Wild Flower
JF-Expert Member
- Jul 20, 2023
- 372
- 751
Sheria ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi inatoa haki mbalimbali kwa mhusika wa taarifa binafsi ili kuhakikisha faragha na ulinzi wa taarifa zake. Haki hizi ni pamoja na:
- Kufahamishwa kuhusu ukusanyaji na madhumuni ya ukusanyaji wa taarifa hizo.
- Kukataa kutoa taarifa binafsi ikiwa mkusanyaji hataeleza madhumuni ya kukusanya taarifa hizo.
- Kuomba na kupatiwa nakala ya taarifa zake binafsi zilizo katika taasisi au mtu husika.
- Kurekebisha au kusahihisha taarifa binafsi iwapo zina makosa au hazijakamilika.
- Kuomba taarifa binafsi kufutwa ikiwa hazihitajiki tena kwa madhumuni yaliyokusudiwa au kama zimechakatwa kinyume cha sheria.
- Kuwasilisha malalamiko kwa Tume ya Ulinzi wa Taarifa Binafsi ikiwa anaamini kuwa haki zake zimekiukwa.