IROKOS
JF-Expert Member
- Aug 13, 2011
- 10,182
- 7,838
Huu ni usuluhisho wa mda.
Dawa ni wafugaji kuweka senyenge maeneo yao yote na kuachana na open ranching.
Ng'ombe wakionekana nje ya senyenge utakuwa uchokozi na wataifishwe. Mfereji una haribu mazingira na si salama.
Pia uta saidia kwa maeneo madogo na nighari kwa vijiji vikubwa
Mkuu kisheria kila Kijiji kinatakiwa kuandaa na kupitisha mpango wake wa matumizi bora ya ardhi ya Kijiji. Jambo hili linaratibiwa na tume ya taifa ya matumizi bora ya ardhi (NLUPC) na kutekelezwa na Halmashauri za wilaya husika ambazo zinatakiwa kuwa na timu ya wilaya ya matumizi bora ya ardhi (PLUM team).
Kijiji ambacho kimeandaa mpango huu kinakuwa kimetenga maeneo yake yoote kwa matumizi mbalimbali (kilimo, malisho, makazi, makaburi etc) na maeneo hayo huwekwa vibao vinavyoelekeza hayo matumizi na katazo kwa kisichokatikiwa (mfano: Eneo la Mashamba...ni marufuku kulisha/kuchungia mifugo; ...eneo la malisho..marufuku kulima..etc). Katika moja ya mikutano ya NLUPC niliyopata kushiriki niliona takwimu kwamba vijiji vya Tanzania vyenye mipango hii ni chini ya 30% (wakati huo idadi ya vijiji ilikuwa around 15,000; maana kabla ya uchaguzi vimeongezwa tena).
Kwa maelezo ya hapo juu utaona bayana kwamba tuna sheria nzuri tuu ambayo ingesaidia sana kukabiliana na hii migogoro ya kugombea matumizi ya ardhi. Tatizo liko wapi sasa?? Kwanza vijiji vyenye mipango hiyo ni vichache, pili hata hivyo vijiji vyenye hiyo mipango ya matumizi bora ya ardhi (ambayo ipo kisheria na imepitishwa na mabaraza ya madiwani ya halmashauri mbalimbali) haitekelezwi kabisa!! Ndiyo maana hata mawaziri wanapokwenda kutatua hiyo migogoro inapotokea sijawahi kusikia wakianza na kumuuliza DED, DC au Afisa ardhi je kijiji hiki kina mpango wa matumizi bora ya ardhi? je mpango huo unasemaje kuhusu maeneo ya kulisha mifugo na mashamba? Kwa hiyo kuna haja ya watu wa tume (NLUPC) kutuambia je kuna umuhimu wa vijiji kuandaa hii mipango kama sheria inavyotaka ikiwa haifuatiliwi?
Tatizo lingine ambalo nimeliona ni serikali yenyewe kujichanganya: Unakuta Serikali imegharamia kuwezesha vijiji kuandaa hii mipango, mfano mwaka juzi hukohuko Mvomero NLUPC walisaidia vijiji zaidi ya 40 kuandaa hii mipango (mamiliono yalitumika). Lakini baada ya miezi sita tuu baadhi ya vijiji vilivoandaa mipango hiyo vikagawanywa na kuunda vijiji vipya (nadhani hili linasimamiwa na Tamisemi) na matokeo yake vijiji vivyo mipango yake ikafa hata kabla ya kuanza kutumika kwa sababu mipaka ya kijiji na ukubwa vimebadilika. Kwa hiyo utaona kwamba serikali inajivuta shati yenyewe kwa kupunguza idadi ya vijiji vilivyokuwa na mipango yake kwa kuanzisha vijiji vipya kisiasa.