Je, Rais ana mamlaka ya Kumvua Mtu "Ubunge"?

Ukiteuliwa kuwa balozi. Then the public Service Act inasema balozi haruhusiwi kichika nyadhifa yoyote ya kisiasa serikalini. Then automatically Possi anatakiwa kujivua ubunge. Pia katiba katika ibara ya 67 (2)g ambayo inakataza maofisa waandamizi wa serikali kuwa wabunge hivyo possi anapoteza sifa ya kuwa mbunge
Lakini bado haifuti ukweli kwamba possi alikwishateuliwa kuwa mbunge miongoni mwa zile nafasi kumi.. Kwa maana kwamba possi amekula nafasi moja kati ya zile kumi za rais,kwahiyo hapa kama bulembo na prof kabudi wakiapa kuwa wabunge bado ibara ya 66(1)(e) itakuwa imekiukwa!
 
Taifa linapita katka wakat mgum sana watanzania tuliombee, limekua taifa km vile tumetoka msituni juzi hatuna katba wala sheria, duuu atar!!! Malaika huyu tuliyempata hana mfano
 
Ni takribani mwaka mmoja baada ya Dkt Abdalah Possi kuteuliwa kuwa Mbunge na naibu waziri, ofisi ya waziri mkuu sera, bunge, kazi,vijana, ajira na walemavu.

Ni dhahiri kabisa Dkt possi hajatosha na katumbuliwa kwani kuwa mbunge na nafasi aliyokuwa nayo ya unaibu waziri hadi kushushwa kuwa balozi ni nafasi tatu tofauti kabisa nikimaanisha ubunge, uwaziri na ubalozi.
Dkt Abdalah Possi hapa umeshushwa viwango! Kaa chini ujitafakari kwa iyo nafasi uliyopewa haifanani na wadhifa uliokua nao!

Naamini hautatuangusha na utatunza heshima yako, hakika umetolewa sadaka baada ya katiba ya jamhuri kukanyagwa!

Tunasubiri kauli yako mh Dkt
 
Kwanza tujiulize wale wateuliwa wa enzi zileeee walikuwa na cheo cha ubunge at the same time waliteuliwa kuwa wakuu wa mkoa.., nafasi zao za ubunge zilikoma au kikatiba ikoje.., mfano kama sikosei ni stela manyanya
 
Pamoja na Rais kumteua Mhe. Posi kuwa balozi lakini ubunge wake unabaki pale pale!

Hivyo bado kuna wabunge 6 wa kiume ambao Rais ameteua kinyume cha katiba!!

Katiba imevunjwa huo ndiyo ukweli na hatua za kumwajibisha Rais zinapashwa kuanza kuchukuliwa!!

Rais aliapa kulinda katiba lakini sasa amekiuka! Sheria ni msumeno unakata mbele na nyuma!!!
kazi IPO,
 
Rais hana mamlaka ya kumvua yeyote ubunge; Huu ni mchezo umechezwa baada ya yeye kuchemka kwenye teuzi, hivyo kilichofanyika ni namna ya kupunguza idadi ya wabunge walioteuliwa ili kuleta uwiano kama katiba inavyosema, hivyo Posi atalazimika kujiuzulu ubunge wake!!
Tuangalie ibara hii kwenye katiba..
* Ibara ya 71*

Mbunge atakoma kuwa Mbunge na ataacha kiti chake katika Bunge litokeapo lolote kati ya mambo yafuatayo-

(a) ikiwa litatokea jambo lolote ambalo, kama asingekuwa Mbunge lingemfanya asiwe na sifa za uchaguzi au apoteze sifa za uchaguzi au asiweze kuchaguliwa au kuteuliwa kwa mujibu wa masharti ya Katiba hii;

(b) ikiwa Mbunge huyo atachaguliwa kuwa Rais;

(c) ikiwa Mbunge atakosa kuhudhuria vikao vya Mikutano ya Bunge Mitatu mfululizo bila ya ruhusa ya Spika;

(d) ikiwa itathibitishwa kwamba amevunja masharti ya Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma;

(e) ikiwa Mbunge ataacha kuwa mwanachama wa chama alichokuwamo wakati alipochaguliwa au alipoteuliwa kuwa Mbunge;

(f) iwapo Mbunge anachaguliwa au anateuliwa kuwa Makamu wa Rais;

(g) kwa Mbunge ambaye anatakiwa kutoa taarifa rasmi ya mali kwa mujibu wa masharti ya ibara ya 70, ikiwa atashindwa kutoa hilo tamko rasmi kwa mujibu wa masharti ya hiyo ibara ya 70 katika muda uliowekwa mahususi kwa ajili hiyo kwa mujibu wa sheria iliyotungwa na Bunge

*lakini iwapo Mbunge hatakoma kuwa Mbunge kwa mujibu wa jambo lolote kati ya mambo hayo yaliyotajwa na kama hatajiuzulu au kufariki mapema zaidi, basi Mbunge ataendelea kushika madaraka yake kama Mbunge mpaka wakati Bunge litakapovunjwa kwa mujibu wa ibara ya 90, bila ya kuathiri haki na stahili zinazotokana na ubunge wake*
 
Back
Top Bottom