha tu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…