Je, serikali itaruhusu mafuta ya Alizeti kutoka Marekani yaingizwe nchini na kupelekwa Dodoma wakati Singida wauzaji wanakosa soko?

Resilience

JF-Expert Member
Jan 4, 2023
1,038
4,752
Waziri Bashe ameongea kuhusu msaada wa mchele na mafuta kama vile yeye siyo waziri mwenye dhamana. Anaonyesha kushtushwa na mchele huo na mafuta kuingizwa nchni.

Je, kama sovereign state tutaruhusu kuletewa mafuta ya alizeti ambayo hata Dodoma na Singida yapo? Hii misaada nani huwa anakwenda kuomba? Lakini hata kama ni misaada, Dodoma watoto wamekosa msosi?

Uhuru wetu upo wapi? Kwanini tunakuwa wapole sana kwa mambo yasiyohitaji upole? Kwa kweli havijakaa vyema, bora wapeleka Ethiopia kuna njaa kali lakini siyo Tanzania ambayo mazao mengi yamevuniwa. Wapo watu wanakula mlo mmoja Sidhani tukawasaidie

National food reserve inafanya nini hadi akina Ndugai wanakwenda kuomba misaada nje wa chakula?
 
Hivi virutubisho vinawafanya watoto kukosa homoni za kiume na kuzidisha homoni za kike......uzuri hata wizara haitapima

Wazazi acheni kupenda misaada waleyeni watoto wenu wenyewe
 
Hivi virutubisho vinawafanya watoto kukosa homoni za kiume na kuzidisha homoni za kike......uzuri hata wizara haitapima

Wazazi acheni kupenda misaada waleyeni watoto wenu wenyewe
Hizi ni propoganda tu, hakuna kitu kama hicho
 
Wengine miaka ya sitini tulikunywa sana maziwa shule zote za msingi std 1 to 4 kwa hisani ya watu wa Marekani
Miaka ya sabini tulikula sana sembe la njano kwa hisani ya watu wa Marekani
Siku hizi tunasikia matangazo ya afya na elimu kwa nini hisani ya watu wa Marekani.
Hata hivyo shida ya lishe imezungumzwa sana na Proffesa Lipumba, na mafuta ya Singida watu wa Bahi hawamudu kununua.
 
Waziri hana nguvu yoyote,wapo wenye mbwa ndiyo wenye maamuzi. Bashe ni kama kiroboto tu kwa wenye mbwa
 
Majambazi yaliyopo kwenye ofisi za uma, tayari yameshajipanga na mifuko mipya. Mchele na hayo mafuta yatasambaa nchi nzima kwa majina mapya...."Anaupiga Mwingi Cooking Oil"
 
Back
Top Bottom