Akilihuru
JF-Expert Member
- May 20, 2022
- 1,511
- 2,967
Ishu vipi wakuu,
Kama swali linavyouliza hapo juu, narudia tena kuuliza. Je, serikali yetu ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na kuendeshwa na Rais Samia au Waziri Mkuu Majaliwa?
Nauliza hivi kwa sababu kuna madudu mengi yanayofanywa na viongozi wa serikali ambao wengine ni wateule wa Rais, lakini cha kushangaza mpambanaji wa madudu hayo ni mmoja tu Majaliwa peke yake, huku mwenye dhamana na jukumu kuu la kuchukua hatua Rais Samia na Makamu wake Dkt. Mpango wakiwa busy kupambana na wanaopinga mikopo badala ya ku deal na wabadhilifu wa mali zao.
Raisi Samia na makamu wake wamekuwa wakikutana na madudu mbali mbali katika ziara zao lakini hakuna hata siku moja ambayo waliwahi kuchukua hatua ya papo hapo dhidi ya wafanya madudu hao. Je wanakuaga wanawaogopa au kuwaonea aibu wafanya madudu hao?
Juzi kati makamu wa raisi ambae ni mtu wa pili kwa nguvu ya madaraka baada ya ile ya kwanza inayoshikiliwa na raisi alikabidhiwa majina ya familia 12 zinazoitafuna nchi ili achukue hatua. Lakini cha kushangaza makamu huyo hakuchukua hatua yoyote zaidi ya kuwahadaa watu kwamba anakwenda kulifanyia kazi swala lile bila kusema itamchukua muda gani kumaliza kulifanyia kazi swala hilo na kuwachukulia hatua wahusika.
Mbona Majaliwa huwa haombi muda wa kulifanyia kazi swala la namna hiyo na badala yake huchukua hatua ya papo hapo?
Je, kama wote watatu wangekuwa wanachukua hatua hizi za Majaliwa unafikiri ujinga huu wa kupiga hela ungeendelea?