Je, Wanaoshangilia na Kupongeza Bajeti Wanajua Wanashangilia Nini? , Au Tunashangilia Ujinga?! .

Mkuu Beth, kwanza asante kwa kutuletea humu bajeti ya serikali, enzi za JK, budget day huwa ni siku muhimu sana, siku hiyo rais hapangiwa shughuli zozote hata kama kuna ugeni, haupangiwa kuja on budget day.

Hizi hesabu zimekaaje? au mimi ndio nazeeka nashindwa kufanya calculus?. Umepanga kukusanya tirilioni 32.48, ukafanikiwa kukusanya tirilioni 12.9 tuu, hata nusu haijafika, halafu unatuambia hii ni.87.4%?!

Tuelewesheni maana sisi wengine hesabu ni mbingu na nchi.
P
Jamaa kazingua hesabu gani hizi?
 
Ndugu yangu na rafiki yangu Paskali nionavyo miye KUNA TATIZO katika kufikiria kwa watu walio wengi (na hata baadhi ya wabunge wamo kundi hili), TAKWIMU bila uhalisia ni SIFURI....Yaani kusema katika familia: NTAWANUNULIA watoto woote baskeli (huku uwezo wako kama mzazi huwezi kukidhi mahitaji muhimu nyumbani kama chakula) ni URONGO mtupu. Hiki ndicho ninacho kiona katika hii kitu inayoitwa BAJETI ya Serikali...
Katika kupanga lazima upange makubwa( aim high) ndo maana inaitwa makisio sio halisi
 
Wajameni, bandiko hili bado liko valid, bajeti ya serikali kwa mwaka wa 4 wa awamu ya 5 ya rais Magufuli imesomwa jana, ikionyesha kwa miaka yote minne, hakuna hata mara moja, tumeweza kukusanya tulichotarajia. Swali ni kwa nini tunaendelea kupanga mi bajeti mikubwa kuliko makusanyo yetu?, hivyo kujikuta kila mwaka tunapanga bajeti tegemezi tukitegemea wafadhili na wasipotoa tunajikuta tunalazimika kukopa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kama ule mkopo wa dola milioni 500 kutoka benki ya Credit Suise ya Uswisi yenye riba ya asilimia 80%!. Tumekopa dola milioni 500, tutalipa dola milioni 900 baada ya miaka 5!.

Kwa nini tusipange cash budget yenye actualities, tupange kutumia kile tuna uwezo nacho, halafu akija mjomba na msaada wake, akiishatoa ndipo tupangie kilicho mkononi?.

P
Budget ya Tanzania ni kama mtu kacheza tatu mzuka akaota atashinda million 100 akaanza na kupanga kabisa nitanunua hichi na kile na anaishi kwa raha kabisa akiwa ana matumaini wakati wowote nitapigiwa simu ya ushindi lakini mara ghafla anatumiwa sms umeshinda alfu 10 hapo anapanguwa mipango anacheza tu 3 mzuka. Kawaida ya budget unapanga kwanza matumizi ya kawaida halafu ukijuwa tunamudu matumizi ya kawaida unaweka propose miradi ya maendeleo kwa vipaumbele vyenu katika pesa iliyobaki kwa maana makusanyo ya uhakika zaidi baada ya hapo miradi mingine inawekwa kwenye list kwa kusema tukipata ziada tutafanya kitu hiki hii unakuwa una review budget kila baada ya miezi 3 kuona ulichotegemea kupata na ulichopata na hapo unarekebisha number zako kwa kuangalia kwanini hatukupata tulifikiri tutapata ukijuwa sababu ndio utajuwa miezi 3 mingine utapata nini mbona haya mambo basic sana. kuna fixed cost ambayo ni matumizi ya kawaida mishahara na mambo ya kila siku ya lazima ila vitu sio vya lazima japo viko katika matumizi ya kawaida unakata ili kufidia. Budget ya mwaka jana hatukuweza kutimiza % leo bila kujuwa kwanini tunaongeza number tutapata wapi vyanzo gani? kwa kweli sijui la kusema naona siasa katika ubora wake...
 
