Je, umemgonga mtu na ukagundua 100% haujaonekana utafanyaje?

Kuna jamaa alikua na pick-up akamgonga mtu alikua anavuka tena kwenye zebra, ile paaaaah mtu aliegongwa akarushwa juu kisha akaja kutua ndani ya bodi ya ile gari, sasa dereva yeye hakuona kuwa aliegongwa katumbukia kwenye bodi ya gari, na kwa kuwa ilikua usiku dereva hakunotice kitu yeye akaamua kuchukua maamuzi ya kukimbia...
Acha utani mkuu duuh...!!
 
Kuna siku ilikuwa asubuhi tunawahi gari ya mkoa ubungo sasa sister alikuwa faster sana na garii kuna kona tulipigaa ghafla akashtuka gari imepanda kama tuta vile lakini kuangalia kwa mbali kumbe ni mtu alikuwa kalala barabarani sijui alikuwa kashakufa ua alikuwa mlevi hilo hatukujuaa maana hatukusimama...!!
 
Kuna siku ilikuwa asubuhi tunawahi gari ya mkoa ubungo sasa sister alikuwa faster sana na garii kuna kona tulipigaa ghafla akashtuka gari imepanda kama tuta vile lakini kuangalia kwa mbali kumbe ni mtu alikuwa kalala barabarani sijui alikuwa kashakufa ua alikuwa mlevi hilo hatukujuaa maana hatukusimama...!!
Aisee
 
Mungu atunusuru na mtihan huo, kuna m1 alimgonga mtu ila akamchukua akampeleka hosptal akawa anaenda kumuangali mara kwa mara. Kuna cku akawa anatoka kumuangalia c akakutana na ndgu yke kwnye kusalimiana yle ndgu akasema anaenda kumuangalia mwanae kapata ajal kumbe ndo yule aliyemgonga yeye
 
Jumapili moja hiyo Mwanza (mwaka siutaji), mchana tulianzia The Joint Isamilo hiyo, saa 2 usiku tukahamia Igoma pale City center piga sana mtungi hadi saa 6 hivi usiku, jamaa yetu mmoja akatuita pale Taiwan maeneo Nyamhongolo (wakazi wa Mwanza wanafahamu hivi viwanja).

Yule mjinga alifanya kufuru pale, ilikuwa ni mwendo wa weka kreti toa kreti mtiririko moja kwa moja, kwenye saa 8 hivi usiku mmoja wetu akatoa ushauri twendeni Jb Belmont wakati huo anapiga mziki wa Squencer jamaa mmoja anaitwa Zarii Edosha, tuna magari mawili.......hao vyombo vikawaka tukachomoka zetu kwenda town, kama mashindano ya magari vile.

Kufika mabatini kwenye lile daraja kuna mlevi mmoja anakatiza kilevi pale.....weeeeeeeeeeeeee............aisee tulimfyatua vibaya sana, tuliokuwa kwenye gari pombe zikakata, dereva akachanganyikiwa nikamwambia usisimame, nyoosha moja kwa moja, nikawapigia wenzetu wa gari ya pili nikawaambia wasitufuate wao wanyooshe sisi tukapandia mlango mmoja haooooo tukanyoosha, pitia njia za nyuma nyuma hadi tukatokezea furahisha daraja la Rock city mall.

Boda boda wakajichanganya wakaanza kuifukuzia ile gari ya nyuma yetu wakijua yenyewe ndio imegonga, jamaa full kutetemeka hawajui wafanyeje, nikawapigia kuwaambia nyie route yenu isibadilike iendelee kuwa ya Jb Belmont, na wakiwakuta pale msikubali kama tulikuwa pamoja, ndio kilichotokea tukawa tumesevu ivo hadi leo.
 
Jumapili moja hiyo Mwanza (mwaka siutaji), mchana tulianzia The Joint Isamilo hiyo, saa 2 usiku tukahamia Igoma pale City center piga sana mtungi hadi saa 6 hivi usiku, jamaa yetu mmoja akatuita pale Taiwan maeneo Nyamhongolo (wakazi wa Mwanza wanafahamu hivi viwanja)...
Ulimugonga baba mkwe wangu
 
Naomba nikiri mimi binafs nilisepa victim alikuwa na baiskeli had leo skujua if she is alive or not maana ilikuwaa mkoani huko usku..Lkn kijiji hakikuwa mbali sana
 
Ingekuwa nchi za watu nasimama, ila Bongo sisimami.

Yaani wewe, ni fulu kopiraiti na baba Taibali aahahahhaaaaa

Kuna mabungo mawili yako kwenye ungo na pilipili ya unga ile nyekundu iko pakti nzima, nasubiri pakuche nikudolishie....
 
Kuna siku nlikua natoka kwa mchuchu Sasa akawa amenivuruga nkaomdoka na mattress yangu jamaa wa bajaji akijichanganya nikampush akaingia mtaroni Sasa wenzio wakawa wamenidukua wakaanza kunikimbiza ile siku ndo nilijua kumbe ninaweza kuingia kwenye mbio za magari maana nilijua kuifumua haswaaa kila nikiwachek kwenye site mirror nawaona tu na vibajaji vyao vinayumba yumba tu niliwapiga gap la hatar wakaamua kuniacha niende zangu maana kulikua hakuna dalili za kunikamata na njia ilikua nyeupeeeeeee
 
Kuna jamaa alikua na pick-up akamgonga mtu alikua anavuka tena kwenye zebra, ile paaaaah mtu aliegongwa akarushwa juu kisha akaja kutua ndani ya bodi ya ile gari, sasa dereva yeye hakuona kuwa aliegongwa katumbukia kwenye bodi ya gari, na kwa kuwa ilikua usiku dereva hakunotice kitu yeye akaamua kuchukua maamuzi ya kukimbia..
Unafanyaje kwa situation hii?
 
Uaminifu, utu, ubinadamu ni jambo binafsi.

Sijawahi kupatwa na hiyo hali na sijajua ikitokea ntafanya nini.

Mola, niepushe na majaribu mojawapo ni kama hii. Amen!
Umesema cha maana,hili jaribu lisikubate aisee wewe wala jamaa yako .Mungu utuepushe Amen
 
Back
Top Bottom