Je, ulifika Third floor(30s) bila kuwa na familia? Hali ilikuwaje?

Kuna kitu nahitaji kuwafunza mabinti ambao hawajafika 30.

Ukipata mpenzi ukamuona ana hofu ya Mungu, maisha yake yapo wazi hasa tabia zake, anakupenda kwa dhati, yupo tayari kukutambulisha kwa ndugu zake na kwa familia yake.

Yamkini asiwe na kipato kikubwa sana ila ana uwezo wa kufanya wote mle na mkalala, ISHI HAPO.

Acha tamaa za kutaka uolewe na mwanaume mwenye pesa, anayefanya kazi TRA, bandari, mfanyabiashara mkubwa, mwenye muonekano fulani n.k mwisho mtakuja kuangukia kwa wanaume za watu au kwa wanaume ambao wataishia kukuchezea. Kumbuka sehemu kubwa ya mwanaume mwenye pesa, ngono anachukulia starehe tu, kwahiyo atakuchukua na kukutumia baada ya kukutamani akijua anapiga na kupita zake.

Binti yangu, huyo mwanaume wa mtu unayemuona ana pesa, hazijaja tu hivi hivi, alianza chini kabisa kama huyo kijana ambae kwa sasa wewe unamdharau.

Kama umewahi kumnyanyasa kijana wa watu kisa masikini, yeye sijui hana umbo zuri n.k moyo wake ukaumia, katafute suluhu naye sababu huenda kuna mambo yako yakafunguka.

Mabinti sio kwamba mnakosa watu wa kuwaoa ila tamaa za maisha zimekuwa zikiwatesa wengi, (kumbuka Hawa alidanganywa kwa kutamani pale bustani ya edeni, mwanamke ukiishinda tamaa una sehemu kubwa sana ya kuishi maisha ya furaha duniani). Mnapenda smartphones, kila wiki msuke, utolewe out n.k mnaishi maisha ya udangaji kisa mna uzuri wa sura au mna matako makubwa, kwa bahati mbaya sana, ukishazoea kudanga, mwanaume yeyote atakujua tu, udangaji ni kama ngozi, HAIJIFICHI na hata ukijitahidi, mtu atasikia tu stori zako.

Sasa hivi kijana wa 30, 31, 32 ambapo kwa sehemu kubwa ndo vijana wengi walau kwa sehemu wanaanza kuona mwanga ktk eneo la uchumi hawezi kuwa na mwanamke wa 30, lazima atafute wa 24, 25 au 26 unless awe mpumbavu.

Girls kuweni makini sana na umri, uliowatupa kisa hawana ela, wakipata ela na wao watakuona wewe sio hadhi yao. Tafuta kijana mwezio mtakaopendana, mtie moyo ktk utafutaji, mpende sana na kumpa heshima hata pale ambapo anapungukiwa, mwanaume huyo hatokusahau.
AHSANTE SANA NIMEONDOKA NA KITU
 
Back
Top Bottom