Uzi wa Mayalla umenikumbusha ngoma za mdundiko mitaa ya Gongolamboto unaweza ukakuta ngoma.hiyo inaelekea Chanika, watoto wakajiunga kuja kushtuka wako Chanika na hata hawajui ngoma ilikuwa inahusu nini. Asante Pascal Mayala kutukumbusha tu namna ya kufikiri
 
042301d96ce598d1b63fe51c91a92ca3.jpg

Wanabodi

Kwanza naomba nami nianze kwa kuishangilia na kuipongeza hii bajeti kwa sababu tuu watu walipiga makofi, kushangilia na kupongeza, as when you are in Rome, do as the Romans does!, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu waliokuwa wakishangilia bajeti, wanashangilia nini?!.

Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeti ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali la logic tuu kuhusu failures za utekelezaji wa unrealistic bajeti tegemezi zilizotangulia ambazo tunapanga kutumia fedha ambazo hatunazo, tukitegemea makusanyo ya kodi zaidi, misaada na mikopo, kisha tunaidhinisha matumizi ya fedha ambazo haziko mkononi, mwisho wa siku, fedha ambazo zimepangwa na kuidhinishwa na Bunge, zinashindwa kupatikana, lakini kitu cha ajabu kabisa, serikali yetu inakuja na matumizi makubwa ya ajabu ambayo japo ni muhimu, kama ununuzi wa ndege kwa kulipa cash, lakini matumizi hayo hayakuidhishwa na Bunge!. Sasa kama kile tuu kilichopangwa na kuidhinishwa, hakikupatikana hicho kikubwa, kisichopangwa wala kuidhinishwa, kimetokea wapi?!.

Hoja zangu hapa ziko based on kitu kinachoitwa a common sense logic na sio economic indicators inawezaje kupanga kutumia kitu ambacho hauna, kisha unashindwa kutekeleza kile ulichokipanga kutokana na ukosefu wa fedha za utekelezaji, lakini ripoti ya CAG wako inakuja na taarifa ya matumizi makubwa ambayo hayakuidhishwa!.

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini? na wapongezaji wanapongeza nini?!, au nao wanashangilia tuu kwa sababu watu wanashangilia, na kupongeza kwa sababu watu wanapongeza, lakini hawajui wanashangilia nini au wanapongeza nini?!.

Mkiwa kwenye grupu la watu, mnapata kitu kinachoitwa a group pschology inayotokana na group mentality!. Mfano ni wakati mtu akihitubia halafu akaibuka mtu mmoja akianzisha kupiga makofi ya kupongeza, automatically hujikuta wote mnapiga makofi bila hata kujijua, na wengine wala hawajui ni makofi ya nini au msemaji amesema nini!.

Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa hata nusu tuu?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, lakini wakawa hawajui wanashangilia nini, jee ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?!. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha huku vyanzo vya mapato vikiwa ni vile vile, halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi kuliko ile iliotangulia na kushindikana, halafu watu wanashangilia?!. Watu hawa wanashangilia nini?!.

Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, angalau tujue tushangilie nini?.

Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza bajeti hii?!. Jee huku kuishangilia bajeti ya fedha ambazo hauna, yaani kushangilia tuu mipango kuwa nitafanya hiki, nitakusanya hiki, haiwezi kuwa ni kama ile ndoto ya Alinacha?. Kiukweli huku kushangilia usichonacho, sio kuishangilia ujinga?!. Jee kuna ugumu gani kama tungejipanga kwanza kutumia kile tuu tunachokusanya, tukakusanya kwanza, kisha baada ya kuona tunaweza ndipo tukapanga kutumia tulicho nacho mkononi, na kama kuna chochote ambacho tumeahidiwa na nchi wafadhili kupitia General Budget Support, tusikipangie kwanza, tusubiri, tukabidhiwe na kupokea ndipo tupange kutumia, ili ulifika wakati wa kushangilia, tushangilia matokeo lakini sisi tunashangilia mipango?!.

Wewe unaishi nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi na usafiri wako ni baiskeli, kisha jirani yako Apeche Alolo akajitokeza na kukuahidi kukujengea ghorofa na kukununulia Range Sports, kitu cha kwanza ni kuruka ruka kushangilia, au kujiuliza why and how?. Tuambizane ukweli jameni kwa uchumi wetu huu huu wa kijungu jiko, hii bajeti ya trillion 31 tunakwenda kuitekeleza vipi?.

Ili tupate maendeleo ya kweli, Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kuwa wakweli, kwa kujenga nidhamu ya matumizi, lazima tuje na realistic budget, tupange kutumia kile tuu tulichonacho mkononi na sio tulichoahidiwa, serikali yetu iache kabisa hii tabia mbaya ya kufanya matumizi makubwa bila kuidhinishwa na Bunge unless ni dharura kweli au majanga!, lakini dharura ya pangaboi!, kweli kulikuwa na udharura huo?!.

Pia natoa wito kwa Watanzania wenzangu, sasa tujenge utamaduni wa kushangilia matokeo, yaani results oriented achievements na sio kushangilia ahadi tuu hadi sasa kila kijiji bado kinasubiri zile million 50 zake za kila mwaka huku walimu wetu wakisubiri zile laptops zao!. Tunashangiliaje mipango badala ya kushangilia matokeo?

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu, Jee Wanashangilia Bajeti Hii, Wanajua Kweli Wanashangilia Nini au Wanashangilia Tuu kwa Vile Watu Wanashangilia, au ndio yale yale ya Watu Kushangilia Wasichojua, ikitokea Wakaletewa hata Ujinga Tuu, Watu wa Namna Hii si Watashangilia tuu?!.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti hii, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wetu wakijadili bajeti hii, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakilishi wetu wakichangia bajeti hii, hivyo Bunge letu tukufu kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali
Ni bajeti nzuri ya kizalendo.Pato la mtanzania limeongezeka kwa shs laki moja
 
Tabia hizi za NDIYOOO na kugonga meza kabla ya kutafakari ndio zimetusababishia sakata la makinikia ya dhahabu, kwa mfano; bajeti inapendekeza kufuta road licence na kuhamishia tozo kwenye petroli na mafuta ya taa; jamani kuna gari linalotumia mafuta ya taa?! Why punish hawa masikini?! Unamuona mbunge mzima anashangilia kama zuzu! Selfish interests zinatufanya tunajitoa akili ili kupitisha sheria na mikataba ya hovyo hovyo, no wonder tuliizika
rasimu ya katiba ya Warioba!! God save mother Tanganyika!!!
Kuna mambo mengie ni magumu mkuu yaani huwezi kupandisha petroli na diesel ukaacha mafuta ya taa bei ya chini kitachofuta ni mafuta yaa kuchangwa na diesel au petrol na wafanya biashara wenye tamaa.

Mimi nashauri badala ya kila mwaka kuanzisha vyanzo vipya vya kodi jambo ambalo sio baya, waangalie pia kipi kinakwamisha kufikia lengo la makusanyo ya ndani waliojiwekea. Binafsi naona bado kuna uzembe mkubwa kwenye ukusanyaji wa kodi unaofanywa naTRA. Wananchi wengi hawana elimu ya kodi hivyo kuna mapato kibao ya serikali ambaye yanapotea kwa wananchi kutokudai risiti za EFD.

Wafanya biashara wengi hawana tabia yakutoa risiti na hata ukiwadai baadhi yao wanato zile risiti za kitabu mpka uwe mjanja ukiwabana wanakupa za EFD. Sasa jiulize ni wananchi wangapi wanamuda huo ikiwa hata elimu ya kodi haija muingia, maana hata matangazo ya uhamasishaji siku hizi hamna TRA wameshindwa hata kuwatumia wasani kuhamisisha hili jambo.

Nashauri hili swala la kudai na kutoa risiti za EFD liwanyiwe kampeni kama ilivyokuwa kwa mifuko ya plastiki ndani ya mwezi mmoja tu naamini serikali itakusanya kodi nyingi sana iliyokuwa inapotea.
 
hii bajeti ni ngumu kuipongeza sababu iliyopita pesa nyingi hazikwenda sasa sijui hii watafanya miujiza gani ili ifanikiwe

Bajeti za aina hii hukumbushia kisa cha kina ZERO hawa:

Tunazurura kitaani huku stori zikiaendelea namwambia mzururaji mwenzangu ati mara pwa linaonekana burungutu, ndani kuna millioni. Tugawane! Mimi nasema lazma nichukue laki tisa, ndoto nimeota mimi. Ngumi zinaanzia hapo!
 
Uzi wa Mayalla umenikumbusha ngoma za mdundiko mitaa ya Gongolamboto unaweza ukakuta ngoma.hiyo inaelekea Chanika, watoto wakajiunga kuja kushtuka wako Chanika na hata hawajui ngoma ilikuwa inahusu nini. Asante Pascal Mayala kutukumbusha tu namna ya kufikiri
Hata mm nakumbuka mwaka 1992 tuliwahi kujikuta tupo chanika toka majumba sita

Dah nimekumbuka mbali Sana Aisee😀😀
 
042301d96ce598d1b63fe51c91a92ca3.jpg

Wanabodi

Kwanza naomba nami nianze kwa kuishangilia na kuipongeza hii bajeti kwa sababu tuu watu walipiga makofi, kushangilia na kupongeza, as when you are in Rome, do as the Romans does!, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu waliokuwa wakishangilia bajeti, wanashangilia nini?!.

Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeti ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali la logic tuu kuhusu failures za utekelezaji wa unrealistic bajeti tegemezi zilizotangulia ambazo tunapanga kutumia fedha ambazo hatunazo, tukitegemea makusanyo ya kodi zaidi, misaada na mikopo, kisha tunaidhinisha matumizi ya fedha ambazo haziko mkononi, mwisho wa siku, fedha ambazo zimepangwa na kuidhinishwa na Bunge, zinashindwa kupatikana, lakini kitu cha ajabu kabisa, serikali yetu inakuja na matumizi makubwa ya ajabu ambayo japo ni muhimu, kama ununuzi wa ndege kwa kulipa cash, lakini matumizi hayo hayakuidhishwa na Bunge!. Sasa kama kile tuu kilichopangwa na kuidhinishwa, hakikupatikana hicho kikubwa, kisichopangwa wala kuidhinishwa, kimetokea wapi?!.

Hoja zangu hapa ziko based on kitu kinachoitwa a common sense logic na sio economic indicators inawezaje kupanga kutumia kitu ambacho hauna, kisha unashindwa kutekeleza kile ulichokipanga kutokana na ukosefu wa fedha za utekelezaji, lakini ripoti ya CAG wako inakuja na taarifa ya matumizi makubwa ambayo hayakuidhishwa!.

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini? na wapongezaji wanapongeza nini?!, au nao wanashangilia tuu kwa sababu watu wanashangilia, na kupongeza kwa sababu watu wanapongeza, lakini hawajui wanashangilia nini au wanapongeza nini?!.

Mkiwa kwenye grupu la watu, mnapata kitu kinachoitwa a group pschology inayotokana na group mentality!. Mfano ni wakati mtu akihitubia halafu akaibuka mtu mmoja akianzisha kupiga makofi ya kupongeza, automatically hujikuta wote mnapiga makofi bila hata kujijua, na wengine wala hawajui ni makofi ya nini au msemaji amesema nini!.

Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa hata nusu tuu?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, lakini wakawa hawajui wanashangilia nini, jee ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?!. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha huku vyanzo vya mapato vikiwa ni vile vile, halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi kuliko ile iliotangulia na kushindikana, halafu watu wanashangilia?!. Watu hawa wanashangilia nini?!.

Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, angalau tujue tushangilie nini?.

Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza bajeti hii?!. Jee huku kuishangilia bajeti ya fedha ambazo hauna, yaani kushangilia tuu mipango kuwa nitafanya hiki, nitakusanya hiki, haiwezi kuwa ni kama ile ndoto ya Alinacha?. Kiukweli huku kushangilia usichonacho, sio kuishangilia ujinga?!. Jee kuna ugumu gani kama tungejipanga kwanza kutumia kile tuu tunachokusanya, tukakusanya kwanza, kisha baada ya kuona tunaweza ndipo tukapanga kutumia tulicho nacho mkononi, na kama kuna chochote ambacho tumeahidiwa na nchi wafadhili kupitia General Budget Support, tusikipangie kwanza, tusubiri, tukabidhiwe na kupokea ndipo tupange kutumia, ili ulifika wakati wa kushangilia, tushangilia matokeo lakini sisi tunashangilia mipango?!.

Wewe unaishi nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi na usafiri wako ni baiskeli, kisha jirani yako Apeche Alolo akajitokeza na kukuahidi kukujengea ghorofa na kukununulia Range Sports, kitu cha kwanza ni kuruka ruka kushangilia, au kujiuliza why and how?. Tuambizane ukweli jameni kwa uchumi wetu huu huu wa kijungu jiko, hii bajeti ya trillion 31 tunakwenda kuitekeleza vipi?.

Ili tupate maendeleo ya kweli, Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kuwa wakweli, kwa kujenga nidhamu ya matumizi, lazima tuje na realistic budget, tupange kutumia kile tuu tulichonacho mkononi na sio tulichoahidiwa, serikali yetu iache kabisa hii tabia mbaya ya kufanya matumizi makubwa bila kuidhinishwa na Bunge unless ni dharura kweli au majanga!, lakini dharura ya pangaboi!, kweli kulikuwa na udharura huo?!.

Pia natoa wito kwa Watanzania wenzangu, sasa tujenge utamaduni wa kushangilia matokeo, yaani results oriented achievements na sio kushangilia ahadi tuu hadi sasa kila kijiji bado kinasubiri zile million 50 zake za kila mwaka huku walimu wetu wakisubiri zile laptops zao!. Tunashangiliaje mipango badala ya kushangilia matokeo?

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu, Jee Wanashangilia Bajeti Hii, Wanajua Kweli Wanashangilia Nini au Wanashangilia Tuu kwa Vile Watu Wanashangilia, au ndio yale yale ya Watu Kushangilia Wasichojua, ikitokea Wakaletewa hata Ujinga Tuu, Watu wa Namna Hii si Watashangilia tuu?!.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti hii, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wetu wakijadili bajeti hii, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakilishi wetu wakichangia bajeti hii, hivyo Bunge letu tukufu kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali
Mkuu Pasco, kwanza salute kwako kwa kumiliki brain yenye uwezo wa kuwaangazia wengine waone vizuri mahali walipokuwa wanadhania wanaona vizuri kumbe walikuwa wakiona ukungu tu. Pili naunga mkono bandiko lako.
 
Unapo muagiza mkeo leo pika pilau, lazima umuachie Pesa ya mchele nyama, viungo...! Unaagiza lipikwe pilau huku unaandika BILA kuacha Pesa unategemea utaikuta pilau?? hhhhhhhhh...
 
Hata mimi nimewaza sana hii hesabu lakini nikaona kwa kuwa hesabu kwangu zilinipita kushoto
Mkuu Beth, kwanza asante kwa kutuletea humu bajeti ya serikali, enzi za JK, budget day huwa ni siku muhimu sana, siku hiyo rais hapangiwa shughuli zozote hata kama kuna ugeni, haupangiwa kuja on budget day.

Hizi hesabu zimekaaje? au mimi ndio nazeeka nashindwa kufanya calculus?. Umepanga kukusanya tirilioni 32.48, ukafanikiwa kukusanya tirilioni 12.9 tuu, hata nusu haijafika, halafu unatuambia hii ni.87.4%?!

Tuelewesheni maana sisi wengine hesabu ni mbingu na nchi.
P
 
Wajameni, bandiko hili bado liko valid, bajeti ya serikali kwa mwaka wa 4 wa awamu ya 5 ya rais Magufuli imesomwa jana, ikionyesha kwa miaka yote minne, hakuna hata mara moja, tumeweza kukusanya tulichotarajia. Swali ni kwa nini tunaendelea kupanga mi bajeti mikubwa kuliko makusanyo yetu?, hivyo kujikuta kila mwaka tunapanga bajeti tegemezi tukitegemea wafadhili na wasipotoa tunajikuta tunalazimika kukopa mikopo kwenye mabenki ya kibiashara kama ule mkopo wa dola milioni 500 kutoka benki ya Credit Suise ya Uswisi yenye riba ya asilimia 80%!. Tumekopa dola milioni 500, tutalipa dola milioni 900 baada ya miaka 5!.

Kwa nini tusipange cash budget yenye actualities, tupange kutumia kile tuna uwezo nacho, halafu akija mjomba na msaada wake, akiishatoa ndipo tupangie kilicho mkononi?.

P
Na bajeti ya mwaka huu ni bajeti ya 5!. Iko vile vile, mambo yale yale ni bajeti tegemezi!. Why?.
P
 
042301d96ce598d1b63fe51c91a92ca3.jpg

Wanabodi

Kwanza naomba nami nianze kwa kuishangilia na kuipongeza hii bajeti kwa sababu tuu watu walipiga makofi, kushangilia na kupongeza, as when you are in Rome, do as the Romans does!, lakini naomba kukiri kuwa mimi sio mchumi, hivyo sijui hata watu waliokuwa wakishangilia bajeti, wanashangilia nini?!.

Hivyo nimekuja hapa na swali kuhusu bajeti ambalo haliko based kiuchumi bali ni swali la logic tuu kuhusu failures za utekelezaji wa unrealistic bajeti tegemezi zilizotangulia ambazo tunapanga kutumia fedha ambazo hatunazo, tukitegemea makusanyo ya kodi zaidi, misaada na mikopo, kisha tunaidhinisha matumizi ya fedha ambazo haziko mkononi, mwisho wa siku, fedha ambazo zimepangwa na kuidhinishwa na Bunge, zinashindwa kupatikana, lakini kitu cha ajabu kabisa, serikali yetu inakuja na matumizi makubwa ya ajabu ambayo japo ni muhimu, kama ununuzi wa ndege kwa kulipa cash, lakini matumizi hayo hayakuidhishwa na Bunge!. Sasa kama kile tuu kilichopangwa na kuidhinishwa, hakikupatikana hicho kikubwa, kisichopangwa wala kuidhinishwa, kimetokea wapi?!.

Hoja zangu hapa ziko based on kitu kinachoitwa a common sense logic na sio economic indicators inawezaje kupanga kutumia kitu ambacho hauna, kisha unashindwa kutekeleza kile ulichokipanga kutokana na ukosefu wa fedha za utekelezaji, lakini ripoti ya CAG wako inakuja na taarifa ya matumizi makubwa ambayo hayakuidhishwa!.

Tangu kutangazwa kwa bajeti mpya ya serikali, nime note watu wengi wakiishangilia na wakipongeza bajeti hii, mimi ambaye sio mchumi ninajiuliza hivi washangiliaji hawa wanajua wanashangilia nini? na wapongezaji wanapongeza nini?!, au nao wanashangilia tuu kwa sababu watu wanashangilia, na kupongeza kwa sababu watu wanapongeza, lakini hawajui wanashangilia nini au wanapongeza nini?!.

Mkiwa kwenye grupu la watu, mnapata kitu kinachoitwa a group pschology inayotokana na group mentality!. Mfano ni wakati mtu akihitubia halafu akaibuka mtu mmoja akianzisha kupiga makofi ya kupongeza, automatically hujikuta wote mnapiga makofi bila hata kujijua, na wengine wala hawajui ni makofi ya nini au msemaji amesema nini!.

Unawezaje kuishangilia bajeti mpya kubwa kuliko bajeti ndogo iliyotangulia ambayo imeshindwa kutekelezwa hata nusu tuu?!. Ikitokea baadhi ya wapongezaji na washangiliaji, wanapongeza tuu na kuishangilia kwa sababu tuu watu wamepiga makofi, lakini wakawa hawajui wanashangilia nini, jee ikiwekwa hoja kuwa wanashangilia kitu wasichokijua, jee huku kutakuwa sio kuishangilia ujinga?!. Yaani itoke bajeti hewa ya kwanza ishindwe kutekelezwa kutokana na ukosefu wa fedha huku vyanzo vya mapato vikiwa ni vile vile, halafu inaletwa bajeti kubwa zaidi kuliko ile iliotangulia na kushindikana, halafu watu wanashangilia?!. Watu hawa wanashangilia nini?!.

Wachumi wetu humu tusaidieani akina sisi tusiojua uchumi kwa kutuelimisha kuhusu bajeti hii, ili kama ni kuishangilia, angalau tujue tushangilie nini?.

Naunga mkono kwenye mazuri kupongeza hivyo ni haki ya wabunge kupongeza mazuri yaliyoletwa katika bajeti hii, lakini kama hatujiulizi pale tuliposhindwa tulishindwa nini na badala yake kuja na bajeti mpya kubwa zaidi bila mipango madhubuti ya kuonyesha tutapata wapi fedha za kuitekeleza bajeti hii?!. Jee huku kuishangilia bajeti ya fedha ambazo hauna, yaani kushangilia tuu mipango kuwa nitafanya hiki, nitakusanya hiki, haiwezi kuwa ni kama ile ndoto ya Alinacha?. Kiukweli huku kushangilia usichonacho, sio kuishangilia ujinga?!. Jee kuna ugumu gani kama tungejipanga kwanza kutumia kile tuu tunachokusanya, tukakusanya kwanza, kisha baada ya kuona tunaweza ndipo tukapanga kutumia tulicho nacho mkononi, na kama kuna chochote ambacho tumeahidiwa na nchi wafadhili kupitia General Budget Support, tusikipangie kwanza, tusubiri, tukabidhiwe na kupokea ndipo tupange kutumia, ili ulifika wakati wa kushangilia, tushangilia matokeo lakini sisi tunashangilia mipango?!.

Wewe unaishi nyumba ya udongo iliyoezekwa kwa nyasi na usafiri wako ni baiskeli, kisha jirani yako Apeche Alolo akajitokeza na kukuahidi kukujengea ghorofa na kukununulia Range Sports, kitu cha kwanza ni kuruka ruka kushangilia, au kujiuliza why and how?. Tuambizane ukweli jameni kwa uchumi wetu huu huu wa kijungu jiko, hii bajeti ya trillion 31 tunakwenda kuitekeleza vipi?.

Ili tupate maendeleo ya kweli, Watanzania lazima tujenge utamaduni wa kuwa wakweli, kwa kujenga nidhamu ya matumizi, lazima tuje na realistic budget, tupange kutumia kile tuu tulichonacho mkononi na sio tulichoahidiwa, serikali yetu iache kabisa hii tabia mbaya ya kufanya matumizi makubwa bila kuidhinishwa na Bunge unless ni dharura kweli au majanga!, lakini dharura ya pangaboi!, kweli kulikuwa na udharura huo?!.

Pia natoa wito kwa Watanzania wenzangu, sasa tujenge utamaduni wa kushangilia matokeo, yaani results oriented achievements na sio kushangilia ahadi tuu hadi sasa kila kijiji bado kinasubiri zile million 50 zake za kila mwaka huku walimu wetu wakisubiri zile laptops zao!. Tunashangiliaje mipango badala ya kushangilia matokeo?

Namalizia kwa kulirudia hili swali la msingi la uzi huu, Jee Wanashangilia Bajeti Hii, Wanajua Kweli Wanashangilia Nini au Wanashangilia Tuu kwa Vile Watu Wanashangilia, au ndio yale yale ya Watu Kushangilia Wasichojua, ikitokea Wakaletewa hata Ujinga Tuu, Watu wa Namna Hii si Watashangilia tuu?!.

Keshokutwa Jumatatu, wabunge wetu wanaanza kuchangia bajeti hii, natoa rai kwa Bunge letu tukufu kuruhusu matangazo ya moja kwa moja wakati wabunge wetu wakijadili bajeti hii, kama waliweza kuruhusu matangazo ya moja kwa moja ya bajeti, pia tupate fursa ya kuwasikia wawakilishi wetu wakichangia bajeti hii, hivyo Bunge letu tukufu kututendea haki sisi wananchi

Jumamosi njema
Paskali

No asilimia ndogo sana budget inafuatwa an mwaka guy map to yatashuka itakuwa asilimia ndogo sana labda 20% tu
 
Back
Top Bottom